PDA

View Full Version : Itakuwa tumerogwa!



mwanakijiji
02-26-2009, 09:12 AM
Sisi ndiyo watu wa ajabu kweli duniani. Tumeumbwa kuamini geresha na ndani yetu kuna visumaku vya kukubali maneno matamu na ahadi zenye "nia nzuri".

Yaani, hawa hawa ambao hadi leo hii hawajatoa maelezo ya Kagoda tunataka tuamini kuwa leo wameokoka na wana nia nzuri!

Yaani, hawahawa ambao hawajamaliza suala la rada tunataka kuwapa la kitambulisho

Yaani, hawahawa ambao hawajamaliza la Minara Pacha, leo wanakuja na mradi mwingine tunatakiwa tukumbatie kwa sababu "una lengo zuri"!

Yaani, hawa hawa waliotuingiza kwenye Richmond kwa lengo zuri la kutupatia umeme ndiyo hawa hawa tunaambiwa tukubali tu kwa vile wana "mshauri mzuri!"

Yaani, hawahawa ambao hadi leo hii hawajatuelezea Shilingi trilioni moja iliyokwapuliwa BoT imeenda wapi, leo tunatakiwa tukubali wachukue bilioni 200 kwa mradi "muhimu wa TAifa!"

Yaani, hawahawa ambao wanataka kujenga flyover Dar, wanakuja na mradi mabasi yaendayo kasi lakini wameshindwa kufunga taa za kuongozea magari karibu kila kona za Jiji la Dar au miji mingine ati tunatakiwa tuwashangilie na mradi wa vitambulisho!

Yaani, hawahawa?

Kuna uwezekano sisi tumerogwa, tunaumwa au tunawazimu!!! Nawaandikia barua... maana kama ni uhuni huu ndiyo halisi.. yes I mean Uhuni!!