Kunjombe
03-18-2009, 08:01 PM
KWAMBA RAIS AKISTAAFU HAWEZI SHITAKIWA NI UPOTOSHAJI WA SHERIA
Kwa muda sasa kumekuwa na vuguvugu la hapa na pale juu ya kinga ambayo rais amepewa kikatiba nchini Tanzania. Mambo haya yamekuja kuwa gumzo zaidi hasa wakati huu ambapo Watanzania wameibuka na kuhoji,ikiwa ni pamoja na kudiriki kuchukua hatua juu ya viongozi mbalimbali wa nchi ambao wamekuwa kwa namna moja au nyingine wakitakiwa kuwajibika kutokana na maovu waliyoyafanya wakiwa madarakani.
Ikiwa ni katika sehemu hiyohiyo ya vita dhidi ya ufisadi nchini Tanzania zimeibuka tuhuma dhidi ya viongozi mbalimbali akiwemo aliyekuwa rais wa awamu ya tatu nchini, Mh.Ben Mkapa, ya kuwa alitumia madaraka yake vibaya alipokuwa ilkulu.
Mpaka sasa, kwa mujibu wa vyombo vya habari na tafiti mbalimbali, inadaiwa kuwa Mh.Mkapa alijifanyia Ikulu kuwa mahala pa kufanyia biashara akihusishwa haswa kwa lile jambo la kutumia mamlaka yake kujiuzia,yeye na wenziwe, mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira ambao ulikuwa unaandaliwa kwaajili ya kuzalisha umeme.
Wananchi mbalimbali wakiwepo wanazuoni, wanasheria na wanasiasa wamekuwa wakitaka Mh.Mkapa ashtakiwe kwa vitendo vyake hivyo wakidai kuwa alitumia madaraka yake vibaya hapo Ikulu. Lakini wakati haya yakiendelea wapo wanaodai kuwa pamoja na kuwa rais mstaafu alifanya kosa hilo gapaswi kushtakiwa kwa kuwa ana kinga ile iliyo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara.
Kama ni kweli Mkapa alivurunda katika mkao wake Ikulu mimi sijui itaamua mahakama hapo atakapofikishwa huko, japo utafiti umeshaonesha uvunjifu wa nsheria. Hapa katika makala hii napenda kuweka bayana kuwa sheria nchini Tanzania haimuweki mtu yeyote kuwa juu ya sheria. Na hivyo tukisema kuwa rais nchini Tanzania hawezi kushitakiwa hata baada ya kustaafu ina maana ya kuwa nchini mwetu rais hatakiwi kuishi kwa mujibu wa sheria za nchi na hivyo anaweza kufanya chochote pasipo kuwajibishwa kisheria. Mtizamo huu si sahihi.
Labda kwanza tutizame Katiba inasema nini juu ya Kinga hii kwa rais nchini Tanzania. Kwa mujibu wa upembuzi wa wale wanaodai kuwa rais Tanzania anakinga dhidi ya mashitaka wana taja Ibara ya 46 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kuwa ndiyo inayosababisha rais nchini asishtakiwe hata iweje.
Ukidurusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ndogo ya 46(1)inasema ?Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshtaki au kuendesha mashtaka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.?
Ibara ndogo ya 46(2) inaendelea kusema kuwa ? Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa analodai.?
Si hivyo tu bali Ibara ndogo ya 46(3) inaendelea kuwa ?Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10),(yaani kwa kuondolewa na Bunge) itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na ?jambo lolote alilofanya yeye kama Rais? wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.?
Ibara ndogo ya 46(1) hapo juu inampa kinga rais asishtakiwe kwa kosa la jinai wakati akiwa bado ameshika madaraka. Hii ina maana ya kuwa rais anaweza kushtakiwa. Ila tu ni mara baada ya kumaliza muda wake kama rais. Kwa hiyo jambo la msingi hapa ni muda tu. Katiba inatamka kuwa rais akimaliza muda wake anaweza kushtakiwa. Kwa mfano Mh.J.Kikwete akifanya kosa la jinai leo hii, tunachotakiwa na kipengele hiki cha sheria ni kuwa na subira tu. Akimaliza muda wake 2010 ndipo tumshitaki. Hii nadhani ipo wazi kabisa hapa.
Nikija kwenye Ibara ndogo ya 46(2) ni kwamba rais amepewa kinga ya kuto shitakiwa wakati akiwa bado madarakani ?kwa makosa yale aliyoyatenda yeye kama raia wa kawaida?, hata kama makosa hayo ameyatenda kabla au baada ya kushika madaraka, ila tu kama inapaswa kufanya hivyo basi ni muhimu kuzingatia kuwa rais anataarifiwa walau siku thelathini (30) kabla ya kufunguliwa kwa kesi dhidi yake. Hapa ni kwamba katiba inazungumzia kumshitaki rais kwa makosa yake kama Mtanzania wa kawaida. Hivyo kwa mtizamo wangu Katiba haijampa kinga rais kuwa hawezi kushitakiwa lahasha bali imeweka utaratibu ni namna gani aweze kushitakiwa(yaani kwa kupewa taarifa mwezi mmoja kabla ya kushitakiwa).
Naam,mwisho ni katika Ibara ndogo ya 46(3) ambayo inazungumzia kumshitaki rais baada ya kuachia kiti cha urais. Hapa Katiba inaweka bayana kuwa kama rais hakuondolewa madarakani na wabunge kwa utaratibu uliowekwa katika Ibara ya 46A(10) basi rais huyo hastahili kushtakiwa kwa kosa lolote allilolifanya yeye kama rais kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Hapa niweke msisitizo kwenye ?makosa aliyoyafanya yeye kama rais? kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.
Baada ya kutizama sehemu hii ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nirudi kwenye mada kama ni kweli rais mstaafu hawezi kushtakiwa kwa kuwa ana kinga dhidi ya makosa aliyoyatenda akiwa madarakani.
Moja kwa moja katika suala hili kipengele husika hapa ni Ibara ya 46 kama nilivyo ainisha hapo awali. Katika hatua hii labda tujiulize je rais akienda katika sherehe fulani huko Bagamoyo na akiwa huko akampiga mtu hata akamuua, hapo anakuwa ana kinga? Au rais akitumia mamlaka yake kule Kibaha akamnyang?anya mwananchi shamba lake katiba inamlinda? Na je rais akichukua Hifadhi ya Ngorongoro kule Arusha na kumpa rafiki yake wa kule Arabuni katiba inampa kinga? Au ikiwa rais akaona ni vema kuingia katika vita na Kenya na madhara yake watanzania wengi wakapoteza maisha na uchumi wa nchi ukaporomoka vibaya kutokana na vita hiyo, anastahili kinga kwa mujibu wa katiba?
Ili kujibu maswali hayo yote na mengine yanayofanana nayo ni budi kujiuliza swali moja tu la msingi; Je jambo ambalo rais amefanya kalifanya kama nani? Amelifanya yeye kama JK au amefanya akiwa anatimiza majukumu yake kama rais? Endapo amefanya kosa akiwa katika kutimiza majukumu yake kama rais basi hapo anakinga. Kwa mfano akiamuru nchi kuingia vitani, hata kama itakuwa na madhara kiasi gani,hii ni kwa sababu jambo hilo atakuwa ameruhusiwa kulifanya kikatiba.
Rais hana kinga pale anapokuwa amejihusisha na mambo yasiyohusiana na kazi yake Kikatiba kama rais. Hii ina maana ya kuwa inapotokea rais akaiba hapo hakuna kinga yoyote. Rais akijihusisha katika rushwa na ufisadi hapo hakuna kinga. Rais akijihusisha katika uporaji wa mali za umma na mambo mengine mengi hapo hakuna kinga na hana nafasi ya utetezi kutoka katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 kwa sababu hapo hatendi makosa hayo yeye kama sehemu ya majukumu yake, kama rais. Rais hachaguliwi na wanacnhi ili aibe. Rais hapigiwi kura ili afanye dhuluma au ufisadi.Raisi hawekwi madarakani ili awagawie rafiki zake mali za umma.Hapo ni hapana.
Ni kwa muda sasa wanajamii wengi akiwemo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Bw Hosea wamesikika akisema kuwa haiwezekani kumshitaki rais mstaafu, Bwana Mkapa, juu ya madai ya kujimilikisha Mgodi wa Kiwira kwa kisingizio kuwa anakinga chini ya Katiba. Kwa mtizamo wangu na kama nilivyojadili katika makala hii, huu ni upotoshaji wa mambo, upindishaji washeria na watu kushindwa kutimiza wajibu walionao katika taasisi husika, ikiwamo TAKUKURU.
Ni vema ikafahamika kuwa, pamoja na mapungufu yaliyomo katika Katiba ya Nchi yetu, kuendelea kufikiri kuwa rais hawezi kushtakiwa eti katiba inamlinda,huu ni ufinyu wa fikra unaobebwa na mfumo dhaifu wa ?Law enforcement? na matokeo yake inaleta tafsiri kuwa ukiwa rais nchini Tanzania basi wewe ni ?Mungu mtu.? Jambo hili si kweli na kamwe si la kulikumbatia katika nchi yetu.
Japo kuna tafsiri nyingi zinazoweza kutolewa juu ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,Tanzania, ni vema ikumbukwe kuwa kuitafsiri vibaya katiba ya Nchi yetu kunaweza kuipotosha jamii nzima na kupotosha ukweli huku tukiendelea kulea uovu katika jamii. Kama inagundulika kuwa rais aliacha majukumu aliyotumwa kuwatimizia wananchi, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri, basi na ashitakiwe ili kujenga jamii wajibikaji kwa mujibu wa sheria na taratibu zake.
----------------Mwisho---------------
Nakaribisha maoni,changamoto na mitizamo tofauti juu ya makala yangu
Na Phil Kunjombe