mwanakijiji
03-18-2009, 12:36 AM
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/breakingnews3_phixr.jpg
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/national/klhnsiren.gif
Mbunge wa Kyela Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe kesho asubuhi anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam katika kile kinachotarajiwa kujibu madai yaliyotolewa kwenye gazeti la Mtanzania la Jumatatu tarehe 15 Machi ambapo alidaiwa kuwa anaumiliki wa kampuni ya kufua umeme na ya kuwa hakutangaza maslahi hayo wakati anaongoza Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchungwa kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond.
Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania "Wachunguzi wa mambo wanaamini kuwa ushujaa wa Dk. Mwakyembe kuishambulia kampuni ya Richmond, na baadaye Dowans, unatokana na mgongano wa kimaslahi."
Katika taarifa hiyo gazeti hilo ambalo linatajwa kumilikiwa na Mbunge wa Igunga ambaye alihusika katika kuikaribisha kampuni ya Dowans nchini Mhe. Rostam Aziz "Dk. Mwakyembe na wenzake walianzisha kampuni yao kabla ya ujio wa kampuni iliyozua utata mkubwa wa Richmond. Matarajio yao yalikuwa kwamba wazalishe umeme na kisha waiuzie Tanesco, lakini ujio wa Richmond ulionekana kutaka kuwakwaza. Richmond ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ajiuzulu Februari mwaka jana."
Kutokana na madai hayo na mengine mengi yaliyomo kwenye taarifa ya gazeti hilo, vyanzo vya karibu vya Dr. Mwakyembe vimeiambia KLHN kuwa Dr. Mwakyembe atatoa maelezo yake na vinasema kuwa "mstari uliokuwa hauvukwi kesho utavukwa".
Mmoja wa watu wa karibu wa Mwakyembe wameiambia KLHN kuwa "Dokta atawatolea uvivu kesho". Alipobanwa kuelezea ni kwa jinsi gani uvivu huo utatolewa jamaa huyo alikataa na kusema "subirini kesho". Hadi tunakwenda mitamboni jioni hii haijawekwa sawa mkutano huo utafanyika wapi lakini muda uliopangwa hadi hivi sasa ni saa nne za asubuhi.
Mara nyingi mikutano hii ya waandishi hufanyika katika ukumbi wa Maelezo katikati ya JIji la Dar. Hata hivyo baadhi ya mikutano hii imekuwa ikifanyika kwenye mahoteli na pindi tukijua mkutano utafanyika wapi tutawataarifu.