PDA

View Full Version : Kikwete anahusika Kagoda?



mwanakijiji
03-13-2009, 04:06 AM
Nimejiuliza kwanini kumekuwa na ugumu wa kuwafikisha mahakamani wahusika wa Kagoda licha ya kuwa wanajulikana na kuwa waliweza kurudisha kiasi cha fedha walizokwapua? Katika pita pita yangu nikakutana na kikundi cha watu kikijiuliza hivyo hivyo.

Mmoja akatoa pendekezo kuwa itakuwaje kuwa bwana mkubwa mwenyewe naye ni mnufaika na fedha za EPA na ushahidi wake upo Dubai/Oman?

Kwa hiyo, tumsamehe kwenye hili la Kagoda na tumuache aendelee na hawa wengine?

Mponjoli
03-13-2009, 12:49 PM
Kwanza tutafute ukweli jinsi anavyohusika. Kama alihusika akijua kwamba walicheza dili, basi naye asubiri kesi yake. Lakini kama alihusika kimazingira tu, kwa kuwa watu walitumia pesa hizo kwa kampeni , bila yeye kujua, basi ajitokeze ,atueleze na aombe msamaha. Lakini wale wachoraji wa mpango mzima lazima waswekwe rumande, tukianza na RA na mpaka akina Kingunge....

jatropha
03-13-2009, 03:42 PM
Mwanakijiji mbona umetuchanganya unadai kuwa ushahidi upo Dubai/Oman. Hebu tuweke wazi kidogo tuweze kchangia mada vizuri

Mpita Njia
03-13-2009, 08:35 PM
Anaogopa nini wakati kuna kinga juu ya rais?

Dua
03-14-2009, 01:48 AM
Tunakokwenda huko hakutakuwa na kinga. Wezi wote watashughulikiwa tu acheni waendelee kujidanganya.

edo
03-14-2009, 11:29 AM
Mwanakijiji,
Siamini kama nafasi ya mtu inaweza kuwa kigezo cha kumfanya asamehewe kwani mbele ya sheria,watu wote tunawajibika kwa makosa tuliyotenda.

Huo ushahidi unaosema uko Dubai/Oman kwa nini usiwekwe hadharani? Inaweza kusaidia kutujuvya wengi!

mwanakijiji
03-15-2009, 05:39 AM
Mwanakijiji,
Siamini kama nafasi ya mtu inaweza kuwa kigezo cha kumfanya asamehewe kwani mbele ya sheria,watu wote tunawajibika kwa makosa tuliyotenda.

Huo ushahidi unaosema uko Dubai/Oman kwa nini usiwekwe hadharani? Inaweza kusaidia kutujuvya wengi!

usiwe na wasiwasi.. wiki hii mambo mengi yatazidi kufumuka..

dude
03-15-2009, 09:27 AM
so far nafahamu kalamagi alitoa 500mil katika kampeni za kikwete na ndo maana kikwete alimpa uwaziri wa nishati na madini ili akisign mkataba mmpja tu kama ule wa buzwagi awe amerudisha hela yake,we fikilia mfanyabiashara kalamagi hajawahi hata kuwa kiongozi popote pale gafla unampa wizara nyeti tena sio naibu bali ni full waziri then baada ya mda anatoka ahaa,

mujuni
03-15-2009, 07:55 PM
Dude umeniacha tuu na hizo L L L zako lazima utakuwa wa kwetu(Iringa) au sio ?

Daywell
03-15-2009, 08:16 PM
Natumaini ukweli tutaujua muda si mrefu,kama anahusika ajiandae kushtakiwa,kwani jamani tunasahau yaliyomkuta chiluba nao walikuwa na kinga kama yetu lakini sheria msumeno ilichukua mkondo wake!

kozimani
03-16-2009, 05:03 PM
Mzee mwanakijiji hilo ni swali ambalo jibu lake wazi kabisa. Hao jamaa wa CCM wamekuwa wezi