PDA

View Full Version : Kamati Kuu ya CCM kukutana leo



mwanakijiji
03-06-2009, 07:13 PM
Imehaririwa: 06.03.2009 0101 EAT Gazeti: Uhuru



? Kamati Kuu CCM kukutana Dodoma leo

sogeza Habari Nyingine
? Kamati Kuu CCM kukutana kesho 31.10.2008 [Habari Zaidi]
? Halmashauri Kuu CCM kukutana Dodoma kesho 09.09.2008 [Habari Zaidi]
? Wanafunzi vyuo vikuu wasimamisha mgomo 08.11.2008 [Habari Zaidi]

NA MWANDISHI WETU

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana leo mjini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM makao makuu ilisema kikao hicho kitakuwa cha siku moja.

Kamati Kuu itaandaa ajenda kwa ajili ya mkutano maalumu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, utakaofanyika kesho mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, ajenda ya kikao hicho ni kupitia taarifa ya Kamati Ndogo ya kupendekeza namna ya kutekeleza kwa ufanisi uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa kuwashirikisha wanachama wote wa CCM katika kupiga kura za maoni na kuwapata wabunge/ wawakilishi wanawake kufikia asilimia 50.

Kikao hicho wa mujibu wa taarifa kitaanza saa 7.30 mchana.

Keil
03-08-2009, 09:44 AM
Mwanakijiji,

Ka-nzi hakajapita mitaa ya Dodoma? Maana naona kimya mpaka leo ama agenda za safari hii ni siri sana?