PDA

View Full Version : Kikwete in Dubai: Kukutana na Al-Adawi?



mwanakijiji
03-18-2009, 05:30 PM
Rais Kikwete na ujumbe wake wako Dubai wakiwa njiani kurudi nyumbani kutoka mkutano wake na Waziri Mkuu wa Uingereza huko London siku chache tu zilizopita. Vyanzo vyetu vya uhakika vinadokeza kuwa akiwa Dubai kuna uwezekano mkubwa Rais Kikwete kukutana Bw. Al-Adawi mmmiliki wa Dowans mwekezaji ambaye yeye alimualika kupitia Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz.


Hata hivyo, haijajulikana hadi hivi sasa kama Rais Kikwete au uongozi wa serikali unatambua kuwa kampuni ya Dowans Tanzania Limited ilianzishwa kwa kutumia false pretense pale iliposema kuwa mmoja wa wanahisa wake wakubwa ni kampuni ya Portek Systems and Equipment LTD. Hiini kwa mujibu wa nyaraka za kampuni hiyo zilizoko BRELA.

Uchunguzi wa kijarida cha leo cha Cheche unaonesha pasipo shaka kuwa kampuni ya Portek yenye makao makuu huko Indonesia haina hisa yoyote kwenye DTL kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa mara kwa mara na baadhi ya vyombo vyetu vya habari. LIcha ya hayo uchunguzi umeonesha kuwa kampuni ya Portek haijihusishi na biashara ya kufua umeme kama ambavyo iliandikwa na mojawapo ya magazeti ya Habari Corporation karibu miaka miwili iliyopita.

Chanzo chetu kinadokeza kuwa mojawapo ya maamuzi ambayo yanatarajiwa kuchukuliwa ni kuona jinsi gani serikali itaweza kuyanunua majenereta hayo licha ya upinzani mkali kwani ahadi iliyotolewa kwa mmiliki wa kampuni hiyo kuwa baadaya mkataba serikali itanunua majenereta hayo imeanza kuwa deni baada ya kuonekana ni vigumu kutekeleza ahadi hiyo katika mazingira ya sasa ya kisiasa nchini.

Hata hivyo, njia nyingine ambayo inatajwa tajwa kama desperation move ni kutokuweka timu nzito ya kuitetea TANESCO kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Mapatanisho ya Kibiashara (IAC) huko Paris, Ufaransa. Endapo TANESCO itashindwa kesi hiyo kampuni ya Dowans italipwa zaidi ya dola milioni 100 na kuzidi kwa kiasi thamani ya majenereta yenyewe.

Suala la kutaifisha mitambo hiyo haliangaliwi kwa ukaribu kama inavyodekezwa na wapasha habari wetu. "Kutaifisha wanaogopa kwani wanaona itatuma ujumbe mbaya kwa wawekezaji kuwa Tanzania inataka kurudi kuwa nchi ya kijamaa" amesema mdokezaji wetu.

Mwekezaji huyo wa Oman pamoja na washirika wake wa kibiashara bado hawajakubali kushindwa na wanatumia "ushawishi" wao wote kuhakikisha kuwa suala la Dowans linapotea katika vichwa vya magazeti ili hatimaye uamuzi wa kununua uje kutangazwa tu baadaye kuwa "ilikuwa ni lazima, tusingeweza kuacha nchi iingie gizani" tumetonywa.

Mpita Njia
03-18-2009, 08:57 PM
Kwa nini hiyo safari ya Dubai imefichwa? Alipoondoka ratiba yake haikuonyesha kuwa atapita huko!!!!

Dua
03-19-2009, 01:29 AM
Kwa nini asiende Dubai? Hivi nyinyi mnafikiri akishaacha urais atakwenda wapi? Hiyo mizoga yote anayoiacha kuichukulia hatua si patakuwa hapatoshi. Dowans ni ya JK na kundi lake la Mafisadi.