View Full Version : Unasemaje ya dc yamungu
dickabudi
03-02-2009, 01:45 PM
DC Yamungu amekanusha maneno ya kwamba anaungana na Mnali kuona adhabu ya viboko kwa Waaalimu ilikuwa sahihi nini cha kweli kuhusiana na taarifa hizo?
Tafsiri yake kwa haraka inaonyesha jinsi gani uandishi wa habari wa Tanzania unavyojikita kwenye upotoshaji mwaonaje wanakijiji
hofstede
03-02-2009, 03:16 PM
Tatizo kwa muda mrefu nchi imekuwa ikiteua hawa viongozi kwa kuangalia maslahi binafsi. Mfano baada ya uasi wa jeshi mwaka 1964, viongozi wetu waliona njia pekee ya kutuliza nchi ni kuwashirikisha wanajeshi katika uongozi na kuanza kuwapa vyeo vya ukuu wa mikoa na wilaya. Hii ilisaidia ila kwa wakti huu mambo yamebadilika sana, democrasy imekuwa na haki za binadamu zinaheshimiwa, sasa unapompa mtu alikuwa trained kuuwa (mjeshi) kuongoza raia wasio na silaha ni lazima atakuwa na mtazamo wa kijeshijeshi tu. Jeshini wanapigana viboko sana, ila mbinu hii ukiitumia uraiani hueleweki. Hawa wote Yamungu na Mnali ni wanajeshi. Umefika wakati sasa kuteua viongozi kulingana na hali halisi ya sasa na si kuwapatia wanajeshi kwa kuogopa uasi. Unapompa mwanajeshi hati ya kutawala raia ni lazima atawapeleka kijeshijeshi. Either hawa wanajeshi wapewe mafunzo ya kudeal na raia au wasipewe nafasi yoyote ya kudeal na raia wakati wa udikteta umepita kwa hiyo hawa askari kwa sasa kuwapa uongozi ni kuwaonea tu kwani ni kinyume na mafunzo yao.
Kama hao waandishi watakuwa na audio recording ya hayo mazungumzo ndo tutajua yupi hasa ni mkweli.Kwa maana ni rahisi kwa mtu kuyakana/kuyaruka maneno yake hasa kama ameona kuwa kuna uwezekano wa kum_backfire.
Mpita Njia
03-03-2009, 01:08 PM
Kama alivyosema 911, ni vigumu kwa sasa kujua nani anasema ukweli kati ya mwandishi na huyu mzee Yamungu *(sijui ni mzee kweli au vipi)
mwanakijiji
03-03-2009, 05:11 PM
mi bwana hata sielewi:
a. Masha alinukuliwa kusema kuwa hawajui kabisa SAGEM wala hajawahi kukutana nao maishani mwake. Masaa machache baadaye akanukuliwa kusema kuwa anawajua na amekutana nao japo alisema kuwa si nje ya nchi.
b. Vyombo vya habari vikaripoti kuwa JK amewashukia viongozi wastaafu na kuwataka wakae kimya wakiiga mfano wa Kawawa ambaye hajajitokeza kukosoa walio madarakani. Siku mbili baadaye gazeti jingine likasema Kawawa asema CCM na viongozi wa serikali wasifanya mambi ya maslahi ya kibinafsi n.k Wote wawili tunaambiwa walikuwa kwenye tukio hilo hilo moja walipoyasema hayo waliyonukuliwa kusema!
c. Sasa hili la Mnali na Yamungu nalo ndiyo kabisa.. Inakuwa ni kama suala la Pinda na mauaji ya "papo kwa papo"!
Ach-F
03-07-2009, 02:44 AM
Mzee Mwanakijiji usikonde watakuletea habari za popo bawa.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.