PDA

View Full Version : Zitto alikosea?



mwanakijiji
03-10-2009, 04:31 PM
Unachukuliaje msimamo wa Zitto kuhusu suala la Dowans?

Keil
03-10-2009, 07:41 PM
Ni ngumu kumhukumu kama alikosea ama hakukosea. Katika michango yangu kule JamiiForum nilimtahadharisha kwamba asije akawa amelishwa kasa kwa kupewa info nusu na yeye akajikuta anaenda hewani huku akijua kwamba info zote alizopewa zilikuwa sahihi, na kumbe mafisadi walimtumia kwa maslahi yao pasipo yeye mwenyewe kujijua kwamba anatumika. Katika mazingira ya sasa, mafisadi wanahitaji sana support ya watu kama Zitto kwa kuwa jamii/public ina imani kubwa sana na mtu kama huyo na hasa baada ya sakata la Buzwagi pamoja na list of shame na mengineyo.

Mh. Zitto amesema kwamba yeye ana-support pendekezo la Tanesco la kununua mitambo (hapa hayuko specific kama ni ya Dowans ama mipya, ingawa magazeti yalimnukuu akisema hata ikibidi kubadilisha sheria na pia yeye mwenyewe alikomaa kwamba aonyeshwe kipengele cha sheria kinavchokataza kununua mitumba). Kimazingira ama impliedly msimamo wa Tanesco umekuja kuwa wazi baada ya wao kujitoa kununua mitambo ya Dowans. Dr Rashidi alisema kwamba nchi ikiingia gizani yeye asije akaulizwa. Hilo pekee linaonyesha kwamba hakuwa na mpango wa kununua mitambo mingine zaidi ya ile ya Dowans. Kama angekuwa na wazo la kununua mitambo mipya basi angesema mchakato wa kununua mitambo mipya utaanza mara moja, lakini kwa kuwa inaweza kuchukua muda mrefu kupata mitambo mipya basi ikitokea tumeingia gizani itakuwa ni kwa bahati mbaya na siyo makusudi. Sasa kama by implication kwamba msimamo wa Tanesco ulikuwa ni kununua mitambo ya Dowans, basi Zitto alifichwa kitu na hivyo amejikuta anasema ana-support pendekezo la Tanesco ambalo ni kama blank cheque then mtu anakwenda kujiandikia amount anayoitaka.

Pendekezo la TANESCO lilipopigwa nyundo na kamati ya nishati na madini, mambo yalienda kimya kabisa na Ngeleja alitutangazia kwamba mitambo ya Dowans haitanunuliwa. Sasa hili la kuanza kuunga mkono ununuzi wa mitambo hiyo limetoka wapi? Ninapata woga sana kwamba Zitto alitumika na mafisadi bila yeye mwenyewe kujua kwamba jamaa walikuwa wana-push agenda ya siri.

Kuna info nyingi ambazo zina-miss na zinapingana sana. Kwanza Kamati ya Nishati na Madini inasema Bodi ya TANESCO ilikataa proposal ya kununua mitambo ya Dowans, halafu ZItto anasema kwamba kwenye semina iliyowakutanisha PAC, TANESCO na serikali; PAC iliuliza msimamo wa Bodi, na kwamba Mwenyekiti wa Bodi alikuwepo na alijibu kwamba wao kama Bodi hawana tatizo, lakini some media houses na Mwakyembe wanasema Kikao cha Bodi cha 4/12/2008 Bodi ilipinga. Hapo kuna utata.

Zitto anasema Kamati ya Nishati na Madini haikutoa nafasi ya kusikiliza hoja za TANESCO, Mwakyembe anakana anasema walikutana kwa siku nzima siku ya 14/12/2008. Sasa yupi anasema kweli na yupi ana info nusu?

Makamu wa Kamati ya PAC anasema alichosema Zitto ni msimamo wa kwake na siyo msimamo wa PAC. Sasa ukiona mwenyekiti na makamu wake wanapingana lazima kuna utata somewhere, nani anasema kweli na nani anadanganya?

Kama documents zipo, ziwekwe hadharani watu tuzisome na tutajua kama kweli Zitto alichemsha ama anaonewa na hivyo watu hatukumwelewa. Pamoja na hayo hoja ya kununua mitambo ya Dowans ni hoja tete sana na ilihitaji sana umakini kabla Mh. Zitto hajaenda hewani, na kwa kuwa ni hoja tete angekaa kimya bila kusema lolote kusubiri majibu ya barua aliyotuma kwa Mh. Sitta.

Swala hili kwa sasa litageuzwa kuwa mtaji wa kisiasa na hasa kwa baadhi ya wabunge wa CCM. CCM ya leo ina makundi. Kundi la kwanza ni la RA/EL ambalo linatetea ufisadi kwa sababu ambazo wote tunazijua maana wasipofanya hivyo nhilo ndiyo litakuwa anguko lao. Pamoja na hayo, kwa kuwa waliingia kwenye ubunge kwa njia za kifisadi, sasa hivi wanasaka hela kwa udi na uvumba ili ziweze kuwasaidia kurudi tena. Hapo inabidi uzingatie kwamba majina yao yamechafuka sana na hivyo wanahitaji nguvu ya ziada (fedha) ili kujisafisha na hatimaye warudi tena Bungeni.

Kundi la pili ni la waheshimiwa wanaopiga kelele za ufisadi (Sendeka, Kimaro, Kilango, Sellelii, Mwakyembe, et al), hawa wana tumaini kwamba hoja ya kupinga ufisadi ndani ya CCM ndiyo itakuwa mtaji wao ili waweze kurudi tena Bungeni 2010, Hao wabunge wamekuwa wakisemwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba wameshindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi na wao pia wamekuwa wakilalamikiwa kwamba kuna mapandikizi wa mafisadi ambao wanaandaliwa ili waje kugombea ubunge.

Kundi la tatu ni wenzangu na mimi ambao wanafuata upepo tu, kwa hiyo leo anawezakuwa huku na kesho akabadilika akawa upande wa pili. Hawana kambi ya kudumu ni sawa na aliye mguu mmoja ndani na mguu mwingine nje.

Hoja ya ununuzi wa mitambo ya Dowans imegonganisha maslahi ya kambi mbili zinazopingana. Kambi ya mafisadi inatuhumiwa ku-own mitambo ya Dowans na hivyo hela za mauzo ya mitambo ya Dowans itawapa nguvu zaidi kuelekea uchaguzi wa mwakani. Wakipata hela hizo itakuwa ni rahisi kwa kambi ya mafisadi kuwashughulikia wapinga ufisadi na hivyo kuwafutilia mbali kwa kuwa kambi ya mafisadi inaelewa kwamba wapiga kura wa Tanzania ni masikini na hivyo wakipewa hela kidogo watawachagua watu wao na hivyo Bunge la 2010 liwe dominated na wabunge wenye mawazo na mitazamo ya akina Serukamba.

mohammedzahor
03-10-2009, 11:51 PM
tunahitaji kujipanga upya ili kuona tahadhari ya dr, Idris haitufikii, aidha sasa viongozi wetu wajitahidi kuwa makini na mawazo yao mana mara nyingi sasa kunatokea tofauti kati yao wao na public, hivyo kuifanya serikali kuonekana inapingana na mihimili mengine ya nchi jambo ambalo linatoa picha mbaya kwa jamii na kwa mataifa mengine.

Ach-F
03-11-2009, 02:03 AM
Jamani mbona mnamuandama sana Zito? Zito hata miaka 40 hajafikisha wahenga walisema kua uyaone.

dickabudi
03-11-2009, 11:51 AM
Na Masha nae mbona hajafikisha 40 anaandamwa??? wote ni kwa sababu wameingia kwenye kazi ya kutumikia wananchi, kazi inayotaka uwe msafi saa zote, kazi ambayo 360 degrees Performance Apraisal haisubiri boss wako awaombe wadau waifanye

mwanakijiji
03-11-2009, 04:52 PM
Sidhani kama umri ni hoja, hoja ni umakini. Nadhani kwa hili Zitto atajifunza kupima sana misimamo yake.