mwanakijiji
03-09-2009, 09:54 PM
Na Boniface Meena
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Dominique Strauss-Kahn ameitaka Tanzania kuwatumia wataalam wa ndani kukuza uchumi wa nchi badala ya kutegemea mawazo kutoka IMF.
Kahn alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, katika mdahalo wa hali ya uchumi duniani uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alisema sekta binafsi inakuwa kwa kasi kubwa hapa nchini zaidi ya nchi nyingine, hivyo ni muhimu wachumi wa nchini wakatumika kukuza uchumi.
"Msitegemee mawazo kutoka IMF katika kushughulika na uchumi wenu, ni muhimu mtumie wataalamu wenu zaidi ili kujisaidia kiuchumi," alisema Khan.
Alisema Tanzania haitaathirika kwa kiasi kikubwa na mgogoro wa kifedha unaoendelea duniani kwa kuwa iko katika hali nzuri na inayo nafasi ya kupambana nao huo kutokana na uwekezaji wa ndani.
"Tanzania inayo nafasi nzuri ya kupambana na mgogoro wa kiuchumi kwa kuwa uwekezaji ni mzuri ndani ya nchi," alisema Khan.
Aliongeza kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimekuwa zikifuata mawazo ya IMF yaliyotolewa miaka 10 iliyopita hivyo kuifanya iwe katika wakati mzuri wa kupambana na mgogoro wa kiuchumi unaoendelea duniani hivi sasa.
Khan alisema IMF haiwezi kuzuia migogoro ya kiuchumi inayotokea duniani, bali ina uwezo wa kutoa tahadhari juu ya kuwepo kwa matatizo kama ilivyofanya mwaka 2006 kuhusina na mgogoro uliopo sasa.
"Sisi wenyewe tumeshangazwa na mgogoro huu, lakini hatuwezi kuzuia ila tunatoa onyo kama tulivyofanya mwaka 2006 kwamba, tutakuwa na matatizo zaidi ya kiuchumi siku za baadaye," alisema Khan.
Wakati huohuo, Khan ametoa msaada wa wa Sh 6.6 milioni kwa hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kuimarisha huduma ya watoto wenye ulemavu.
Fedha huzo zilikabidhiwa jana na mkurugenzi huyo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Karatu, Dk Wilbroad Slaa alipotembelea hospitali hiyo iliyopo Msasani jijini Dar es Salaam.
Dk Slaa alisema msaada huyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza huduma kwa watoto wenye ulemavu waliopo katika hospitali hiyo.
Khan pia alitembelea soko la Manzese kujionea shughuli za kibiashara zinavyoendeshwa na kununua baadhi ya vitu katika eneo hilo.
Wazo:
Hivi kumbe tunawategemea IMF kimawazo?