PDA

View Full Version : Hoteli zaungua Bagamoyo

Mpita Njia
03-23-2009, 02:26 PM
Hoteli kadhaa, zikiwamo Paradise, Oceanic Bay na Malaika, inadaiwa zinateketea kwa moto hivi sasa

mwanakijiji
03-23-2009, 04:33 PM
Lakini hawa na wenyewe huwa wanajitakia tu.. kwanini wanatumia makuti bado? akili nyingine kwa kweli hazina akili.. !

Mpita Njia
03-23-2009, 08:20 PM
Mpaka sasa imethibitishwas kuwa ni Paradise na Oceanic bay ndiz zilizoungua na zimeteketea kabisa. Boto ulianza kwenye jiko ya Paradise baada ya mtungi wa gesi kulipuka. Fire tenders ilibidi zitoke dar na Kibaha kwenye B'moyo na wakakuta moto umeshawaka na kujizimikia wenyewe!

mwanakijiji
03-24-2009, 05:09 PM
Mpaka sasa imethibitishwas kuwa ni Paradise na Oceanic bay ndiz zilizoungua na zimeteketea kabisa. Boto ulianza kwenye jiko ya Paradise baada ya mtungi wa gesi kulipuka. Fire tenders ilibidi zitoke dar na Kibaha kwenye B'moyo na wakakuta moto umeshawaka na kujizimikia wenyewe!

Niliandika makala huko nyuma inayosema "Taifa lisilojiandaa kwa maafa, limejiandaa kwa majanga!".. ndiyo haya haya.. ile hoteli gani nyingine ya kitalii iliungua miaka kama miwili iliyopita hivi..? Was it Sea Cliff?

dickabudi
03-24-2009, 11:19 PM
Labda tuwasaidie kidogo kuhusu suala la utumiaji makuti, kule kwa Mzee Madiba upo mji unaitwa MAGHARIBISBURG una appartment na hotel nyingi za makuti, lakini makuti na nyasi zile zipo treated na ni fire proof

pia pale Mafinga, kwa Mzee Joseph Mungai yupo mwekezaji anaetreat mbao kwa ajili ya kujengea nyumba za mbao ambazo ni fire proof

Basi kwa kuwa wawekezaji wengi wa hotel ya kandokando ya bahari wanaona kuziezeka hotel zao kwa makuti na nyasi ni suala la kupendeza walazimishwe kutumia malighafi iliyofanyiwa treatment kupambana na moto unaowaka pasipostahili

Hili linawezekana