PDA

View Full Version : Utetezi wa wazi wa Dr. Harrison Mwakyembe



mwanakijiji
03-20-2009, 10:04 AM
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/utetezi.jpg

UTANGULIZI
Ndani ya siku hizi chache tumeshuhudia hoja ambazo zina hisia nyingi na ambazo naamini kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya yale yale mapambano ya kifikra. Hoja hizi zimejengwa hasa dhidi ya Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond ambayo ripoti yake Bungeni ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu kujiuzulu kufuatia kashfa ya kampuni feki ya Richmond.

Kuanzia matukio yale ya kihistoria ya mwaka jana hadi leo hii kumekuwepo na majaribio ya kila aina ya kumdhalilisha na kumbomoa Dr. Mwakyembe na ninaamini hili la sasa hivi limedhaniwa kuwa ndilo linaloweza kufanikiwa. Kuanzia suala la kukatiwa maji na DAWASCO mwezi wa nne mwaka jana. Wakati ule kama ilivyo sasa walioathirika na ripoti ya Mwakyembe Bungeni walionesha kufurahia kuwa hatimaye kumbe na Dr. Mwakyembe naye ni fisadi.

Katika jaribio jingine la sasa kuna imani ya kwamba hatimaye safari hii wamempata. Hata hivyo hilo ni kundi moja tu.

Kuna kundi la pili la wale ambao wanaamini katika maadili ya uongozi ambao wanaamini kuwa kwa jinsi walivyosoma na kutambua kuwa Dr. Mwakyembe naye ni mmiliki wa kampuni ya kufua umeme basi alitakiwa kutangaza maslahi hayo katika Kamati Teule (wakati wa kuzungumza Bungeni mwaka jana) na pia katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo yeye ni mjumbe. Hawa wanaamini Dr. Mwakyembe amevunja maadili na amekiuka miiko fulani.

Hawa naweza kusema wanaongozwa na kanuni.

Ni makusudio yangu kumtetea Dr. Mwakyembe dhidi ya makundi yote mawili na kuonesha kuwa hoja zao ni za kuvutia masikio lakini hazina msingi, ni dhaifu na tukiziangalia kwa karibu tutaona zina makosa mengi. Kwamba, makundi yote mawili yamekosea kwa hoja zao na kwa ushahidi wanaotoa. Tafadhali fuatana nami katika utetezi huu wa wazi wa Dr. Harrison Mwakyembe.

Unapofuatana nami hakikisha unaangalia sana matumizi ya maneno yangu kwani najitahidi kuchagua maneno vizuri kutaka kumaanisha kile ninachokisema na kusema ninachomaanisha. Ukikosea stepu usisite kurudi nyuma kunipata vizuri.

Kwa wale wageni na makala zangu za utetezi hii siyo makala ya kwanza au hoja ya kwanza ya utetezi. Huko nyuma nilisimama kumtetea marehemu Amina Chifupa baada ya ?kunyamazishwa?, nimemtetea Waziri Sofia Simba, na nimewatetea mabinti wa Nyegezi kina Nsia Swai. Na huu utetezi hautakuwa wa mwisho kwa mtu yeyote ambaye dhamira yangu inanituma kuamini kuwa aidha anaonewa au kutokana na nguvu zaidi anawekwa mahali ambapo hawezi kushinda.

karibu....

Baraka
03-20-2009, 03:10 PM
Watanzania tumegeuzwa watoto wajinga kwa muda mrefu, na sababu zinazoitwa za kihistoria zilitulemaza. hoja ya msingi hapa ni UFISADI. TUSIYUMBISHWE!! Je Mwakyembe kuwa na hisa kwenye kampuni kunaondoa ukweli wa tuhuma kuwa RICHMOND ILIKUWA UTAPELI? JE,INABADILISHA TUHUMA DHIDI YA DOWANS? nadhani tukikazania hoja tutapata ukweli wa ni nani RICHMOND, DOWANS, MEREMETA, TANGOLD. Tunaomba waandishi wa habari wajali taaluma na wasimamie ukweli wasiyumbishe ukweli kwa virushwa vidogovidogo. Mwanakijiji nakupa Hi kwa kutukumbusha wajibu wetu kwa Taifa. Mwakyembe ametuwezesha kujua kuwa tukiamua kusimamia haki yetu inawezekana. kama kuna mgongano wa maslahi tuelezwe ilishiriki vipi katika dili la rushwa ya RICHMOND na DOWANS. Ila nasikitishwa sana na Zitto Kabwe, siku za karibuni amekuwa mtetezi wa vitu visivyoeleweka, hivi huu ni msimamo wa CHADEMA?

mwanakijiji
03-20-2009, 04:58 PM
Hapa the is issue is Mwakyembe na sababu ya kuiangusha Dowans/Richmond.

Mpita Njia
03-20-2009, 07:16 PM
Hapa the is issue is Mwakyembe na sababu ya kuiangusha Dowans/Richmond.

No, wanalenga mbali zaidi-kumsafisha Lowassa is the major target