PDA

View Full Version : Kina dada watongoze?

mwanakijiji
11-11-2008, 06:46 PM
Mojawapo ya tamaduni za kikwetu ni kuwa mara nyingi ni wavulana/kina baba ndio wanakuwa wa kwanza kutamka neno la mapenzi na kuonesha mtu amemdondokea mwingine. Ni kawaida sana kwa kijana kufukuzia na kusema kilichoko moyoni.

Kuna wakati hata hivyo dada amejikuta amependa lakini kutokana tamaduni zetu anakuwa na ishara zote za "kualika" lakini hatokuwa wa kwanza kumsemesha kijana aidha kwa kuona aibu, kuonekana vibaya au kudhaniwa kuwa yuko "very cheap'. Kutona na hivyo bila kutoa ishara kwa kijana atajikuta moyo wake unamuuma pale yule anayempenda atakapoanza mahusiano na mtu mwingine.

Ni jinsi gani basi binti anaweza kumtongoza mvulana bila kujivunjia heshima?

Kepa
11-12-2008, 01:14 PM
Ingekuwa rahisi sana akinadada wangekuwa nao wanaspeak out their minds, Lakini mmmhh hapatatosha ndugu yangu mbona mashati yatachanika? Hi heri turudi kule kule kwenye enzi zetu, kazi ya kutongoza ni ya akina Anko, Shangazi, Nyanya, na Babu. ilikuwa inareta raha fulani.

anonymous
11-12-2008, 01:55 PM
Mojawapo ya tamaduni za kikwetu ni kuwa mara nyingi ni wavulana/kina baba ndio wanakuwa wa kwanza kutamka neno la mapenzi na kuonesha mtu amemdondokea mwingine. Ni kawaida sana kwa kijana kufukuzia na kusema kilichoko moyoni.

Kuna wakati hata hivyo dada amejikuta amependa lakini kutokana tamaduni zetu anakuwa na ishara zote za "kualika" lakini hatokuwa wa kwanza kumsemesha kijana aidha kwa kuona aibu, kuonekana vibaya au kudhaniwa kuwa yuko "very cheap'. Kutona na hivyo bila kutoa ishara kwa kijana atajikuta moyo wake unamuuma pale yule anayempenda atakapoanza mahusiano na mtu mwingine.

Ni jinsi gani basi binti anaweza kumtongoza mvulana bila kujivunjia heshima?

Sijui kama na mi ni mgeni katika mambo haya lakini nafikiri kama hapo uliposema "...anakuwa na ishara zote za KUALIKA ...." basi nafikiri pia huko ni kutongoza.
Au mnasemaje waungwana. Mi nafikdiri kutongoza si kuongea tu bwana. teh...teh...teh...

Kepa
11-14-2008, 09:05 PM

Anony umenichekesha sana. Mimi sidhani kama huko ni kutongoza labda tuseme huko ni kuweka mazingira safi ili mrembo atongozwe... Sijui tuite kujitongozesha??? Sasa Swali linakuja, Je utajuaje kama mdada anakutongoza bila kukwembia maneno?

mwanakijiji
11-14-2008, 09:12 PM
Kuna wimbo mmoja sijui wa nani yule anajaribu kumtongoza mtoto wa shule, halafu mtoto wa shule ananyayua mabega kukataa lakini haondoki anakaa tu hapo hapo, jamaa anasemesha mtoto anajiuma uma vidole tu mwisho anakubali.. Sasa hapo hatuwezi kusema binti amemtongoza jamaa bali alitengeneza mazingira ya kusemeshwa.

Mimi nadhani kina dada labda wanatongoza kwa kumtega mtu hasa kwenye kona kona fulani hivi kiasi kwamba jamaa anashindwa kujizuia. Kwenye madisko n.k n.k lakini sijaona bado binti ambaye anamsemesha kijana na kumuambia lililo moyoni mwake kuwa kweli amemdondokea..

Kepa
11-15-2008, 01:19 AM
Siku hizi kula kamtindo, teknolojia inasaidia kwenye simu mtu anatuma ujumbe kwa mlengwa.

My more
11-29-2008, 11:14 PM
Siku hizi kula kamtindo, teknolojia inasaidia kwenye simu mtu anatuma ujumbe kwa mlengwa.

Meseji isipojibiwa aibu, inakuchuka mwanamke unakosa raha kama nini. Heri hao hao wanaume waliozowea kupigwa vibuti. :):)

mkessy
03-06-2009, 09:55 AM
mimi nadhani kuwa kwa kuwa ni hali ya uwazi si vibaya nao wakasema yaliyoko moyoni mwao

kinadada waseme tu pale wanapoona moyo umeshindwa kuvumilia kwani kunarahisisha sana mambo maisha yako tight na wanaume wengi wanachacharika na maisha na kazi muda wa kutongoza hakuna. sasa kama dada kakupenda kwani nini asiseme? ila na wanaume tunapoambiwa au kupewa lisign fulani tusishtuke sana haya ni mambo ya kawaida kabisa.

Angeris
03-06-2009, 04:14 PM
mimi kama mwanamke nikimtamani/kumpenda mwanaume sitamtongoza straight kwa kumwambia 'kaka nakupenda'..
Kuna manjonjo mengi nitamfanyia ambao lazima atajua nia yangu juu yake. Muhimu kwanza ni kupata mawasiliano nae. Siku hizi mambo yamebadilika, inabidi uwe muwazi japo nidhamu ya uoga ipo sana kwenye kumtongoza mwanaume!

mwanakijiji
03-06-2009, 10:45 PM
Unajua kina dada wengi (msiniulize nimejuaje) wanajikuta wanakutwa na uchungu moyoni kwani yule wanayempenda wala haoneshi dalili ya kuwapenda. Wanaanza kuwa na kisirani na kina dada wanaotongozwa naye na wao wanabakia kutoka mbali tu wakimfikiria na kumuwazia. Matokeo yake ni mioyo iliyojaa masikitiko kila kukicha.

Ach-F
03-11-2009, 01:00 AM
Watongoze mara ngapi? Kila siku wanatongoza kwani kuna formula? Oooops muongozo?