PDA

View Full Version : Kikwete afanye nini?



mwanakijiji
03-19-2009, 05:09 PM
Kuna mpasuko ndani ya CCM, kuna mgongano ndani ya chama tawala, mgongano ambao sasa unaanza kuonekana hadharani tena bila ukungu wowote. Kuna kambi kubwa tatu zinazoshindana na kutafutana kisasi.

a. Kambi ya Lowassa
Kambi hii ni kambi ambayo imejeruhiwa, kutupwa nje ya madaraka na kubebeshwa lawama za ufisadi. Ndani ya kambi hii wapo wanasiasa mashuhuri na wafanyabiashara wakubwa. Yumo Edward Lowassa, Andrew Chenge, Nazir Karamagi, Rostam Aziz, Msabaha, na wengine ambao wanaamini kuwa kujiuzulu kwa Lowassa kulikuwa ni kutokana na uonevu mkubwa.

Kambi hii ina kinyongo na CCM chama tawala kwa jinsi walivyoshughulikia suala la Richmond na hasa kwa kushindwa kukaa na kupanga mkakati wa kujibu hoja za Kamati Teule ya Bunge na hatimaye kuzuia Lowassa asing'oke. Inaamini njama au mchezo ulichezwa ili kumwaibisha Waziri Mkuu na kuhakikisha asingeweza kuendelea na majukumu yake chini ya wingu la kuhusishwa na ufisadi.

Hata hivyo hasira zao kwa kiasi kikubwa ziko dhidi ya Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa Tanzania Bw. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kushindwa kusimama na Waziri wake Mkuu wakati ule. Waliona kuwa kwa mtu ambaye alifanya mengi, na alikubali kubeba mzigo mkubwa wa kuhakikisha Kikwete anaingia madarakani the least thing Kikwete angeweza kufanya ni kusema ana imani na Waziri wake Mkuu na kuja kuwa mtetezi wake. Kwa hilo hawajamsamehe Kikwete.

Kambi hii haina mvuto au ushabiki mkubwa kwa wananchi wa kawaida. Haijasimama kukemea ufisadi, haijajitokeza kuonesha kuwa inachukizwa na yaliyotokea Benki Kuu, au kuonesha kwa namna yoyote ile inajali maslahi ya Taifa. Haijafanya hivyo na inaonekana haiwezi kufanya hivyo bila kuonekana ina unafiki.

b. Kambi ya Sitta
Kambi ingeweza pia kuitwa ya kina "mwakyembe" lakini ni wazi ni kambi ambayo kiongozi wa juu aliyemo ni Spika Sitta. Kambi hii inaamini kuwa Sitta angekuwa Waziri Mkuu lakini mchezo ulichezwa kumnyima nafasi hiyo. Lakini kambi hii haikuwa na nguvu mwanzoni hadi pale yalipotokea masuala ya kifisadi yaliyohusisha watu waliomo kwenye kambi ya kwanza. Kwao ilikuwa ni nafasi ya kuua ndege wawili kwa jiwe moja.

Wangeweza kuwashambulia wale inaoamini ni vinara wa vitendo vya ufisadi (baadhi wamo kwenye kambi ya kwanza) na wakati huo huo kujijenga mbele ya jamii na kuonekana ni watetezi wa maslahi ya nchi. Miongoni mwa mashabiki wake ni Mwakyemba, Kumba, Selelii, mama Malecela na wale viongozi wa upinzani Bungeni.

Kambi hii imejipatia umaarufu mkubwa kwa wananchi kwani licha ya baadhi ya wajumbe wake kuwa na historia kama za watu wa kambi ya kwanza, lakini wameweza kujitokeza bila haya na kuanza kutetea maslahi ya nchi huku wakiamini wako katika mapambano dhidi ya mafisadi.

Kambi Maslahi
Kambi hii ya tatu naamini ndiyo kubwa sana Bungeni na kwenye CCM Ni kambi ambayo wajumbe wake wengi wanafuata maslahi tu ya nani mwenye nguvu jiunge naye. Kambi hii iko tayari kusimama na kina Lowassa endapo kwa kufanya hivyo maslahi yao yatalindwa na wako tayari kuwa na kina Sitta endapo kwa kufanya hivyo kutafanya maslahi yao kuwa salama. Kambi hii imeundwa na wabunge wengi walio kimya ambao hawataki kuonekana wamechagua upande.

Ni kambi ambayo tunaweza kusema iko pragmatic. Ni kambi ambayo ina wazee wakongwe ambao wanaangalia kinachoendelea na wengine wanawacheka wale waliompigia debe Kikwete (japo pembeni) wakiamini kuwa walishaurri na kutaka Kikwete asipewe nafasi ya Urais lakini hawakusikilizwa. Hawa ni viongozi ambao wanaamini Tanzania inavuna matunda ya ilichopanda kwa kufuata siasa za sifa na sura.

Kambi hii inaongozwa na wakongwe kina mzee Malecela, Kingunge na wengine. Hawa ni "Wazee wa Chama" ambao wamekuwa hawasikilizwa na kupewa shavu baridi la kusikilizwa zaidi ya kuheshimiwa tuu hadharani. Wengi wa kambi hii hawarudi tena 2010 na sasa wameanza kuandaa watoto wao au warithi wa viti vyao ili kuhakikisha kuwa viti vyao au nafasi zao zinabakia karibu na familia. Kambi hii inaamua kuondoka katika siasa za Tanzania kwa namna hiyo kwa sababu wanaamini zimefikia pabaya na sasa wamechoka mikikimikiki hii ya kisiasa.

Kikwete njia panda
Aliyeko njia panda kwenye haya yote ni Rais Kikwete. Alihusiana na kuwekwa madarakani na kundi la kambi ya kwanza, lakini kazi yake kubwa ya kupambana na ufisadi inatokana na nguvu ya kundi la pili. Hawezi kuwakana walioko kundi la kwanza bila kuonekana msaliti na zaidi ya yote kwa sababu wale waliokundi la kwanza ndio wanajua mambo yake yote machafu tangu akiwa Waziri wa Nishati. NI wao wanajua nani alimsaidia kuingia madarakani na kwa namna gani.

Hawezi kwenda kinyume na wale wenye nguvu ya kambi ya pili kwani hawa ndiyo wanapendwa na wananchi. Kama anataka kuwa katika nafasi ya kushika tena madaraka 2010 hana budi kuwa popular.

Sasa amebakia kuhangaika na kulalamika pembeni.... Afanye nini?

911
03-20-2009, 05:55 PM
Rahisi tu....Aombe chama kisimpendekeze agombee urais kwa awamu ya pili.Thats the best he can do.

flein
03-20-2009, 06:47 PM
Akimaliza miaka yake 2010 aondoke

Mpita Njia
03-20-2009, 06:49 PM
Rahisi tu....Aombe chama kisimpendekeze agombee urais kwa awamu ya pili.Thats the best he can do.

Kote huko???? Aachie ngazi sasa hivi, nchi imemshinda

mwanakijiji
03-20-2009, 06:56 PM
Rahisi tu....Aombe chama kisimpendekeze agombee urais kwa awamu ya pili.Thats the best he can do.

Unajua nadhani anaweza kweli kuchukua uamuzi huo. Akifanya hivyo, huo mchakato wa kutafuta mgombea mwakani utakuwa ni kutoana ngeu!

Mpita Njia
03-20-2009, 07:08 PM
Unajua nadhani anaweza kweli kuchukua uamuzi huo. Akifanya hivyo, huo mchakato wa kutafuta mgombea mwakani utakuwa ni kutoana ngeu!

na afadhali iwe hivyo maana hayo maumivu ya kutoana ngeu yanaweza kurejesha akili zetu katika mstari, tunaweza kuanza kufikiri wenyewe badala ya watu wengine kufikiri kwa niaba yetu

hofstede
03-20-2009, 09:26 PM
Hapa cha kufanya ni rahisi kabisa. aitishe mkutano wa katiba, katiba ibadilishwe na kuwa si ya kulindana tena. Mfano, PCCB na Mwendesha mashitaka wawajibike kwa bunge na wawe huru. Tume ya uchaguzi iwe huru ili ule mchezo wa kuiba kura uwe mwisho. Akifanikiwa katika haya atapata sapoti kubwa ya upinzani na wananchi wa kawaida huku wale waliomweka madarakani wanashughuliwa na vyombo vya dola kwa ufisadi na yeye akiwa ni mwangaliaji kwani hapewi fursa ya kulinda mtu hapo.

Mambo ya maslahi ya chama mbele na Taifa nyuma ndiyo yanayomfanya akune kichwa kwa kucha. Kwa katiba ya sasa kila linalofanyika anapewa credit yeye ama lawama yeye kwani madaraka yake ni makubwa mno.

Aite jeshi, Polisi na vyombo vyote vya dola kama amiri jeshi mkuu na kuwaambia kuwa anataka kubadili nchi na mwenye maslahi binafsi aseme ili asije kuwa kikwazo. Hawa kina Lowasa, Rostam, n.k hawana jeshi hivyo anaweza kuwatosa tu, kwani kwa kufanya hivyo vizazi na vizazi vijavyo vitamuona ni shujaa aliyeibadili nchi na kuifanya kuwa ya mafanikio zaidi. Huwezi tumikia mabwana watatu ukawa salama. Ni lazima achague kundi la pili, kundi la wananchi.

Alternative ajiuzulu na kuunda serikali ya mpito kuelekea uchaguzi mkuu uliohuru na haki. Serikali hii ijumuishe vyama vya upinzani na hasa watu makini wenye kuona Taifa kwanza, chama baadae. Vinginevyo CCM itaendelea kuoneka ni genge la watu wenye maslahi binafsi ambayo wakipoteza uongozi wa nchi basi wapo hatarini kupoteza utajiri wao waliojilimbikizia kwa kuwaibia watanzania.

Pia kuendelea na hali ilivyo sasa basi Kikwete ajiandae na machafuko ya hali ya hewa huko mbeleni, ama kwa wanachi kuamua liwalo na liwe ama kundi la kwanza kumkwamisha na kuivuruga nchi. Asisubiri hayo, na wala asikae na kuomba tu mungu utawala wake uishe kwa amani bali ayakabili haya sasa ili yasilipuke baadaye. Hasira zinazojikusanya kwa wananchi sasa dhidi ya serikali yao ni bomu ambalo baadae litakosa mteguaji hata kwa mizinga na vifaru. Amani huletwa kwa kutenda haki na kuangalia waliowengi si wachache waliokuchangia na kutoa rushwa ili wewe ushinde na kuwanufaisha wao. Marekani kwa miaka mingi middle class walikuwa wanatumiwa na matajiri kuchagua viongozi wanaowataka matajiri, ila tumeona sasa hali hiyo imebadilika na serikali ipo responsible kwa wananchi zaidi ya matajiri. Tanzania pia inawezekana, Kikwete hajapoteza imani ya wananchi yeye bado ni popular kama atafanya right movie.

Mtutu wa bunduki na FFU havitoshi kuifanya nchi iwe tulivu bali haki kwa wananchi ni suluhisho la kudumu kwa nchi yetu. Toa haki kwenye KURA, toa haki kwenye KULETA MAENDELEO, anayepinga vyombo vya dola vimfikishe makamani akapate haki naye. TUSINGOJE MPAKA WATU WAANZE KUCHOMA MOTO MAGARI YA WATU AU NYUMBA ZA WATU NA KUTARGET WATU FULANI, NDIYO TUUNDE SERIKALI YA KITAIFA HAPANA!!