PDA

View Full Version : Watanzania Waasia



mwanakijiji
11-10-2008, 05:54 PM
Hakuna kitu kinachoonesha utii wa mtu kwa nchi yake kama utayari wake kufa kwa ajili ya nchi hiyo. Ni kipimo cha juu kabisa cha mapenzi ya mtu kwa nchi yake. Lakini pia kuitumikia nchi katika nafasi mbalimbali kunaonesha jinsi gani mtu anavyolipenda Taifa lake.

Mojawapo ya vitu ambavyo havionekani sana katika Taifa letu ni Watanzania wenzetu wenye asili ya Asia (wahindi, Waarabu, n.k) kujiunga na vyombo vyetu vya usalama hasa majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama.

Nikikumbuka vizuri baada ya uasi mwaka 1964 ni maafisa wachache wa kizungu ambao waliendelea na jeshi na ni mmoja ambaye aliendelea kuitumikia kwa muda mrefu tu. Sifahamu sasa hivi kama kuna maafisa wowote wa JWTZ ambao aidha wana asili ya Uhindi au Uarabuni.

Kwa upande wa Polisi kumekuwepo na maafisa kadhaa wa Kihindi na wenye asili ya Uarabuni lakini nadhani sasa hivi wengi watakuwa wameshastaafu. Nafahamu wapo vijana wachache ambao waliingia huko (namkumbuka Bi. Khadija K. binti wa kiarabu aliyejiunga toka Tanga) na pia Insp. Khan ambao at the time nilikuwa nashangaa kweli kuwaona kwenye jeshi letu.

Hata kwenye taasisi nyingine (ukiondoa za Kitaaluma) bado jamii hii ya Watanzania inakosekana sana. Sijui idadi yao kwenye TRA, Public service n.k

Kwa upande wa Magereza ndiyo sijui kabisa kama kuna watanzania wenye asili ya nje ya bara letu ambao wanaitumikia nchi yao hivyo. Wakati ambao nakumbuka tuliweza kuwaona Wahindi na Waarabu wengi ni wakati wa JKT ule. Sijui katika JKT hiii ya kujitolea inakuwaje.

BIla ya shaka unajiuliza "what is the point". Point yangu ni kuwa inaonekana aidha kwa makusudi au by default mchango wa Watanzania hawa unataka kuishia kwenye siasa na biashara au sekta binafsi na siyo kwenye utumishi wa umma.

Nakabiliwa na maswali machache:

a. Kwanini Watanzania wenye asili ya Uhindi au Uarabuni hawaingii kwenye vikosi vya usalama? Zamani nakumbuka tulikuwa tunawatania kuwa wao ni "watoto mayai" hawawezi kazi za shurba lakini nikagundua kuwa hata kule Uhindi na Uarabuni kuna majeshi na POlisi na wao wanapewa mafunzo ya kijeshi na kuhenyeka kama sisi. Hivyo suala la "umayai" halipo.

b. Ni juhudi gani zinafanyika kurecruit Watanzania hawa hasa kutokana na ujuzi wao wa mambo ya biashara, utaalamu wa IT, n.k n.k na hivyo kuleta vipaji ambavyo vinahitajika sana kwenye vyombo vyetu hivi?

c. NI kwa kiasi gani familia za ndugu zetu hawa zinawa encourage watoto wao kuitumikia nchi yao kwa zaidi ya siasa na biashara na kuingia kwenye utumishi wa umma. Watakuwa wanaendelea kutoa misaada tu mpaka lini.

Desert Eagle
11-10-2008, 09:52 PM
Bwana mkubwa umesahau kitu kimoja very interesting,,Mie toka nimezaliwa na kukua hapa Tanzania sijawahi kubahatika kuona Mu-asia hasa Muhindi ameolewa au ameoa Mtanzania original (mweusi) nimewahi kuwaona waarabu pale Maskati fisi Shinyanga vijijini wameoana na kujichanganya lakini muhindi sijapata kuona labda nipewe ushahidi la sivyo ni "Wabaguzi" namba moja.

Tena ukiachia kuoana wapo wengi pale Upanga wamekua na kulelewa pale lakini hata kiswahili hawakijui vizuri..kwa kifupi hawana shida wala mapenzi na TZ,

Thats why wanafanya biashara haram ndani ya ardhi yetu, wengine mafisadi, wengine wauza madawa ya kulevya na michezo yote michafu ambayo mtu mwenye uchungu au upendo kwa nchi yake hawezi fanya hivyo

mwanakijiji
11-11-2008, 04:41 PM
DE, unachosema hata mimi nimekiona; lakini yawezekana kuna vitu zaidi ya ubaguzi wao. Ndicho hicho ninachojaribu kukitafuta. Tatizo hasa liko wapi?

Kepa
11-11-2008, 11:49 PM
Naungana na Dee an Mkjj, Lakini hawa watu wanapatage nguvu ya kutubagua wakati wapo ( genini) / kwetu?. Jamani hivi hili linawezekana?

Mimi naona wenyeji ndo tumewapa hicho kiburi hadi wanajioana kwamba wao ni bora zaidi kuliko sisi, Tuseme ule ukweli, hawa watu hata wakishikwa na Nyara za Serikali, au mabomu mengine utashangaa wala hawapelekwi kwenye vyombo vya haki. Wakisababisha ajali pia hilo si kosa. kisa eti ni Magabachori. Kodi ya mapato wanalipa kwa kujipangia ukiuliza eti oohh wamekata kitu kidogo.

Mimi naona kuna tundu dogo liliachwa wazi tangu miaka ya sitini, tundu hilo baadae likakumbwa na mlipuko wa volkano, ambayo iitengeneza ufa mkubwa mno, kuuziba labda twende tukajiulize kwa Mzee Robert Mugabe.