View Full Version : Hivi Ikulu inawaonaje Watanzania?
mwanakijiji
03-05-2009, 09:13 AM
Kuna kitu hakiko sawa. Kwanza Waziri Mkuu anatoa tangazo kuwa watuhumiwa wa mauaji ya albino wauawe papo hapo bila ya kufuata mchakato wa sheria. Leo Ikulu nao wanakuja na kusema kuwa tuweze kuwaruhusu wawekezaji wawekeze kwenye mambo ambayo yanahitaji tenda kwa kuiita utaratibu kuwa kuwa ni "dhana" tu. Tunachoshuhudia ni jaribio la nguvu la kutaka Watanzania wailipe Dowans kwa mbinu zote na sasa inakuwa kama tumekwidwa mashati na kulazimishwa kulipa kampuni ya kitapeli. Tunasema inatosha. Soma kijarida cha Cheche kwenye Forums na fuata maelekezo ya nini wewe Mtanzania ufanye kuonesha kutokubaliana na serikali katika suala hili. Haitoshi kulalamika pembeni. Ifuatayo ni taarifa ya Ikulu kuhusu mkutano wa Rais Kikwete na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Tanesco
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/salva.jpg
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makubaliano makuu yaliyofikiwa katika mkutano wa tathmini ya utendaji wa Serikali uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumanne, Machi 3, 2009 kati ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake:
(a) Kwamba sekta ya madini isimamiwe kikamilifu kwa kuhakikisha kuwa wenye leseni za kutafuta na kuchimba madini wanazitumia kwa masharti yaliyoombewa, na kuwa wasiozitumia leseni hizo kwa kuzingatia masharti ya leseni hizo wanyang’nywe leseni hizo badala ya kuzitumia kuendesha ulanguzi tu.
(b) Kwamba zichukuliwe hatua za haraka kukomesha kabisa wizi wa mafuta ya transfoma ambao unasababisha hasara kubwa kwa taifa na kuruvuga mtandao wa kusambaza umeme kwa wananchi.
(c) Kwamba Kamishna wa Madini Nchini, kwa kutumia madaraka na mamlaka yake kisheria, achukue hatua mara moja kukomesha uchimbaji wa kokoto katika maeneo yasiyostahili, na hasa katika eneo la Kunduchi/Tegeta, Dar es Salaam ambako tayari Serikali ilikwishakupiga marufuku uchimbaji wa kokoto, lakini baadhi ya wachimbaji wamerudi katika eneo hilo kuendesha uchimbaji.
(d) Kwamba ziongezwe juhudi katika uzalishaji wa umeme nchini kwa sababu programu ya taifa ya uzalishaji umeme bado iko nyuma na bado liko pengo kubwa kati ya mahitaji halisi ya umeme nchini na umeme unaozalishwa kwa sasa.
(e) Kwamba dhana ya tenda na Sheria ya Manunuzi isiruhusiwe kuwa kikwazo katika miradi mikubwa mikubwa ya miundombinu ya nishati, hasa ile ambako wawekezaji wanajitokeza wenyewe kuwekeza katika maeneo ambako taifa linahitaji uwekezaji mkubwa na wa haraka na ambako nchi inaonekana ilichelewa kuwekeza.
(f) Kwamba kasi iongezwe katika kuhakikisha kuwa maeneo yaliyoahidiwa umeme yanapatiwa umeme bila ucheleweshaji usiokuwa na sababu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
03 Machi, 2009
Our Take:
Hivi "dhana ya tenda" ndiyo upupu gani?

Mwanakijiji, kwa uchache wa mambo na nyongeza ya hoja hii lipo jambo ambalo labda likichunguzwa na kuzungumzwa linaweza kutoa mwanga wa mambo mengi ambayo yapo gizani. Hii "DIZAINI" ya mara kwa mara Mheshimiwa Rais "amemuagiza" ama hili la juzi tuu pale bandarini kwamba Mheshimiwa Rais ana majina ya baadhi ya waharibifu wa usaidiaji ukwepaji kodi na yupo tayari kuyakabidhi majina haya kwa wahusika wakuu ili watu hao wachukuliwe hatua ama kufutwa kazi..... (Tunasema HONGERA JK) Lakini hii kazi ni ya hao wakurugenzi na wakuu wa bandarini na sehemu ya kodi, inakuwaje wao wenyewe hawajui mazingira ndani ya sehemu zao za kazi mpaka Rais aje awashtue!!!? Huku ni kumpa madaraka zaidi Rais ya kuingilia hata taratibu za kazi ambazo zipo bayana tu.. sasa hili lililojiri la DOWANS tena lina leta sura kama ile ya bandarini kwamba wapo wavivu wameshindwa kazi zao na badala ya wao kuwajibishwa basi IKULU inakuwa muamuzi mkuu na hata ikibidi kuvunja taratibu na kuja na misemo mingi tu kama "dhana ya tenda" nk nk.... ... Mwanakijiji hii safisha safisha inabidi ianzie mbali sana (Labda ile "MRAMBATSVINA" ya Zimbabwe ipite huko sijui...!!):eek:
dickabudi
03-05-2009, 01:13 PM
1.Naomba ithibitishwe kuwa hii barua imetoka kurugenzi ya mawasiliano IKULU maana sioni aliyesaini hapo
2.Tenda ni moja tu ya aina ya taratibu za manunuzi ni kweli si lazima uifuate zipo nyingine kama vile INTERNATIONAL SHOPPING ambapo kupitia mitandao na majarida mbalimbali unaweza pata wenye mali na kuomba wakupe quotations zao na mkafanya biashara na ipo ndani ya msahafu wa tararibu za manunuzi ya umma na unaelezeka ni wapi na kwa sababu gani utumike, tusipumbazwe na Tenda kuona kuwa kuna transparency na fairness tukasahau weakness za utaratibu huu ambapo urasimu ni kitu kikubwa
3.Ni jana tu Kurugenzi ya mawasiliano imekuja juu kukanusha taarifa za Dowans kuingiliwa kati na Mh. Rais sasa tujadili kitu ambacho tunahakika nacho tusijadili mambo ya KUFIKIRIKA kwenye riwaya za Marehemu Shaban Robert
mwanakijiji
03-05-2009, 04:39 PM
1.Naomba ithibitishwe kuwa hii barua imetoka kurugenzi ya mawasiliano IKULU maana sioni aliyesaini hapo
Hii ni taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari. Tuna akili timamu kuweza kuamua kuweka kitu cha uongo na kukisema kuwa ni cha kutoka Ikulu.

Sheria ya tenda haitoi uhuru hivyo. Taasisi binafsi zinaweza kufanya zinavyopenda, kwenye taasisi za umma Sheria ya Tenda ya 2004 na kanuni za manunuzi za 2005 zinaongoza. Nje ya hapo ni uvunjaji wa sheria.
3.Ni jana tu Kurugenzi ya mawasiliano imekuja juu kukanusha taarifa za Dowans kuingiliwa kati na Mh. Rais sasa tujadili kitu ambacho tunahakika nacho tusijadili mambo ya KUFIKIRIKA kwenye riwaya za Marehemu Shaban Robert
Hii taarifa ya ilitoka kabla ya yeye kuja kukanusha.
dickabudi
03-05-2009, 04:59 PM
Hii ni taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari. Tuna akili timamu kuweza kuamua kuweka kitu cha uongo na kukisema kuwa ni cha kutoka Ikulu.
Ni vizuri kupokea taarifa iliyosainiwa maana Mtu hawezi tena kuikana na umuhimu wa sahihi unaeleweka otherwise lets be frank its working unprofessional
Sheria ya tenda haitoi uhuru hivyo. Taasisi binafsi zinaweza kufanya zinavyopenda, kwenye taasisi za umma Sheria ya Tenda ya 2004 na kanuni za manunuzi za 2005 zinaongoza. Nje ya hapo ni uvunjaji wa sheria.
Mzee Isome vizuri na kwa mapana utakuta manunuzi ya kawaida yana aina mbili za tenda, pia local shopping na international shopping zina nafasi yake katika manunuzi ya serikali, hasa katika manunuzi ya vifaa maalum na zana za kivita, vifaa maalum ni pamoja na mitambo mikubwa inayohitaji ujuzi wa ziada na imetajwa kuwa ni uzalishaji wa nishati, uchunguzi na matibabu
Hii taarifa ya ilitoka kabla ya yeye kuja kukanusha.
Nini kauli yako kuhusu kanusho la Mkurugenzi wa Mawasiliano State House, kwa nini msimbane na hii barua
Ohotaite
03-05-2009, 05:22 PM
Nawasalimu wote. Ni mara ya kwanza kutoa maoni katika baraza hili. Nina maswali yafuatayo:
1. Je ni lini Dr. Idrisa aligundua kuwa kuna hatari ya nchi kuingia gizani? Je juma lililopita au ni kabla ya hapo?
2. Baada ya kuvunja mkataba na Dowans mwezi wa nane 2008, Je Dr. Idrisa alishauri nini kifanyike ili nchi isiingie gizani?
3. Wakati a kukatisha mkataba na Dowans walitwambia mitambo yao ni mibovu. Je walisema hayo baada ya kuikagua?
4. Leo wanasema mitambo ni mizuri kabisa. Je wameikagua kwa sababu gani na kwa ghrama za nani?
Inawezekana Dr. Idrisa na Mh. Ngeleja na Mh Zitto wanajua kinachoendelea na wana siri kubwa au maskini hawajui ila wanatumiwa tu.
Leo nimemtumia sms Mheshimiwa Waziri na Dr. Idrisa na kuwashauri watangaze tenda na kama Dowans akishinda basi atuuzie mtambo. Waziri kanijibu na kusema ni wazo zuri. Daktari Rashid hakujibu.
TUENDELEE KUABALISHANA:confused:
dickabudi
03-05-2009, 05:53 PM
(e) Kwamba dhana ya tenda na Sheria ya Manunuzi isiruhusiwe kuwa kikwazo katika miradi mikubwa mikubwa ya miundombinu ya nishati, hasa ile ambako wawekezaji wanajitokeza wenyewe kuwekeza katika maeneo ambako taifa linahitaji uwekezaji mkubwa na wa haraka na ambako nchi inaonekana ilichelewa kuwekeza.(f) Kwamba kasi iongezwe katika kuhakikisha kuwa maeneo yaliyoahidiwa umeme yanapatiwa umeme bila ucheleweshaji usiokuwa na sababu.
Mwanakijiji,
Kwanza nimefarijika kuona scanned document na ndipo sasa naweza tema cheche zangu
Kurugenzi ya mawasiliano inaeleweka ipo wapi wape hiki kipengere watafsiri waeleze walikuwa wanalenga miradi ipi, na wa Dowans umo??? wabane wajikaange kwa mafuta yao wenyewe tusiwasemee, ila tuwabane kwa hoja watamke wao wenyewe, wawekezaji kwenye mambo ya nishati ni wepi na wangapi wamekuwa wakikwamishwa na taratibu za tenda??
Ohotaite
03-05-2009, 06:13 PM
1.Naomba ithibitishwe kuwa hii barua imetoka kurugenzi ya mawasiliano IKULU maana sioni aliyesaini hapo
2.Tenda ni moja tu ya aina ya taratibu za manunuzi ni kweli si lazima uifuate zipo nyingine kama vile INTERNATIONAL SHOPPING ambapo kupitia mitandao na majarida mbalimbali unaweza pata wenye mali na kuomba wakupe quotations zao na mkafanya biashara na ipo ndani ya msahafu wa tararibu za manunuzi ya umma na unaelezeka ni wapi na kwa sababu gani utumike, tusipumbazwe na Tenda kuona kuwa kuna transparency na fairness tukasahau weakness za utaratibu huu ambapo urasimu ni kitu kikubwa
3.Ni jana tu Kurugenzi ya mawasiliano imekuja juu kukanusha taarifa za Dowans kuingiliwa kati na Mh. Rais sasa tujadili kitu ambacho tunahakika nacho tusijadili mambo ya KUFIKIRIKA kwenye riwaya za Marehemu Shaban Robert
Nafikiri kilichotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ni PRESS RELEASE ambayo naona mara nyingi zinatoka bila kuwekwa sahihi ya mtoaji. Lakini tusisahau kuwa alichotoa MWanakijiji ndiyo hicho hicho kilichosomwa kwenye taarifa ya habari ya ITV. Sasa kama kilikuwa 'fake' kwa Mwanakijiji basi na IPP Media walipata kitu 'fake'. Je kwa akili ya kawaida hili linawezekana? TUENDELEE KUHABARISHANA:cool:
dickabudi
03-05-2009, 07:10 PM
(e) [B]Kwamba dhana ya tenda na Sheria ya Manunuzi isiruhusiwe kuwa kikwazo katika miradi mikubwa mikubwa ya miundombinu ya nishati, hasa ile ambako wawekezaji wanajitokeza wenyewe kuwekeza katika maeneo ambako taifa linahitaji uwekezaji mkubwa na wa haraka na ambako nchi inaonekana ilichelewa kuwekeza.[/B
Mwanakijiji,
Kwanza nimefarijika kuona scanned document na ndipo sasa naweza tema cheche zangu
Kurugenzi ya mawasiliano inaeleweka ipo wapi wape hiki kipengere watafsiri waeleze walikuwa wanalenga miradi ipi, na wa Dowans umo??? wabane wajikaange kwa mafuta yao wenyewe tusiwasemee, ila tuwabane kwa hoja watamke wao wenyewe, wawekezaji kwenye mambo ya nishati ni wepi na wangapi wamekuwa wakikwamishwa na taratibu za tenda??
Mzee tupo huku tunataka tafsiri ya kipengere 'e' kutoka kwa Kurugenzi ya habari IKULU
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.