dRU
03-17-2009, 05:33 PM
Kile kipindi tulikuwa tunaimba nyimbo nyingi za kuhamasisha na wengi tulipewa hamasa hiyo na hasa sehemu kama vile makambi ya Jeshi na Mashuleni.
Palikuwa na nyimbo za hamasa za kumn’goa kaburu na hata watu waliyohusishwa na mambo kama hayo.. “tulisema.. kaburu matata hiya, hiya.. akija Kambona Chinja, akija Kaburu Chinja” na tuliendelea hata kusifu wasifu wa watu kwa nyimbo zingine za hamasa kama “Nyerere yupo, Nyerere yupo, ukiona kundi la Siasa Nyerere yupo” ..
Basi ilimuradi tulikuwa na ile tahadhari ya mara kwa mara tunakumbushwa nini cha kukipinga na nini cha kukisifia.
Sasa kipindi hiki ambacho kimegubikwa na ujanja mwingine mpya.. ukaburu mpya ama ukupe na ubepari mpya ambao sisi wenyewe waswahili kwa waswahili tunakomoana, iweje tunashindwa kuwa na nyimbo za hamasa kama zile za zama zile lakini sasa kuhamasisha watu wakawa na tahadhari ya fisadi “kwa kumtaja kwa jina na ubini wake” na tukawa tayari kusema “CHINJA”….
:confused: