View Full Version : Maximo wa nini?
pangamawe
03-18-2009, 12:08 PM
Wadau naomba mnisaidie, hivi do we still need Maximo? Huyu jamaa tumekaa naye kwa miaka mitatu sasa na hatujapata kikombe chochote kweli tuna haja ya kuendelea naye? TFF siwashangai najua ni lazima wampigie chapuo aendelee kuwepo kwani hiyo maana yake mzigo wa kulipa mshahara wa kocha utaendelea kubebwa na ikulu. Viongozi wa TFF kweli dhamira zao zinamkubali Maximo au ni unafiki na ubinafsi tu ndiyo vinawafanya wajidai wanamfagilia. Naamini kwa support kubwa kutoka serikalini,NMB, Serengeti na wananchi kwa ujumla makocha wetu wazalendo akina Mziray,Kibadeni, Kayuni wangepewa timu ya taifa wangefanya vizuri kuliko huyo Maximo ambaye amejaa kiburi huku timu ya taifa ikiwa haina mafanikio ya kujivunia (kikombe chochote) tangu kuja kwake. Kocha kama mzazi hapaswi kuendesha timu kwa hisia na chuki kwa baadhi ya wachezaji mfano kocha amediriki kuipeleka taifa stars CHAN bila kuwa na kipa wa uhakika huku akiacha nyumbani makipa wenye uwezo mkubwa kama shaban kado na kaseja bila sababu yoyote, matokeo yake tumeyaona. Vilevile watanzania wenzangu tufumbue macho huyu kocha angekuwa mzuri kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini lazima kwa muda aliokaa hapa tungesikia akiwaniwa na vilabu na timu za mataifa mbalimbali kama ilivyotokea kwa mfaransa kocha wa Zambia ambaye baada ya kuonekana CHAN timu kibao zinamwania zikiwemo za taifa, huyu Maximo vipi? Tutafute kocha mwenye uwezo ili wahisani wetu akina NMB na Serengeti wasije kata tamaa kuona mamilioni wanayomwaga hayazai matunda. Sawa "Tuko pamoja polepole tutafika" lakini ndiyo miaka mitatu bilabila?
mwanakijiji
03-18-2009, 05:39 PM

Pangamawe, sisi hatutaki kutatua matatizo tunapenda kuyaonesha na kuyaahirisha. Kiasi anacholipwa Maximo kwa karibu miaka mitatu tungechagua vijana wa Kitanzania wapatao 25 hivi na kuwapeleka mafunzo ya juu ya ukocha au kusomea shahada za michezo leo hii tungekuwa na darasa zima lamakocha wapya wakitanzania ambao wamesomea fani hizo.
Badala yake katika wazimu wa akili zetu tuko tayari kumlipa Maximo dola elfu 10 na ushee kwa mwezi ili tushinde mechi moja au mbili za kimataifa na tujisikie vizuri.
Badala ya kujenga timu za mikoani ili hatimaye tuwe na timu nzuri ya Taifa sisi tunataka kujenga timu ya Taifa huku tukiendeleza ubovu timu za mitaani kwetu. Tumekuwa mabingwa wa kupindua vipaumbele!
Mpita Njia
03-18-2009, 08:47 PM
Tunapenda sana njia za mkato, ndio maana tubnamuona maximo kuwa bora
Tulisema tangu zamani wakati mkataba wake wa kwanza unaisha, wasimwongezee lakini hawakusikia, sikio la kufa halisikii dawa. Mwacheni amalize makombo ya walipa kodi.
ponda
03-19-2009, 04:38 PM
Hakuna umuhimu wa "MALUMBANO" kati ya "MAXIMO NA WAALIMU WENGINE" wala kufikiria kama kuna nchi zingine zinahitaji uwezo wake wa kuwahudumia,hayatotufikisha mbali katika kuleta heshima ya mpira wa kimataifa katika nchi yetu.
MAXIMO anahitajika kupewa uhuru wa kutimiza aliyoyahahidi kuyaleta katika TAIFA STARS,anahitajika pia kuheshimu na kusikiliza maoni mbali mbali ya waalimu wengine nchini kuna wengi wana kiwango cha utaalamu kutufikisha hapo "MAXIMO NA EL BASHIR" wametufikisha.
Waalimu wengine wakiacha ubinafsi na kupewa uwezo wote toka serikalini,uwezo ambao haukuwepo wakati uliyopita,uliwasimamisha kiutaalam kutufikisha tulipofikia.
Tunashukuru wakubwa wanaohusika wametukubalia na kuwapa nafasi"MAXIMO na EL BASHIR ya kuendelea.
Mhs waziri Mkuchika na Naibu Mhs Bendera wahakikishe pia
viongozi wa TFF wanahusishwa katika maswala magumu ya kutoa uamuzi wa kila siku,maoni na kiuwezo katika gharama za matumizi,bila ya hivyo kuna hatari ya kutofikia katika lengo letu la kiwango cha mpira wa kimataifa,malumbano yataendelea
Maximo analala Hoteli tangu afike Tanzania, tunaweza ku-afford hiyo luxury? Hata kama ukisoma ujinga mwingine hauwezi kubadilika.
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.