PDA

View Full Version : Tununue tu mitambo ya Dowans?



mwanakijiji
02-27-2009, 04:44 PM
Nadhani kuna kuzungushana hapa; kwanini tusiamue kuinunua hii mitambo ya Dowans ili yaishe?

Atubonekisye Massapa
02-28-2009, 10:16 AM
what do you expect? The deal is concluded and you better shut up! Unafanya dua ya kuku? Namhurumia Dr Mwaky.... alidhani amefanya kazi nzuri, kumbe wapi bwana yale yale ya Githongo....Nji Hii bwana we acha tu.

Mpita Njia
02-28-2009, 10:58 AM
Nadhani kuna kuzungushana hapa; kwanini tusiamue kuinunua hii mitambo ya Dowans ili yaishe?

Ni uamuzi mzuri vilevile provided utatupatia muda wa kufikiria masuala mengine kwani hili litakuwa limemalizwa. lakini, doesnt it mean accepting defeat?

Ach-F
02-28-2009, 02:59 PM
Sioni sababu yoyote ya kununua mitambo iliyo kongoroka (second hand). Kutokana na uchumi wa dunia jinsi unavyoshuka unaweza kupata mitambo mipya miwili kwa bei ya mtambo moja. (Buy one get one free). The principal issue being, the Government or any Parastatal Organisation should follow proper laid down procedures of tendering.

Mpita Njia
02-28-2009, 03:25 PM
Sioni sababu yoyote ya kununua mitambo iliyo kongoroka (second hand). Kutokana na uchumi wa dunia jinsi unavyoshuka unaweza kupata mitambo mipya miwili kwa bei ya mtambo moja. (Buy one get one free). The principal issue being, the Government or any Parastatal Organisation should follow proper laid down procedures of tendering.

Tatioz ni kuwa hawa wenzetu hawaangalii urahisi wa bei (ingawa hilo wanalisema katika hoja zao) lakini lengo ni kuhakikisha kuwa serikali inanunua mitambo hiyo kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu

hofstede
03-02-2009, 08:11 PM
Mkjj kama ulivyotuhabarisha mwanzo kuhusu hawa Richmond printing, hebu fuatilia mitambo hiyo inauzwaje ikiwa mipya, maana suala la kusema kununua iliyopo au kuagiza ya kukodi ni sawa na mchezo wa kujificha, kombolela. Kama tuna hela za kununua ya zamani kwa nini tusinunue mipya ?, hapa inatakiwa kuwa makini kabla kopo halija butuliwa, vinginevyo tuwaambie kombolela, yaani tumewaona kabla hawaja butua kopo.

Haiingii akilini kabisa kwa hawa Tanesco katika mpango huu, hapa someone anahofia mitambo hii kuoza kwani haina soko kokote duniani zaidi ya Danganyika.

911
03-02-2009, 09:12 PM
Mh Zitto naye kashupalia ununuzi wa hyo mitambo ya Dowans via kukutana kwa kamati mbili!!Hii inatia shaka sana.

Dua
03-03-2009, 12:53 AM
Who the hell is Tanesco. Hivi Tanzania bado tunajivuna tuna viongozi? The buck should stop with the President himself haiwezekeni mazingaombwe kama haya yaendelee bila yeye mwenyewe kuwa mshiriki katika kufilisi pesa za walipa kodi under his nose.

mwanakijiji
03-05-2009, 06:24 PM
Saed Kubenea - MwanaHALISI

Kelele za sasa ndani ya serikali kuhusu Ununuzi wa mitambo ya Dowans ni jitihada zinazolenga ?kukidhi mslahi binafsi?,MwanaHALISI limegundua.

Vyanzo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam na mikoani vimeonesha kuwa hakuna tatizo la umeme hivi sasa nchini; wala hakuna upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme.

Uchunguzi wa gazeti hili sasa unathibitisha kuwa madai ya serikali kwamba nchi karibu itaingia gizani kutokana na ukosefu wa meme, hayana msingi wowote. Kwa wiki nzima sasa serikali, ikishirikiana na Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) wamekuwa wakitoa tahadhari kuwa iwapo mitambo ya umeme ya kampuni ya Dowans haitanunuliwa mara moja, taifa litaingia gizani wakati wowote kuanzia sasa.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema serikali ina nia ya kununu mitambo ya Dowans ili kukabiliana na tishio la uhaba mkubwa wa umeme kutokana na mabwawa kukauka.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Dr. Idris Rashid amesema kwamba mahitaji ya umeme yameongezeka nchini na kwamba kinachohitaji ni serikali kununua mitambo yote ya Dowans pamoja na vifraa vyote vya kuunganishia kwenye gridi ya taifa.

Hata hivyo, taarifa ndani ya Tanesco zinasema vyanzo muhimu vya nishati hiyo, ambavyo ni mabwawa ya maji, bado viko imara na maji yako kwenye viwango thabiti vya kuzalisha umeme. Kwa mfano, hadi juzi Jumatatu bwawa la Mtera mkoani Dodoma lilikuwa na maji ya kutosha ya kuzalishia umeme.

Kima cha juu cha ujazo katika bwawa la Mtera ni mita 698.50 na kina cha chini kwa ajili ya uzalishaji umeme ni mita 690. Lakini hivi sasa Mtera ina ujazo wa mita 695.91. Hii ina maana kwamba kile kinachoitwa ?tishio ma mabwawa kukauka? hakipo hatika bwawa hilo Kinachoonekana kuwa upungufu, wataalamu wamesema hakiwezi kuleta athari yoyote kubwa katika miezi ya karibuni.

Hali kama hiyo ipo katika bwawa la Kidatu Mkoani Morogoro. Hadi juzi Jumatatu, maji katika bwawa hilo yalikuwa mita 449.37. Kima cha juu cha maji kwa Kidatu ni mita 451 huku kima cha chini ni mita 441.

?Kwa maana hiyo, mpaka sasa na kutokana na takwimu hizi hakuna ushahidi wa mabwawa hayo kukauka au kuwa hatarini kukauka?. Amefafanua injinia mmoja wa Tanesco makao makuu Dar-es-Salaam.

Aidha, Mamlaka ya Hali ya Hewa imetangaza kuwa mvua kubwa zimeanza kunyesha katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga. Watalaa wa Tanesco wanasema ni mvua ambazo zitajaza mabwawa ya Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Kidatu na Hale kabla ya miezi ya Machi na Aprili mwaka huu.

?Kwa mvua hizi zinazonyesha? kimeeleza chanzo chetu cha habari, ?huenda zikalazimu Tanesco kuachia kingo za mabwawa na kuachia maji yatoke ili kuzuia yasibomoke.? Hadi Jumapili iliyopita Waziri Ngeleja alikuwa ameanza kampeni kubwa akidai kuwa kununua mitambo ya kuzalisha umeme ya Dowans ?siyo kufanya ufisadi? bali ni kuweka maslahi ya taifa kwanza.

Katika wimbo huo, Ngeleja aliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirikika ya Umma, Zittoa Kambwe ambaye alisema anaweka mbele ?maslahi ya taifa?. Lakini ni Ngeleja aliyeliambia Bungeni zaidi ya miezi mitatu iliyopita kuwa serikali haiwezi kununua mitambo hiyo kuwa imetumika na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Ununuzi aw Vifaa na Huduma serikalini kwa mwaka 2004.

Katika haraka isiyo ya kawaida serikali na Tanesco wametupilia mbali ushauri wa Kamatti ya Nishati na Madini zya Bunge na kudandia Kamati ya Zitto wakidai wanatafuta Bunge kuwaruhusu kununua mitambo ya Dowans. Kamati ya Nishati na Madini ilishauri Tanesco kufanya kile ambacho wanaona kimo katika uwezo na uamuzi wao. Dowans ni sehemu ya sakata la Richmond ambalo maazimio ya Bunge juu yake hayajatekelezwa na serikali.

Hatahivyo, bado serikali inakabiliwa na mgogoo wa nani hasa wajadiliwe naye katika kununua mitambo ya Dowans iliyoko Ubungo, Dar-es-Salaam. MwanaHALISI imebaini kuwa wakati kampuni ya Dowans ilikuwa inaweka mitambo yake na baada ya kuanza uzalishaji, haikuwa na ofisi nchini na wala mmiliki wake halisi alikuwa hajulikani.

Hadi sasa, Bunge ambalo liliunda Kamati Teule kuchunguza mkataba wa kampuni ya Richmond iliyokabidhi shughuli zake kwa Dowans, halifahamu mmiliki wa Dowans. MwanaHALISI imegundua kuwa kuna kampuni inayoitwa Dowans Holdings SA (DH-SA) iliyosajiliwa nchini Costa Rica America ya Kusini tarehe 1 Julai, 2005 na kwamba ndiyo yenye uhusiano na Dowans iliyoko Ubungo.

Kampuni ya DH-SA ilianzishwa na mtu mmoja aitwaye Bernal Zamora Alce. Taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo gazeti hili limeona, zinaonesha Zamora alijitangaza kuwa mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi katika makampuni 52. Hata hivyo, pamoja na utilili huo wa makampuni imefahamika kuwa Zamora hana simu ya mkononi, hana sanduku la barua wala hajulikani mtaa anakoishi (kagoda??)

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari wa kimataifa na wanasheria mashuhuri nchini Costa Rica umegundua kwamba kampuni ya Dowans haikuwa na ofisi nchini humo haikuwa na simu wala gari. Si nchini Costa Rica tu bali kampuni ya Dowans yenye mitambo Ubungo kwa mujibu wa taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, haikuwa na namba za simu wala ofisi, wafanyakazi wake walikuwa wanatumia ofisi za kampuni ya Caspian Limited hapa nchini.

Kampuni ya Caspian inamilikiwa na mfanyabiashara na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz. Ni Rostam aliyethibitishia Bunge kuwa Dowans ilikuwa inatumia anuani zake. Katika andishi lililotumwa serikalini na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Costa Rica, kuitahadharisha serikali ya Tanzania kuhusu Dowans anasema, ?Dowansni kampuni ya mfukoni iliyoanzishwa mahususi kwa ajili ya kufanya kazi maalum?.

Katika mazingira haya, Dr. Rashid apoulizwa Tanesco inajadili na nani kuhusu ununuzi wa mitambo, alijibu haraka wao hawafanyi majadiliano bali wamepeleka mapendekezo serikalini. Alisema ni serikali yenye jukumu la kununua au kutonunua mitambo hiyo.

Alipoulizwa sasa serikali itajadiliana na nani wakati mmiliki wa Dowans hajajulikana, Dr. Rashid alisema ?hayo si yangu, ni mambo ya wanasiasa. Sisi tumetoa ushauri kwa serikali kwamba tunataka mashine za kuzalisha umeme.? Alipoulizwa kwa nini Tanesco isishauri serikali kutaifisha mitambo ya Dowans, kwa hoja kwamba kampuni hiyo ilitapeli serikali kwa kurithi mkataba wa Richmond kienyeji alisema, ?hilo siwezi kulizungumzia.?

Waziri Ngeleja hakupatikana kujibu swali kwanini Tanesco inataka serikali kufanya mazungumzo na Dowans badala ya kuingia katika mchakato wa zabuni

Dua
03-06-2009, 02:08 AM
Huyo Dr sijui nani tulisema kabla hawajampa hiyo nafasi hafai hawakusikia sasa hata akijiuzulu ni sawa na maji yaliyomwagika ni kilaza flani hivi aliye bahatika kukalia hiyo nafasi.

Serikali iko likizo kila kukicha badala ya kutatua matatizo ya walipa kodi ni kushughulikia Ufisadi wao waliouzaa. Ati wamefungua kesi ya kuishitaki serikali hivi Mkuu wa nyumba bado hajalipa madeni yake?

mwanakijiji
03-06-2009, 04:27 PM
Sijui wamefikia wapi? Ngoja tufuatilie mambo haya..

Keil
03-06-2009, 04:32 PM
Dua,

Dr. Rashidi siyo kilaza, tatizo lake kubwa ni kwamba fisadi. Sifahamu madudu aliyoyafanya alipokuwa CEO wa NBC kabla hajateuliwa kuwa Gavana wa BOT.

Akiwa BOT alikula hela za Debt Conversion Program (DCP) ambayo ni kama EPA ya leo na nina mashaka sana dili za EPA ni yeye aliwashitua wajanja kwamba kuna pesa za bure bure ziko ziko tu na zinaweza kutafunwa bila watu kujua. Kasheshe ya Chavda kwa kiasi kikubwa inamgusa Dr. Rashidi wakati akiwa BOT.

Tayari tumeishaambiwa kwamba kwenye dili la Rada pia alipewa mgao wake.

Tatizo la mashirika yetu ni UONGOZI, viongozi tunaopewa kwa kuwa wanateuliwa na Rais na hivyo kuwajibika kwake zaidi, wanajikuta wanatanguliza maslahi binafsi. Sasa ukiweka mtu mwenye sifa za ufisadi kama Dr. Rashid unategemea nini?

Anyway, ngoja tuone next atafanya nini na huyo Rostam wake.

Keil
03-06-2009, 04:40 PM
Kwa wenye utalaam wa sheria, hivi PPRA wanaposema kwamba opinion ya Rais ni amri wana maana gani?

Ina maana Rais anaweza kushauri sheria zipindishwe na asiulizwe? Je, tutajuaje kama sheria hiyo anaipindisha kwa maslahi yake ama kwa maslahi ya Taifa?

Inafika mahali ninakata tamaa kabisa na hawa watalaam wetu, nilitegemea kwamba PPRA wangekuwa wa kwanza kupinga kupindisha sheria kwa sababu fulani fulani mpaka ufanyike uchunguzi wa kina ili kuona kama kweli kuna maslahi ya Taifa au la na si vinginevyo.

mwanakijiji
03-06-2009, 04:41 PM
Kampuni ya Tanesco imejitoa rasmi katika mchakato wa kununua mitambo ya Dowans kwa kudai kuwa suala hili limeingiza malumbano makali ya wanasiasa. Katika kujitoa kwake kampuni hiyo imesema kuwa siku nchi ikiingia kizani wasilaumiwe wao kwa sababu watu walishindwa kufanya maamuzi magumu.

Habari ndiyo hiyo, nyamanyama na mafuta mengine baadaye!

LAKINIWEWE
03-06-2009, 07:07 PM
......nina mashaka kunaweza kufanyika hujuma siku za karibuni ktk uzalishaji wa umeme, ili isemekane kuwa, TULIWAMBIA TUNUNUE MITAMBO YA DOWANS mkakataa, sasa mnaona?????

mwanakijiji
03-06-2009, 10:28 PM
Joseph Lugendo
Daily News; Friday,March 06, 2009 @20:00

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) , Dk. Idris Rashidi, ametangaza uamuzi wa kujitoa kwa shirika hilo katika nia ya kununua mitambo ya kufua umeme ya Dowans.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kutolewa taarifa alizodai kuwa ni za uongo na zilizojaa utashi wa kisiasa zaidi, dhidi ya utaalamu wa Tanesco na kwamba zimechangia kuvunja nguvu ya mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo wanaofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha nchi inapata umeme wa uhakika.

Akisoma uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya Tanesco, Dar es Salaam leo, Rashidi alisema kuwa taarifa hizo zilinukuliwa na vyombo vya habari katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kutoka kwa wanasiasa, wananchi waandamizi aliowaita kwa Kiingereza kuwa ni 'Senior Citizens' na watu wazito wenye majukumu na dhama kubwa.

Aidha, Rashidi ambaye alikataa kuulizwa maswali na kuwataka waandishi kuvuta subira mpaka muda wa maswali na majibu utakapofika bila kutaja siku wala saa, alionya kuwa sasa wananchi ndiyo watakaofanya uamuzi wa mwisho.

"Ni imani yetu kwamba tumeshajieleza na kujenga hoja za kutosha, na umma wa Watanzania utafanya uamuzi wao wakati nchi itakapokuwa imegubikwa na giza, hospitali hazitoi huduma, viwanda havizalishi na wanafunzi vyuoni wakishindwa kusoma," alisema Rashid.

Kwa mujibu wa Rashidi, Desemba 2008 Tanesco iliwasilisha tathmini ya hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini, iliyoainisha mahitaji na matarajio ya uzalishaji kwa muda wa kati na mrefu. Taarifa hiyo iIionyesha kuwa, kwa wakati huo upungufu wa nishati ya umeme ulikuwa megawati 150, na kwamba ukuaji wa mahitaji ya nishati hiyo ni megawati 75 kila mwaka.

Ilijenga hoja alizoziita kuwa ni za kitaalamu na si za kuangalia upepo wa kisiasa, kwamba kutokana na hali ya upungufu uliokuwapo, na ongezeko la mahitaji kwa kila mwaka, ifikapo Desemba 2009, Tanzania itakuwa ikikabiliwa na upungufu wa megawati 225. Alisema tathmini ya hali ya mvua ambayo ndiyo chanzo cha umeme mkubwa kuliko wote na nafuu zaidi, iliyotokana na utabiri wa hali ya hewa, ilionyesha kuwa mvua za mwaka huu hazitalingana na viwango vya kawaida.

Kwa mujibu wa Rashidi, tayari mvua katika mikoa ya Mbeya na Iringa, ambayo ndiyo vyanzo vikuu vya maji ya Bwawa la Mtera, ni za kiwango cha chini na katika maeneo mengine zimesimama. Hoja hiyo ilifafanua kuwa Tanesco ilikuwa na mpango wa mwaka 2009 wa kukamilisha miradi miwili ya kuzalisha umeme ukiwamo wa Kiwira uliokuwa uzalishe megawati 200 na wa Tegeta megawati 45.

Hata hivyo kwa mujibu wa Dk. Rashidi, mradi wa Kiwira uliathirika kwa alichoita kuwa ni malumbano ambayo yamesababisha wawekezaji wakubwa waliotarajiwa kushiriki, kujitoa. Pia mradi wa Tegeta ambao katika mipango ya Tanesco, ulikuwa uanze kuzalisha umeme mwaka huu, umechelewa na sasa utaanza uzalishaji Oktoba 2009.

Kutokana na hoja hizo, Tanesco ilifanya tathmini ya zabuni ya Dowans ya kuuza mitambo yake iliyotangazwa kwenye vyombo vya habari mwaka jana, na kupeleka mapendekezo wizarani ya kununua mitambo hiyo, kwa kuzingatia kuwa haitoshi kupeleka taarifa ya tatizo la uzalishaji wa nishati na mahitaji, bila mapendekezo ya ufumbuzi wa suala hilo.

Mapendekezo hayo yalizingatia pia unafuu na ubora wa mitambo ya Dowans, na yalitolewa kwa tahadhari kwa nia ya kuepusha Tanesco kuingia kwenye mtego usiokwepeka, wa kukodi mitambo hiyo wakati nchi ikiwa kwenye giza katika siku za usoni. Aidha, huku ikijua kuwa ununuzi wa mitambo hiyo si ufumbuzi kamili wa tatizo hilo, Tanesco iliishauri serikali kukaa na wataalamu wa shirika hilo kujadili mpango wa haraka kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa megawati zisizopungua 200, katika kipindi cha miezi 24 tangu Desemba 2008.

Mjadala huo ulikuwa ulenge katika kuharakisha baadhi ya miradi iliyochelewa kuanza ya Kiwira, Tegeta na Ruhuji ambao ni wa maji megawati 350 na mwingine wa Mnazi Bay wa gesi megawati 300. Mtendaji huyo wa TANESCO alisema miongoni wa 'Senior Citizens' wanaodaiwa kupotosha umma, walipata nafasi ya kukaa na Tanesco kubadilishana mawazo kuhusu hali ya umeme, na mara zote shirika hilo limekuwa likieleza kuwa litakuwa tayari kupokea maelekezo kutoka Kamati za Bunge na Serikali kwa kuwa ndizo taasisi za usimamizi na za uwakilishi wa wananchi.

Alisema, "Hivi karibuni kiongozi mmoja amenukuliwa akisema jitihada hizi ni za kusafisha mafisadi, ni kukiuka taratibu za nchi". Rashid alifafanua kuwa kiongozi huyo hakuwa sahihi kwa kuwa hakuna wakati wowote ambao Tanesco ilisema kwamba ununuzi wa mitambo hiyo hautazingatia taratibu husika za kisheria.

Alisema mitambo hiyo haiuzwi dukani kama mavazi au trekta na kutoa mfano wa mtambo wa Warstsila ambao ulinunuliwa kwa dharura ambapo taratibu zote kuanzia zabuni mpaka kupatikana kwa nishati, ilichukua miezi 18, wakati kwa sasa Tanzania inatakiwa kupata mitambo ya dharura ili Septemba nchi isikumbwe na giza. Uamuzi wa Tanesco kujitoa katika ununuzi wa mitambo hiyo, unatokana na mjadala ulioibuka baina ya wanasiasa juu ya hatua hiyo. Mjadala huo ulitokana na kitendo cha Kamati mbili za Kudumu za Bunge kukinzana katika ushauri juu ya ununuzi huo.

Kamati ya Nishati na Madini ikiongozwa na William Shelukindo (CCM) ilishauri serikali isiruhusu Tanesco kununua mitambo hiyo wakati Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma chini ya Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe (CHADEMA) iliunga mkono ununuzi. Hali hiyo ilisababisha Spika wa Bunge, Samuel Sitta kuingilia kati na kutoa mwongozo ambao kwa upande wake, alikuwa akiitahadharisha serikali juu ya uamuzi huo wa kununua mitambo inayodaiwa kuwa imeshatumika.

Wakati huo huo, Theopista Nsanzugwanko anaripoti kuwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeisisitiza serikali ifuate na kuheshimu Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa kutafuta mitambo mipya kutatua tatizo la umeme nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Francis Kiwanga alisema nia ya TANESCO na Serikali ya kununua mitambo hiyo ya kampuni binafsi ya Dowans ambayo ni ya mitumba, ni kinyume na sheria na misingi ya utawala bora.

Alisema jitihada hizo zinakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 na kutengeneza msingi wa uvunjaji wa sheria. ?Kuhusu malumbano ya Bunge na Serikali kuwa ibara ya 63(2) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inalipa Bunge madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba? alisema Kiwanga.

Ohotaite
03-07-2009, 03:45 PM
Ndugu Mtanzania Halisi. Nakuheshimu. Inawezekana kweli uko nje ya nchi au la. Sina uhakika. Hapa mimi nafikiri hatuongei siasa. Tatizo la Watanzania ni ama kusahau haraka ama kutoweka kumbukumbu za maandishi kama vile magazeti. Mimi simfahamu Daktari Rashid na sina ugomvi nae ila kama yeye au mtu yeyote akinipa majibu mazuri kwa maswali haya nitashawishika:
1.Kamati ya Mwakyembe ilitoa taarifa mwezi Februari 2008. Je ni tarehe ngapi TANESCO ilianza kufikiria kuvunja ndoa na DOWANS bin RICHMOND?
2. Ndoa ilivunjika rasmi tarehe 1 August 2008. Je Dk. IDRISA alishauri nini kifanyike baada ya hiyo ndoa kuvunjika?
3. Kwa nini Dk. Rashid alikaa kimya toka August hadi Jumamosi ya tarehe 28 Feb 2009 ndiyo anakuja na wimbo au ngonjera ya dharura?
4. Nini kiliisukuma TANESCO kufanya ukaguzi wa mitambo ya Dowans? Au walishafanya uamuzi wa kuinunua?
Wakati nasubiri majibu naomba kutoa ushauri kwamba KAMA TUNATAKA MITAMBO ILIYOTUMIKA BASI TUTANGAZE TENDA YA KUTAKA MITAMBO AINA HIYO NA WATU WAOMBE AKIWEMO DOWANS.
Nasubiri majibu.

Ohotaite
03-07-2009, 03:52 PM
Kwa wenye utalaam wa sheria, hivi PPRA wanaposema kwamba opinion ya Rais ni amri wana maana gani?

Ina maana Rais anaweza kushauri sheria zipindishwe na asiulizwe? Je, tutajuaje kama sheria hiyo anaipindisha kwa maslahi yake ama kwa maslahi ya Taifa?

Inafika mahali ninakata tamaa kabisa na hawa watalaam wetu, nilitegemea kwamba PPRA wangekuwa wa kwanza kupinga kupindisha sheria kwa sababu fulani fulani mpaka ufanyike uchunguzi wa kina ili kuona kama kweli kuna maslahi ya Taifa au la na si vinginevyo.

Zaidi ya hayo hao PPRA kama walikuwa wakiona kuna mapungufu katika sheria wanayoisimamia tungetarajia wawe wa kwanza kutoa ushauri huo badala ya kysubiri yasemwe na Rais na mara wanadandia. Tatizo la viongozi wetu hawawezi kufanya kazi mbadala wa zile wanazofanya sasa. Anajiuliza je nikikosa kibarua nitakuwa mgeni wa nani. PPRA mlitakiwa kutoa ushauri mapema.

Dua
03-09-2009, 12:17 AM
Keil

Ukilaza alionao Idris ni wa kuliongoza shirika la umeme. Angekuwa sio kilaza kwanza asingekubali kuendeshwa kama gari bovu. Ni sawa na ulivyosema madudu yote ya EPA ni ya kwake. Tanzania iko siku moto utawaka sijui watatokea wapi. Sheria zipo lakini kila uchwao kuna utitiri wa mazingaobwe.

Ohotaite

Hawawezi kujibu maswali hayo madogo wanasubiri utokee mujiza.

Mwanakijiji


Hata hivyo kwa mujibu wa Dk. Rashidi, mradi wa Kiwira uliathirika kwa alichoita kuwa ni malumbano ambayo yamesababisha wawekezaji wakubwa waliotarajiwa kushiriki, kujitoa.

Wanasubiri ati wafadhili wakubwa? Hivi huu ulimbwende utaisha lini? Wafadhili wakubwa ni Watanzania na wapo, hivi wanaposikia Ulaya na marekani wanachapisha pesa basi ndio wanawasujudia? Wawekezaji wakubwa ndio wanaotufilisi damn, Wakiamua kuuza shares za Tanesco kwa WTZ wenyewe wataona jinsi zitakavyopokelewa, hii yote ni dharau kwa walipa kodi kutoka kwa waliopewa dhamana ya kuongoza.

dRU
03-09-2009, 11:06 AM
Ama kweli "Meno ya mbwa hayaumani". Sidhani kama kuna haja ya kulieza hili kwa undani zaidi maana tunayaona. Hapa Dr Idrisa hatoki na ataendelea tu kutoa kauli zake tata na huwa hakawii kususa... (thithi kwetu tungemuita CHIKIRA).