mwanakijiji
03-18-2009, 09:37 PM
Jamani,
Ninayofuraha kijana wetu na Administrator wetu Makange anahitimu Chuo Kikuu (Alhamisi) hii yaani kesho.
Kwa niaba ya utawala mzima wa KLHN, wanachama, wapenzi, mashabiki na wakosoaji wote tunapenda kumpa pongezi za dhati kabisa kwa kufikia hatua hii muhimu katika maisha. Pamoja na kujiandaa na kitabu kwa muda huu wote tumeweza kuwa pamoja katika kuendeleza shughuli zetu mbalimbali na hasa usimamizi wa tovuti yetu hii mahiri.
Tunamtakia mafanikio mema katika mambo atakayoanza kufanya na tunauhakika yote aliyojifunza yatatumika katika kumpa maisha ya heri na fanaka na wakati huo huo kuleta mafanikio kwa Taifa letu.
"Mama nanii.. leteni keki basi..."
M.M.