PDA

View Full Version : Mrema na Maalim Seif wastaafu Uongozi



dickabudi
03-24-2009, 12:26 PM
Wanakijiji

Tumekuwa tunashuhudia Viongozi mbalimbali inapofika wakati wanaona ni vyema wakaacha madaraka na wengine nao washike uongozi

Kuna donda ambalo mimi naona linahitaji wanakijiji kulitibia, hasa kwa viongozi wetu wawili Maalim Seif Sharrif Hamad na Augustine Lyatonga Mrema

Ninafarijika sana nikikutana na watu kama Mzee Edwin Mtei, Bob Makani wakiwa wameachia watu wengine nao waongoze vyama na wagombee nafasi muhimu katika uongozi wa nchi

Siishi hapo napo waona wazee kama Mzee Rashid Mfaume Kawawa, Mh Cleopa Msuya napata faraja sana kuona kwamba viongozi wanaweza kupumzika na kuachia wengine nao wakashika nafasi zao na kuendeleza vyama na nchi kwa ujumla

Tumeshuhudia toka ndani ya CCM, Mh Maalim Seif Sharrif Hamad akichuana na Marehemu Mzee Idriss Abdulwakil akiwania Urais wa Zanzibar, baadae akichuana na Komandoo Dr. Salmin Amour na hatimae Karume (Mtoto) bila mafanikio, na wakati wote akiwa KATIBU MKUU wa CUF tujiulize kweli hakuna wengine ndani ya CUF ambao wanaweza kushika wadhifa wa Katibu Mkuu na Maalim akawa hata Mshauri, Mdhamini wa Chama?

Je tuamini kwamba bila Maalim, CUF haina umaarufu wala mvuto kwa Watanzania? Mbona watangulizi wa Uenyekiti Taifa CUF akina Msobi Mageni wamapumzika na nyadhifa hizo zimezibwa na wengine? kwa nini kila siku Maalim na Ukatibu Mkuu kweli wapinzani tubadilike

Kwa Mh Augustino Lyatonga Mrema, TLP ina watu wengi wa kushika nafasi ya Uenyekiti wa Taifa sasa hii mizengwe kina Mutengireh wanafanyiwa ni kwa nini?
Wametoka kina Jaffu kwa udikteta wako wa kichinichini sasa na hawa waliochuka fomu nafikiri TLP wataisikia tu kwa mbali usipobadilika ,maana mwisho wa yote ni kujengewa mizengwe na tuhuma na hatimae kufukuzwa uongozi na uanachama

Tafadhalini ng'atukeni demokrasia ichukue mkondo wake ndani ya vyama vya upinzani