mwanakijiji
03-02-2009, 07:28 PM
Sema Usikike - Mwandishi Maalum
Kama tungekuwa tunatafuta mzungumzaji wa Kiingereza sanifu chenye lafudhi ya Kimarekani, hapana shaka, Lawrence Kego Masha, ndiye mtu safi kwa nafasi hii, kwani katika vitu ambavyo anaviweza hiki kikubwa zaidi anachojivunia.
Lakini kwa bahati mbaya sana, watu wengi hasa wakaazi wa Nyamagana mkoani Mwanza na Watanzania walio wengi hawamjui vizuri Masha Mbunge na Waziri wa Mambo ya Ndani ni mtu wa namna gani.
Namfahamu Masha tangu akiwa kinda Marekani, baadaye Chuo Kikuu Dar-es-Saalam na hatimaye jijini mwanza alipojiunga na siasa, lakini nilikitaa kumuunga mkono pamoja na kuwa ni ndugu wa karibu, kwa sababu namfahamu udhaifu wake kuliko anavyojijua yeye.
Naandika makala haya sina chuki wala kinyongo naye lakini nimesukumwa na kauli zake za hivi karibuni kuhusu albino, sakata la Reginald Mengi, Deep Green na Vitambulisho vya uraia.
Tatizo kubwa la Masha ni kiburi na jeuri ambavyo kwake anadhani ni ujasiri na utendaji kazi mzuri ambao eti hata rais anaufahamu. Sijui huenda akawa sahihi lakini kwangu ni ubatili mtupu.
Masha ana sura mbili. Sura ya kwanza hujitokeza kama mzalendo wa kweli aliyeacha Marekani na na kurudi kutumikia nchi yake kwa sababu anaguswa na matatizo ya nchi yake. Anasema ameacha hata kazi yake ya mamilioni na kuingia katika siasa ili kutumia Watanzania. Ubatili mtupu.
Sura ya pili ni Masha amba ana uchu wa madraka na ndoto zinazoelea angani. Anataka mali kwa kasi sana bila kujali hizo mali zimepatikana kwa njia gani lakini ili mradi ni mwanashera basi kila alichonacho kakipata toka IMMMA Advocates.
Kaingia CCM juzi, kaukwaa ubunge, unaibu waziri na baadaye uwaziri, ghafla akagundua mteremko hapa, akaanza kuangalia mbali kama isemavyo kauli mbiu ya shule ya Sekndari Nsumba0Lenga mbali naye akaanza kuwaza Uwaziri Mkuu 2015 na baadaye Urais kama Mungu akipenda.
Lakini mimi ninayemfahamu, tangu anakutana na mkewe kule Marekani, ninapata taabu sana kuamini kama Masha amepata wapi jeuri aliyo nayo kiasi cha kutaka wengine wafilisiwe eti wanaiandika vibaya serikali. Sijui jeuri ya kuwaambia wazee wenye umri sawa na baba yake kwamba hawana akili na atawashughulikia ipasavyo. Lakini yote hii chanzo chake ni kiburi.
Kama hayati Nyerere angekuwa na kiburi kama cha Masha, basi baba yaeke Ddr. Fortunatus Masha angefia kizuizini, lakini kwa busara alimuokoa na hata kumwambia akimbie nje ya nchi ? ushahidi upo.
Akakaa uhamishoni Marekani na akawazaa akina Masha ambao leo wanataka wale wanaodhani wanahitilafiana kimawazo wafilisiwe au wafikishe vielelezo kwake ndani ya siku saba. Ninapata taabu sana kuamini uwezo wa kuchanganua mambo wa Waziri Mashaa kutokana na kauli zake tata na zilizojaa kiburi. Mathalani, Masha huyu huyu alisema mauaji ya albino ni tatizo dogo tu linalokuzwa na vyombo vya habari, lakini leo hii Waziri mkuu katoa chozi Bungeni, na Rais kasitisha zira Mbeya kuja kupokea maandamano ya kupinga mauaji ya albino. Huyu bado yupo Wizarani anahangaiaka na vitambulisho.
Lakini masha huyu huyu alikuja Mwanza hapa mwaja jana akaulizwa kwenye mkutano wa hadhara kuhusu anachokifahamu juu ya Kampuni ya Kifisadi ya Deep Green Finance Ltd iliyochota shilingi bilioni 10 toka Benki Kuu ya Tanzania na kisha kufunga virago. Akasimama, akanena ?tuliambiwa na serikali kusajili na kuifunga Deep Green Ltd.. ndiyo ninaifahamu sana?. Tafisi yakinifu ni kwamba serikali ndiyo iliyowatuma akina Masha na IMMMA Advocate kusajili na kisha kufunga kampuni ya kifisadi ya Deep Green. Huu ni ubatili mtupu!
Lakini Masha akaenda mbali zaidi akampa Bw. Mengi siku saba awasilishe ushahidi ofisini kwake juu ya madai yake dhidi ya serikali la sivyo atamshughulikia. Hivi tujiulize , ushahidi uwa unapelekwa mahakamani au ofisini kwa WAziri wa mambo ya Ndani? Mwanasheria kama Masha hajui ushahidi huwa unawasilishwa kortini? Ubatili mtupu.
Kana kwamba haitoshi juzi katoka Dodoma akawaambia waandishi wa habari kwamba hajawahi kukutana na kampuni ya SAGEM aliyojaribu kuitetea wala wakala wao. Ningekuwa mwana habari siku hiyo ningemuuliza alijuaje uwezo wake kiutendaji wa kampuni hiyo? Aliwezaje kuitetea kwa nguvu zote mpaka kuandika waraka wa siri kwa Waziri mkuu? Ubatili mtupu.
Lakini kesho yake tena akaendelea na kampuni yake katika radio moja jijini , sijui alialikwa au alijipeleka, na akasema amewahi kukutana n wawakilishi wa Kampuni ya SAGEM lakini siyo nje ya nchi. Sasa ndani ya saa 24Waziri masha anatoa kauli mbili zinazokinzana, lakini kwangu sikushangaa kwa sababu , huyu ndiye Masha ninayemfahamu.
Kule Mwanza akiwa waziri aliwahi kumtukana hadharani Diwani mmoja wa Chama cha Mapinduzi amatusi ambayo hayaandikiki, na akitaka ushahidi atapewa. Bahatti mbaya diwani huyo naye ni kiboko ikambidi Masha akaungama chini ya ulinzi mkaali.
Hakuishia hapo, Masha aliwahi kukunja ngumi hadharani ili apigane na mhariri na mmiliki wa Gazeli la Mzawa James Nhende, katika hoteli ya New Mwanza Hotel. Akatamka hadharani kwamba ana uwezo wa kumpiga na kuml,ipa gharama zote lakini Mungu aliepusha shari.
Waziri wetu, mwanasheria, na mbunge wetu anataka kupigana hadharani kisa kaandikwa vibaya na gazeti la Mzwa. Ubatili mtupu.
Masha katika kipindi kifupi alichokaa madarakani amejenga maadui wengi ndani na nje ya chama, kiasi cha kumchanganya akili, sasa badala ya kuwapa wauaji wa albino siku saba anawapa akina Mzee Mengi.
Masha huyu anatakiwa akamatwe na kushitakiwa kwa kosa la jinai kwani ushahidi upo wa wazi kabisa kwamba mwaka 2000 Oktoba aliwatishia polisi kwa basota yake sambamba na kuwatolea lugha chafu na kashfa juu.
Nanukuu hukumu ya Mahakama Kuu Mwanza, ?nyinyi polisi ni vibaraka wa CCM, wapumbavu, hamtumii akili, kama silaha sisi tunazo?. Sasa kama Davidi Blunkett Waziri wa Mambo ya Ndani (wa Uingereza) alilazimika kujiuzulu mwaka 2006 kwa kosa la kuajiri yaya ambaye alikuwa mhamiaji haramu miaka kumi iliyopita tena bila kujua, leo Masha anajisikiaje kuongoza polisi aliowaita wapumbavu na vibaraka wa CCM? Ubatili mtupu!
Leo, huyu mtu anajitokea kupiga kelelkwa jeuri na kiburi, lakini nina uhakika kuna siku Watanzania watamfahamu, kwani hata kule Nyamgana, leo hiini hati hati na uwezo wa kushinda tena ni asilimia 50. Sababu, jeuri na kiburi. Bahati mbaya sana, Mwanza waliwahi kumkataa Marehemu Bomani na fedha zake na u maarufu aliokuwa nao wakamchagua mwalimu wa sekondari, kaka yangu Paschal Mabiti.
Kama kura za maoni zikipigwa leo, Masha anayejiptapa kwamba hata akiwa wa tatu jina lake lake litarudi, nina shaka sana kama atashinda tena. Na kibaya zaidi ameshaanza kulalamika kwambakuna watu wanatumwa kumuangusha.
Bw. James Nhende, leo ni shujaa si kwa sababu tajiri au mwandishi wa habari, lakini kwa kukataa mapema kabisa kumuunga mkono Masha, akisema ana kiburi na jeuri ya hali ya juu. Alitumiwa wajumbe wa kila namna na zawadi juu akakataa kugeuka nyuma.
Nilikuwa Marekani nikasikia taarifa hizi, nikajua kumbe tunaomjua Masha tuko kadhaa, lakini wengi hawakuelewa, lakini kila kukicha anazidi kujipambanua, na kufanya Watanzania wamjue ni mtu wa aina gani.
Kwa sababu ameota kama uyoga ndani ya chama na hasa katika siasa anguko lake litakuwa ghafla kwa sababu hakujijenga katika misingi imara ya kulea viongozi wetu wa miaka ijayo. Aliomba ubunge akapewa, akalilia uwaziri akapata, ghafla anataka uwaziri mkuu 2015, na siku Edward Lowassa alipojiuzul uwaziri Mkuu miongoni mwa watu walioumia sana ni pamoja na Masha.
Hakuumia eti kwa sababu ni marafiki, hapana, alidhani ndoto yake kisiasa imekufa, na alisikika akisema maneno makali sana dhidi ya viongozi wakuu serikalini, nilikuwepo pale Dodoma hoteli, nikamsikia lakini bahati nzuri sana JK akazidi kumuinua.
Leo amevaa vita ya Lowassa bila kujua akidhani atalipiza kisasi, lakini anasahau kwamba ni mchanga kisiasa ambaye hakusomea hata uanachama wa chama tawala.
Wiki ijayo nitaeleza Masha alivyopata utajiri wa haraka haraka katika kipindi kifupi.