View Full Version : Ushindi wa Obama una maana gani?
mwanakijiji
11-05-2008, 09:53 AM
Seneta Obama anakuwa Rais wa Kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika na Marekani inakuwa nchi ya kwanza yenye watu wengi weupe kuongozwa na mtu mwenye asili ya Afrika. Je ushindi huu wa Obama una maana gani watu weusi wa Marekani, wale wa Afrika na wale waliotawanyika sehemu mbalimbali duniani?
Matigari
12-06-2008, 07:38 AM
Binafsi naona umetuongezea confidence kuwa tuanaweza kuongoza tukikazana. Hasa ukiangalia alivyo-organize kampeni yake, alivyokaa on topic hakuyumbishwa na hata ilipokuwa ni muhimu yeye kujibu hoja fulani fulani, aliamua kutojibu ili asiyumbe nje ya topic ( uvumilivu). Kuhusu wamerekani weusi, naona imewapa picha kuwa wanaweza kuwa kitu kingine zaidi ya kuwa wacheza mpira na wanamuziki, nadhani wataacha kudharau elimu, pia wamejifunza kuwa kutunza heshima yao, na kuwa na '' tabia nzuri'' ni kitu muhimu, maana ukifanya manyanga ukiwa mtoto ( kijana) utakapotaka kugombea cheo fulani hayo manyanga yatafukuliwa. Kwa weusi wengine duniani, sina uhakika kama tumejifunza kitu maana sisi huwa tuna tabia ya kuona mabo yanayofanyika ulaya na marekani na sehemu nyingine ughaibuni hayawezekani kwetu.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.