View Full Version : Lowassa, Karamagi wakutana Dubai
mwanakijiji
03-09-2009, 09:28 AM
Siku ya Jumapili wakuu hawa wamekutana Dubai katika "kikao" chao. Wakati huo huo mmoja wa wapambe wao Peter Serukamba naye yuko safarini akiwa anapitia Uswisi kuja US (natarajia kumtafuta nikienda NY wiki ijayo, kwani angependa tuonane).
Mkutano wao huo umekuja siku moja baada ya KLHN kufanya kile ambacho hawakufikiri tutakifanya. stay tuned.
Duh! Wanapanga mipango ya kuwamaliza mafisadi wenzao. Kazi ipo. Serikali inayoshindwa kuwashughulikia wahujumu wa uchumi.
jingo
03-09-2009, 11:48 AM
nadhani watakuwa kwenye mkanganyiko baada ya kukwaa kisiki juu ya kuwauzia watanzania zile takataka zao(Majenereta ya Dowans)
wanajipanga upya...mi nadhani wapeleke somalia...sisi watz hatuyataki!
Phoibe
03-09-2009, 11:48 AM
Duh! tusubiri tuone walichokuwa wanajadili
jingo
03-09-2009, 11:54 AM
na hivi sasa watanzania tunakabiliwa na changamoto moja muhimu ya kumshinikiza Rais Kikwete awaondoe madarakani waziri na naibu waziri -Nishati na Madini(Ngeleja na Malima) Management ya TANESCO hasa Mkurugenzi mkuu Dr.Idriss Rashid kwani ameshahaidi kutulaza gizani,wanafunzi wasisome na hospitali zihsondwe kufanya kazi! kisa watanzania wamekataa kununua janereta chakavu ya DOWANS!
Je kwanini mtu kama huyu aendelee kukalia ofisi ya umma?
mwanakijiji
03-09-2009, 04:35 PM
Hawa jamaa hawajakubali kushindwa. Kama tulivyodokeza huko nyuma Dowans lazima watalipwa tu.. Aidha itakuwa sasa hivi, kwenye yao kule Paris, au baadaye wakati umeme ukiwa mgumu na tukapigishwa magoti kuwaomba msamaha Dowans!
mkaguzi
03-09-2009, 07:48 PM
Kazi ipo! Ila wanapaswa kujua Watanzania wa leo c wale wa 47.
mkaguzi
03-09-2009, 07:50 PM
Hivi MMJ, Dr Tenga alikua anahusika na Richmond Pia?
mwanakijiji
03-09-2009, 10:35 PM
Hivi MMJ, Dr Tenga alikua anahusika na Richmond Pia?
hapana kwa kadiri ninavyojua bali alikuwemo kwenye kampuni ya Afritainer ya Rostam..
Ni kipi hicho mlichokifanya enyi KLHN hadi kikawasukuma wao kuruka na kwenda Dubai ''kunong'onezana"??
Mwaga mambo hadharani mkulu,haya ya kuanza kupeana taarifa kwa episodes yameanza lini tena?Au Cheche litakuja kuanika yote....?
mwanakijiji
03-10-2009, 12:40 AM
Ni kipi hicho mlichokifanya enyi KLHN hadi kikawasukuma wao kuruka na kwenda Dubai ''kunong'onezana"??
Mwaga mambo hadharani mkulu,haya ya kuanza kupeana taarifa kwa episodes yameanza lini tena?Au Cheche litakuja kuanika yote....?
usiwe na wasiwasi mwali atawekwa hadharani muda si mrefu...
na hivi sasa watanzania tunakabiliwa na changamoto moja muhimu ya kumshinikiza Rais Kikwete awaondoe madarakani waziri na naibu waziri -Nishati na Madini(Ngeleja na Malima) Management ya TANESCO hasa Mkurugenzi mkuu Dr.Idriss Rashid kwani ameshahaidi kutulaza gizani,wanafunzi wasisome na hospitali zihsondwe kufanya kazi! kisa watanzania wamekataa kununua janereta chakavu ya DOWANS!
Je kwanini mtu kama huyu aendelee kukalia ofisi ya umma?
Rais mwenyewe yuko kwenye kundi la kutusavimbi. Hivi unafikiri kama ingekuwa Venezuela kwa chavez tungekuwa na mburu kenge kama hawa?
hofstede
03-11-2009, 05:01 PM
usiwe na wasiwasi mwali atawekwa hadharani muda si mrefu...
Haya with Mkjj tutabadili mitazamo yetu tu watake wasitake. Saa ya utawala ni sasa tuchukue jukumu la kupenda mazuri kwa nchi yetu si kwetu binafsi
jkileo
03-13-2009, 01:53 PM
hata kama watajipanga vipi lakini Watanzania tumeshajua walichotufanyia haijalishi watashughulikiwa leo au kesho but there is a day watakapojuta walichokifanya
jatropha
03-13-2009, 03:47 PM
Sasa na zitto nae aliingiaje humo?Nani anajua atueleze.
omondi
03-14-2009, 12:30 PM
Jatropha,
JF wameweka minutes za kikao cha kamati ya Zitto. Ukiisoma utabaini kuwa Idris alitumia hila kuidanganya kamati kuwa TANESCO hawakupewa fursa ya kueleza tatizo lao walipokutana na kamati ya nishati na madini. Idris, akisaidiwa na wapambe wa dowans, (Serukamba) walijitahidi kuijengea hofu kamati kuwa mitambo isiponunuliwa, nchi inakwenda gizani. Hata hivyo mitambo ya dowans was not the only option.
On the other hand, nilimsikia Mwakyembe akihojiwa na ITV. Kuna sehemu ya jibu lake alipo "quote" kifungu cha manunuzi ya serikali 72 (ii) alichosema kinaipa uwezo serikali ku forfeit ile mitambo. Kwa nini hilo halikuwa moja ya mapendekezo 18 ya kamati yake, nashidwa kujua! Ukichanganya na kauli yake ya kuifichia aibu serikali inakuwa aibu mara 100!
omondi
03-14-2009, 12:40 PM
Mwanakijiji,
Tutashukuru kupata hints za huyo Mwali!
Fingigwe
03-15-2009, 12:36 AM
Mkuu unatukatisha tamaa unaposisitiza kuwa hawa jamaa lazima walipwe. Yaani kauli zote hizi hata za akina Mwakyembe hazisaidii kitu! Kama kweli wakilipwa basi yule mheshimiwa aliye Ikulu hatakuwa na budi kujiuzulu kwani hatakuwa na nyimbo tena kwa waTZ. Aidha, ndugu yangu W. Mkuu naye itabidi arejeshe kigoda cha mtemi kwani hatakuwa na ubavu wa kuendelea kukikalia ilhali mwenyenacho anaendelea kufanya vitu vyake bila shaka yoyote.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.