PDA

View Full Version : Beware!



dRU
03-12-2009, 08:25 PM
Wanakijiji nimiona hii kweye eThinkTankTz nikaona ni bora niibandike hapa maana si wengi hupita huko.. haya tahadhari hiyo ==:eek:
===============
Beware!

WIZI ULIONIKUTA

Nimeonelea ni vema niwajulishe mbinu hii ya wizi ili isiwa fike nanyi .

Kuna kijana ambaye anadai ametoka Morogoro na ametumwa na mzee wake kununua gari kumbe ni taperi na mwizi .
Kwa kadiri ya wiki mbili kijana alikuwa akifuatilia Gari ambayo nilikuwa naiuza na nikaitangaza katika Dar - Advert . Alisema yakuwa yeye yuko Morogoro na anahitaji kuiona gari ; mnamo tarehe 25 / 12 / 2008 asubuhi, tulipokea simu yakuwa tukutane na kijana ambaye ameondoka morogoro
tumuuzie hilo gari . ( Na mpigaji akiwa ni mzee wake kutoka Morogoro;baada ya muda kijana aliomba udhuru ya kuwa tarehe 25 ni Krismasi baba yake angependa aje kuangalia hilo gari ila yeye hataweza atafika tarehe
26 / 12 / 2008 .

Saa moja asubuhi tarehe 26/12/08 alipiga simu na tukaelewana tukutane naye B.P petrol station Mbezi Beach ..tulipokutana alicheki gari kama
mnunuzi yeyote kutoka bodi mpaka engine.akaomba afanye road test -he is a good driver
Alionyesha kuridhika na gari na kuonyesha nia ya kulipia fedha ambayo alikiri iko kwa jamaa ya baba yake aliyepo jmall ambaye ni agent wa oilcom.; alipotoka j mall alidai amepewa fedha ambayo ni dollar hivyo
ilibidi tuende mlimani city kubadili fedha na kudeposit kwenye account kwani anasisitiza hapendi kulipana fedha mkononi angependa tulipane bank.

Tulipokuwa ndani ya bureau de change alikuwa akiwasiliana na jamaa zake na simu yake ilizima kwa kukosa chaji hivyo aliomba simu yangu kwa
mawasiliano pia alielezea juu ya hali yake kuwa amekunywa dawa amoxyline na tumbo linamsumbua kwani hajapata kifungua kinywa hivyo angependa kwenda kuchukua maziwa hivyo alitoka nje huku akiwasiliana kwa kutumia
simu yangu.


Kwa vile nilishakaa naye kwa muda upatao masaa matatu na juu ya yote alikuwa ameacha bahasha yake ya dollars tulipokuwa tumekaa sikupata na wasiwasi naye kabisa.
Alipotoka ndani tu katika dakika tano nilishuku hivyo nikafungua bahasha yake kuchungulia mzigo wa dolla nikakuta ni magazeti yaliyofungwa vizuri.



Haikuchukua dakika kumi watu ambao contact zao
zilikuwa ndani ya simu yangu walipokea message iliyosomeka ifuatavyo " naomba unitumie vocha ya 5000/= nitakurudishia niko sehemu hapana
duka na nahitaji sasa hivi"


Watu wengi waliibiwa kupitia kutumtumia dolla.
Ninawataarifu jambo hili kwani nimegundua limemtokea na mwenzangu ofisini siku ya jumapili 21/12/08 na mimi nilituma dolla nikifikiri namsaidia kumbe naibiwa. Kwa huyu mwenzangu mbinu iliyotumika ni sawa
kabisa na mbinu iliyotumika kwangu.nina wasiwasi wengi watalizwa na kijana huyu. Kijana ni smart, knowledgeable, polite looking, courageous na kimwili ni mdogo mdogo and very friendly during the discussions si rahisi
kumshuku

Kinachonisikitisha kijana yuko bright laiti angalitumia hizi sifa zake kufanya kazi rasmi naamini angekuwa mbali sana
Haya ...bomu hilo kaeni macho!!!!!!peleka ujumbe huu kwa watu wowote utakaoweza ili kupunguza tatizo.



____________ _________ _________ _________ _________ _______

ROSEMARIE J STEPHEN / ROSSTE@UM.DK

ASSISTANT TO THE AMBASSADOR

DIRECT PHONE +255 (22) 216 5221 / MOBILE +255 754 264 031

EMBASSY OF DENMARK, DAR ES SALAAM

GHANA AVENUE, P.O. BOX 9171

PHONE +255 (22) 216 5200 www.AMBDARESSALAAM. UM.DK

************ ********* ********* ********* ********* ********* ********* ********* ********* ********* ********* ********* ********* ********* *****
Lilian Naman
WWF Tanzania Programme Office
Plot No. 350, Regent Estate Mikocheni,
P.O.Box 63117
Dar es Salaam
Tanzania

Tel: +255 22 277 53 46
+255 22 270 00 77
+255 22 277 24 55
Cel: +255 784 303 939
Fax: +255 22 277 55 35
Email: lnaman@wwftz. org
Web: www.panda.org

mwanakijiji
03-12-2009, 10:42 PM
Duh haya makubwa kweli.. ila unajua nafikiri jinsi cellphones zinatoa huduma zao Tanzania inabidi zibadilike, nina hii feeling pia wao wenyewe wanawaibia sana wananchi.

a. Kwanini sms bado mtu ulipie nje ya huduma yako ya simu?
b. Kwanini bado kuna huduma ya kupiga kwa kutumia dakika?