PDA

View Full Version : Nguvu ya Rostam ni nini?



mwanakijiji
03-30-2009, 09:36 PM
Huyu bwana inaonekana ana nguvu; nguvu ambayo inamfanya awe kwenye ndimi za watu wengi na hususan kwenye suala la ufisadi.. Jina lake linatajwa katika maeneo mengi yanayohusiana na kashfa mbalimbali..

Ninajiuliza nguvu zake zinatokana na nini?

hofstede
03-30-2009, 09:48 PM
Huyu bwana inaonekana ana nguvu; nguvu ambayo inamfanya awe kwenye ndimi za watu wengi na hususan kwenye suala la ufisadi.. Jina lake linatajwa katika maeneo mengi yanayohusiana na kashfa mbalimbali..

Ninajiuliza nguvu zake zinatokana na nini?

Nguvu za huyu jamaa ni kubwa kwa sababu amebeba siri za vigogo mafisadi wengi. Walikuwa wanamtumia huyu kama mfanyabiashara kupitishia fedha za wizi wanazoliibia Taifa. Huyu bwana hawezi kuguswa kabisa, Ila na yeye asipoangalia kama kelele zikiwa nyingi huenda atafuata njia ya balali.

Kitendo cha kumfikisha huyu jamaa kwenye sheria kinaweza kuibua mambo saba wa sabini. Wenyewe walimpa jina la "King Maker", yaani ndiyo mwenye kadi ya ushindi wa CCM kwenye Uchaguzi, kwamba bila hela CCM haipiti na mtu pekee wa kuonekana anatoa hela ambazo zinaibiwa na kwa kupitishia mgongo wake ni yeye RA

mwanakijiji
03-30-2009, 10:37 PM
Nguvu za huyu jamaa ni kubwa kwa sababu amebeba siri za vigogo mafisadi wengi. Walikuwa wanamtumia huyu kama mfanyabiashara kupitishia fedha za wizi wanazoliibia Taifa. Huyu bwana hawezi kuguswa kabisa, Ila na yeye asipoangalia kama kelele zikiwa nyingi huenda atafuata njia ya balali.

Kitendo cha kumfikisha huyu jamaa kwenye sheria kinaweza kuibua mambo saba wa sabini. Wenyewe walimpa jina la "King Maker", yaani ndiyo mwenye kadi ya ushindi wa CCM kwenye Uchaguzi, kwamba bila hela CCM haipiti na mtu pekee wa kuonekana anatoa hela ambazo zinaibiwa na kwa kupitishia mgongo wake ni yeye RA

Hofstede, katika pita pita ya kanzi mitaa ya uarabuni kalikutana na mazungumzo yafuatayo kwenye Benki moja yenye makao makuu Canada.

Mfanyakazi:"Habari za leo kanzi?"

Ka-nzi: "Nzuri tu habari za hapa Dubai"

Mfanyakazi: "kwema tu, naona mambo ya tanzania siyo mabaya bwana"

Ka-nzi: "Kwanini tena, wenzio tunabangaiza tu"

Mfanyakazi: "Hivi wenzetu mnabiashara gani siku hizi Tanzania?"

Ka-nzi: "Una maana gani?"

Mfanyakazi: "Naona hela nyingi kweli inatoka huko kwenu bwana" akajibu huku anamtazama nzi anavyosafisha mikono yake kwenye mbawa zake kujihakikisha kuwa yeye ni msafi.

Ka-Nzi: "Una maana gani hela nyingi"? kakauliza kwa udadisi.

Mfanyakazi: "Wiki hizi mbili zimepitia hapa fedha karibu dola miliioni 30 hivi kutoka Tanzania"

Ka-nzi: "Zimepita kama maji yanavyopita mtoni yakaenda zake au zimepita zikatuwama?" kakagangamala kuuliza.

Mfanyakazi: "Zimepita kama maji mtoni, zimeingie na baada ya muda zikatoweka kwenda akaunti mbalimbali na hii si mara ya kwanza"

Ka-nzi: "Wanajulikana waliopitisha au ni mizimu ya watu wa kale?"

Mfanyakazi: "Wanajulikana sana tu, wanakuja hapa mara kwa mara na kutumia watu wao hapa"

Ka-Nzi: "Ni kina nani hao?" Ka nzi kakauliza. Jamaa hakutoa jibu. Akanyanyuka kupekua kabati lake la kisasa lililoupande wa kushoto wa kiti chake. Dirisha la ofisi yake liliangalia upande wa barabara maarufu ya Sheikh Zayed. Alirudi na makaratasi kadhaa hivi ambayo yamshikanishwa pamoja kwa pini. Akayaweka mezani.

Ka-nzi: "ni watu ambao naweza kuwajua ukiwataja?" aliuliza.

Mfanyakazi:"theluthi mbili unawajua kwani mnao huko huko" alikuwa anaangalia yale makaratasi huku akitingisha kichwa. Alipomaliza akarudia tena "ndiyo karibu asilimia 75 ni watu wenu huko huko". Aliyaweka mezani. Akamuangalia nzi machoni. Kwa haya nzi akapepesa macho yake kwingine.

Mfanyakazi akachukua simu yake na kubonyeza namba fulani na mara baada ya upande wa pili kujibu akazungumza maneno kadhaa kwa lugha ya Kiarabu, na baada ya kumaliza akamgeukia kanzi.

Mfanyakazi: "natoka mara moja nisubiri hapa, nitarudi kama dakika kumi hivi". Akanyanyuka kwa ghafla akiyaacha yale makaratasi mezani. Akafunga mlango nyuma yake na kumuacha kanzi mle ndani. Kuna dirisha kubwa la kioo kwenye ofisi ya "mfanyakazi" lakini likiwa limewekwa vioo vyeusi vinavyozuia walio nje kuona waliyomo ndani, lakini wa ndani kuweza kuona kinachoaendelea.

Ka nzi kakaa pale. Kakabakia kujiuliza swali. "Ni kina nani hao".

* * *

Baada ya dakika kumi, mfanyakazi alirudi.

"Samahani, kulikuwa na jambo nashughulikia." Alisema na kuyaangalia makaratasii yake aliyokuwa ameyaacha mezani.

"hamna neno, miye ni mtu wa subira" alisema ka nzi.

"Aisee natumaini hukuchungulia haya makaratasi maana wakijue nimefungwa." aliyakusanya haraka na kuyarudisha kwenye kabati lake na kutia "komeo".

Ka nzi: "usiwe na wasiwasi mkuu". Hakukanusha.

"Kama nilivyokuambia, kuna mzungunguko wa ajabu sana wa fedha za kigeni kutoka Tanzania, ni mamilioni ya dola na watu ni karibu wale wale tu". alisema mfanyakazi. "Well, tuyaache hayo, habari za familia lakini" aliuliza.

Ka nzi: "Ni nzuri tu, ila magonjwa magonjwa tu kila kukicha"

Wakaendelea kuzungumza mambo ya familia zao huku wakikumbushana maisha yao ya ujana kabla "mfanyakazi" hajapata nafasi ya kwenda Dubai kikazi akitokea Canada. Urafiki wao umekuwa wa muda mrefu na wa pekee, mmoja akiwa ni Mtanzania mwenye asili ya Uhindi na mwingine ana asili ya Uarabuni. Walisoma pamoja shule ya Popatlal Tanga. Walisoma miaka ile ya sabini chini ya mwalimu mkuu mashuhuri Chaudry.

Walipomaliza kukumbushana walikubaliana kuonana nyumbani kwa "mfanyakazi" kwa maakuli ya jioni kwani ka"nzi" alikuwa aendelee na msafara wake maeneo ya Oman katika biashgara zake za "njugu na korosho".

Kanzi aliondoka akisindikizwa hadi kwenye lift na 'mfanyakazi'. Waliachana kwa kutakiana heri.

Alipoingia kwenye lift, ka nzi alishika mfuko wake wa nyuma. Alikuwa amekunja nakala za "makaratasi". Alijisemea moyoni "namna hii tumekwisha!". Kichwa kilikuwa kinamzunguka. Alipofika hotelini tu, hakuchelewa alichukua simu yake na kubonyeza makao makuu ya ANTI-UFISADISM INTERNATIONAL HQ".

Sauti iliyopokea upande wa pili ilikuwa ni ya kike, nyororo na yenye mvuto wote wa haiba na yenye kuweza kufamfanya simba acheze sindimba na nyoka acheze "mugongo mugoongo".

Kanzi: "Mwanakijiji pleaser!"....


The END...

Ach-F
03-31-2009, 12:59 AM
Chama cha Mafisadi watakaposhinda 2010 ndio utaona moto utakavyoanza kuwaka. Watanzania wamekuwa wavumilivu lakini iko siku hata Mugabe alikuwa haambiliki, Mobutu na madikteta kede kede walioshindwa kuendeleza mabavu. RA aendelee tu kuiba, lakini siku ya kufa nyani miti yote inateleza.

pangamawe
03-31-2009, 09:51 AM
Nasikitishwa sana na hali ya mambo inavyoendelea hivi sasa nchini, ambapo mafisadi wanaipeleka nchi puta. Hili suala la Dowans lilishamalizika kabisa kupitia mjadala wa bunge juu ya Richmond, sasa leo serikali ambayo ina deni kwa umma kwa kushindwa utekelezaji wa maazimio yote ya bunge juuya Richmond/Dowans inafanya mipango ya chini chini kutaka kununua mitambo ya Dowans kinyemela. Hili ni jambo la aibu kubwa sana na kiini cha yote haya ni fisadi mmoja wa kimataifa aitwaye Rostam Aziz. Mimi nawatia shime watanzania wenzangu tuamke tuchukue hatua stahiki tusitegemee serikali hii kufanya lolote kwani imejaa mafisadi ndiyo maana leo Wiliam Ngeleja kwa kudhani watanzania ni wajinga anataka kufananisha suala la Dowans na IPTL. Huyu fisadi Rostam Aziz alishawekeza vya kutosha kwa Ngeleja alimtoa Vodacom akamfadhiri katika kampeni za ubunge wa Sengerema hivyo Ngeleja hana jeuri ya kupingana na Rostam. Ninachowaomba watanzania hawa mafisadi tupambane nao sasa kwa kuchukua sheria mkononi tunajua wanakoishi wanakotembelea, nyumba wanazokaa tufanye lolote kuwaonyesha kuwa tumechoshwa na vitendo vyao.

Inasikitisha kuona watanzania wenzetu kwa kuendekeza njaa wanathubutu kuwasaliti watanzania wenzao kwa kutumiwa na fisadi Rostam katika kampeni za kuwachafua watanzania wanaopinga ufisadi, hawa ni kama deodatus balile, muhingo rweyemamu,deusi ngowi, prince bagenda na wengineo. Hawa nao siwakufumbiwa macho ghadhabu ya watanzania nao pia inabidi iwashukie. Lazima jambo la ajabu limpate mmojawapo ndiyo watajua sasa tumechoka wameshatuibia vya kutosha sasa ni sheria mkononi kama wanavyofanyiwa vibaka wanaokwapua simu.

pangamawe
03-31-2009, 09:54 AM
Nasikitishwa sana na hali ya mambo inavyoendelea hivi sasa nchini, ambapo mafisadi wanaipeleka nchi puta. Hili suala la Dowans lilishamalizika kabisa kupitia mjadala wa bunge juu ya Richmond, sasa leo serikali ambayo ina deni kwa umma kwa kushindwa utekelezaji wa maazimio yote ya bunge juuya Richmond/Dowans inafanya mipango ya chini chini kutaka kununua mitambo ya Dowans kinyemela. Hili ni jambo la aibu kubwa sana na kiini cha yote haya ni fisadi mmoja wa kimataifa aitwaye Rostam Aziz. Mimi nawatia shime watanzania wenzangu tuamke tuchukue hatua stahiki tusitegemee serikali hii kufanya lolote kwani imejaa mafisadi ndiyo maana leo Wiliam Ngeleja kwa kudhani watanzania ni wajinga anataka kufananisha suala la Dowans na IPTL. Huyu fisadi Rostam Aziz alishawekeza vya kutosha kwa Ngeleja alimtoa Vodacom akamfadhiri katika kampeni za ubunge wa Sengerema hivyo Ngeleja hana jeuri ya kupingana na Rostam. Ninachowaomba watanzania hawa mafisadi tupambane nao sasa kwa kuchukua sheria mkononi tunajua wanakoishi wanakotembelea, nyumba wanazokaa tufanye lolote kuwaonyesha kuwa tumechoshwa na vitendo vyao.

Inasikitisha kuona watanzania wenzetu kwa kuendekeza njaa wanathubutu kuwasaliti watanzania wenzao kwa kutumiwa na fisadi Rostam katika kampeni za kuwachafua watanzania wanaopinga ufisadi, hawa ni kama deodatus balile, manyerere jackton, muhingo rweyemamu,deusi ngowi, prince bagenda na wengineo. Hawa nao siwakufumbiwa macho ghadhabu ya watanzania nao pia inabidi iwashukie. Lazima jambo la ajabu limpate mmojawapo ndiyo watajua sasa tumechoka wameshatuibia vya kutosha sasa ni sheria mkononi kama wanavyofanyiwa vibaka wanaokwapua simu.

mwanakijiji
03-31-2009, 04:33 PM
sasa unajua huwezi kufanya hivyo kwani wao wana dola na huwezi kushindana na dola. Wao watasema wanatumia sheria kupambana na wewe. Hawa ni watu wa kuangushwa tu.

mwanakijiji
04-01-2009, 04:54 PM
Je hizi kesi zote za mafisadi zifutwe tu ili tuanze upya maana kwa kadiri sijku zinavyokwenda ndivyo tunazidi kupigwa ganzi na ufisadi; tumeanza kuuzoea?

Akajase
04-02-2009, 06:17 PM
Je hizi kesi zote za mafisadi zifutwe tu ili tuanze upya maana kwa kadiri sijku zinavyokwenda ndivyo tunazidi kupigwa ganzi na ufisadi; tumeanza kuuzoea?


mkuu, kesi hizo zisifutwe. acha ziendeshwe kama wanavyotaka wamesahau wanazidi kuutengeneza vizuri ushahidi wa namna wasivyowajibika, waongo walikubuhu na wavivu wa kukumbuka madhara wanayowaachia wananchi.
cheche za mabadiliko ya fikra zinazidi kuzaa matunda. Endelea, si muda mrefu moto utalipuka. Kuanzia kona ipi sijui; ila si muda mrefu.
"Majanga yanapozidi mioyo ya watu huota kutu" ni salamu alizopewa Kikwete na najua lakini anajifanya haoni. Ndiyo maana anawakimbia wananchi penye matatizo au kujua atabanwa kwa namna fulani, ama haendi au anakwenda lakini anakuwa mkali kwa hao watu.

Steve Dii
04-03-2009, 02:44 PM
....Sad to say, hizi ni nyakati za kutamani mapinduzi!!

mwanakijiji
04-03-2009, 04:43 PM
Rostam => Pius Msekwa
Rostam => Jakaya Kikwete
Rostam => Ngeleja
Rostam => Dr. Idris
Rostam => Salva Rweyemamu

Ach-F
04-03-2009, 10:00 PM
The buck stops with Jakaya. Wa kufukuzwa ni Mrisho.

Baraka
04-20-2009, 07:57 PM
SteveD unachosema ndiyo hasa kinachotakiwa. Inakatisha tamaa watu tunavyogeuzwa wajinga fulani tunaomilikiwa na kikundi kidigo cha watu. Wakati tunaongelea mapinduzi tunatakiwa tuwe na dhamira moja na tuwe na uelewa wa tunachokitaka. Tukiongelea mapinduzi, haohao wajanja watakuja na kuteka harakati na kutufanyia kiini macho. Tusikubali kupoozwa kirahisi tumepiga kelele, epaepa, richmond, majengo pacha, radar, sasa hivi wamekuja wachungaji na ufunuo wao wa kutengeneza hela, tumesahau yote tunacheza ngoma ya deci. Ukweli ubaki pale pale ROSTAM ndiye rais wa nchi hii maana anaogopwa kama jehanam, hashikiki hashitakiki na anatuyumbisha tusahau hoja ya msingi. Tunahitaji mapinduzi, tugangamae tusipotezwe lengo

Fingigwe
04-21-2009, 06:28 PM
Rostam => Pius Msekwa
Rostam => Jakaya Kikwete
Rostam => Ngeleja
Rostam => Dr. Idris
Rostam => Salva Rweyemamu

Kwa tathmini yangu ni kuwa nguvu ya mtu kama Rostam inatokana na tamaa na ujinga uliokithiri wa viongozi wetu wa "Chama" na Serikali - kama ipo tofauti yoyote hapo. Kwa vile wao hawakuwa na uwezo wa kuendesha mipango ya ufisadi moja kwa moja, ilibidi atokee mtu wa modeli ya mafia awafanyie kazi hiyo. Bila kusita bwana Rostam akaiona fursa hiyo ya kuwa mwezeshaji (facilitator); akawaingia kwa gia ya uhakika kuwatengenezea mipango ya uhamishiaji wa rasilimali ya Taifa mifukoni mwao kihujumu huku wakibaki na sura za heshima mbele ya jamii ya wa-TZ.
Bila shaka kazi hiyo aliifanya kwa ufanisi wa hali ya juu kama tulivyoshuhudia kwenye miradi mikubwa kama EPA, Richmond/Dowans, n.k. - acha isiyovuma sana kama Vodacom na mingine mingi tu. Kila mwekezaji mzito akikanyaga nchini anaambiwa wasiliana na Rostam kwanza upate mwelekeo. Hadi jamaa anafikia kuteuliwa kuwa mweka hazina wa "Chama" na kuingia CC ambapo wazito wengine wenye kelele nyingi hawaotei hata kuchungulia mlangoni.
Tatizo ni kuwa mtu kama huyo ni smart sana. Kwanza, katika dili zote hizo, wasijidanganye; mgao mkubwa zaidi ni wake! Hivyo, kiuchumi kawazidi kete. Na jamaa zangu wengi wanaovaa kijani na njano kila siku hata kwenye shughuli za ki-Taifa ni watu wa kuchangamkia makombo. Na hilo Rostam analijua na kulitumia vizuri sana.
Pili, kwa kuwawezesha (facilitate) viongozi kwenye mambo yao yasiyo matakatifu bila shaka huyu bwana amekusanya data zao (na za familia zao) nyingi sana mpaka za mvunguni kiasi cha kuwa tishio. Mfano mdogo sana ni jinsi alivyompunguza makali Rev. Mtikila kwa kufichua kamsaada alikomshikisha ka tumilioni tutatu hivi (kama sijakosea hisabu). Unajua mtu wa aina ya mafia ukimruhusu kuingia mpaka uvunguni kwako basi ujue kuwa umekwisha!
Ni aibu sana kwa CCM kuwa na mtu kama Rostam kwenye CC yake halafu kujaribu kutuaminisha kuwa ufisadi ni tatizo la mtu binafsi na si la Chama! Ni mantiki ya ajabu sana hii. Mh. Mpendazoe kasema kweli - wawaondoe mafisadi ndani ya Chama kama wanajali uhai wake siku zijazo. Mtu kama Rostam si wa kuchekea: atakisambaratisha Chama ilihali wakishuhudia kwa macho yao.:mad:

Baraka
04-21-2009, 11:28 PM
Wakati tunaelekeza shutuma kwa serikali? CCM? nadhani inabidi tujiulize huyo CCM ni nani? Huyo serikali ni nani? Hii ndiyo sababu natahadharisha kuwa wote tunahusika na ujinga huu, ni sisi tunaopiga kura kuwaingiza ingawa tunajua picha nzima. Sasa hivi group la mafisadi wana vikao na hawalali, mara wanakutania Dubai, mara wako golden tulip na kona zote wanazozijua, utafikiri tumelogwa, wale waandishi wa habari wanaoonekana kuwa jasiri, wanaalikwa na kupewa mshiko, ndio imetoka!!! watanzania tunabakia kupewa taarifa za kuchonga ukweli ukiachwa kutumaliza.

Kutojiamini ndiko kunakotuponza pamoja naviongozi wetu ndio maana 'watoto wa mjini' wameenda kununua PhD kwa dola alfu tatu na kuja kufakamia uongozi. Jamani mwizi ni mwizi, awe wa kuku au elimu. Amekosa uaminifu na kuiba taaluma, anapewa uwaziri wa sheria, analetewa mikataba hata kuelewa haelewi, itabidi wajuaji kama Rostam washikilie hapo!! na kuokoa jahazi kwa ufisadi. Sikushangaa wakati ishu ya EPA ilipotoka na kagoda kutajwa waziri wa FEDHA akasema ile ilikuwa ni kwa ajili ya shughuli nyeti za serikali. Jamani kwa mtaji huu Rostam ndiye rais wa Tanzania ana kinga zote. watamgusaje wakati ndiye anayefafanua mikataba na sheria zote kwa niaba yao?

dRU
04-24-2009, 01:36 PM
Labda kwa kudodosa tuu hii inaweza kuwa ndiyo sababu kubwa ya miguvu ya huyu Mheshimiwa

Jina Kamili: Rostam Abdulrasul Aziz
Kazi: Director Caspian Construction Ltd
Director Tanzania Leather Industries Ltd
Director African Tannaries Ltd
Director Africa Trade Development
Managing Director Research on Business

dRU
04-24-2009, 01:42 PM
Kwa nyongeza zaidi labda taarifa kama hii itazidi kuwapa wanakijiji mwanga wa kumtambua Mheshimiwa Rostam Abdulrasul Aziz


HEADLINE: CCM magnates in the media

The treasurer of the Chama cha Mapinduzi (CCM) and advisor to the government party on economic and financial issues, the businessman and MP Rostam Aziz has recently acquired a significant stake in the largest press company in the country, Habari Corporation Ltd (HCL).

And yet he is not a newcomer in the Tanzanian press sector, since during the 1990s he had launched the company Mwananchi Communications Ltd (MCL) in partnership with Ferdinand Ruhinda, a former ambassador turned businessman and close ally to former President Benjamin Mkapa.

Aziz and Ruhinda subsequently joined forces with the Aga Khan's Nation Media Group to launch a daily English language newspaper, The Citizen.

They later disagreed with their Kenyan partners over the coverage of Jikaya Kikwete's election campaign last year. A few months ago Aziz therefore sold a large proportion of his shares in MCL and purchased the stakes held by several journalists (Salva Rweyemamu, Jenerali Ulimwengu and William Shoo) in HCL. Since then this press group which was quite virulent under the previous regime has calmed down considerably with the present government. Other CCM dignitaries also have interests in the media. This is so in the case of Minister of Livestock, Anthony Diallo the owner of Sahara Communications Ltd which operates Star Television and Radio Free Africa as well as publishing the weekly magazine Msanii Afrika.

For its part, the IPP Media group (The Guardian Ltd, Media Solutions Ltd, Independent Television and Radio One Ltd) owned by the magnate Reginald Mengi has always been able to butter up successive governments. However, today he is in the line of sight of several CCM executives due to some of his news stories.

dRU
04-24-2009, 01:45 PM
Mwisho wa kauchunguzi kangu ninabandika hili hapa tena la Mheshimiwa
Licensed

Vodacom Group was licensed in December 1999 to operate a GSM cellular network in Tanzania and formed the subsidiary company Vodacom Tanzania Limited. The Group also has operations in Lesotho and the Democratic Republic of Congo (DRC).

When Vodacom entered in Tanzania there was one GSM 900 MHz cellular operator, Tritel, on the mainland of Tanzania with 15 to 20,000 active subscribers and another which was operating exclusively on the island of Zanzibar. There was also an analogue cellular network operator, MIC Tanzania Limited (tiGO), with active subscriber base of 40 to 50,000. tiGo was known as Mobitel when started its operation within the country in late 1993. There was also one government owned fixed-line telecommunications operator,Tanzania Telecommunications Company Limited, TTCL. Vodacom Tanzania was the third licensed network operator in Tanzania and became the largest mobile communications network operator in the country within one year of launching.

Vodacom Tanzania Partnership

It has been claimed that Vodacom Group has a habit of choosing politicians and their friends as business partners to extends its operations on the continent [6]. It was reported by The Mail & Guardian that Mozambican President Armando Guebuza had become a shareholder in Vodacom Mozambique.

Vodacom Tanzania was licensed in Tanzania with its local partners Planetel Communications holding 36% and Caspian Construction holding 16%. Later Planetel decreased its stake to 16%, while Caspian’s increased to 19%[6].

A representative of Caspian on the Vodacom Tanzania board is businessman-politician Rostam Aziz, a close supporter of President Jakaya Kikwete. At the time Vodacom was licensed in Tanzania, neither man was quite as powerful as now.Kikwete was Foreign Minister and Aziz had yet to occupy any formal position in Tanzanian politics.

While spreading its political bets, the CCM's and the former Speaker of Parliament Pius Msekwa was granted Vodacom Tanzania’s non-executive chair between 2003 and 2005. When Vodacom Tanzania hosted a “VIP gala night” to bid farewell to outgoing president Mkapa in December 2005, Msekwa attended, presumably in both capacities.

jingo
04-25-2009, 10:13 AM
HILI PAPA LA UFISADI NASIKIA LINA URAIA WA NCHI TATU!
NA LIMESHIRIKI KIKAMILIFU KUPANGA SAFU ZA UONGOZI KWA LENGO LA KUMUWEZESHA YEYE BINAFSI KUPATA MASLAHI,KUHUJUMU NA KUIFISADI NCHI YETU!
HANA CHA KUPOTEZA KWANI AKIPATA HOFU KUHUSU USALAMA WAKE ANHAMA!
KWA SASA WANASEMA HAKUNA SHERIA WALA MAMLAKA HAPA NCHINI INAYOWEZA KUSUMBUA...YAANI SHERIA NA WALE WANAOZISIMAMIA NI KAMA KAMBA ZA MGOMBA UKIMFUNGA NAZO ATAZIKATA KIULAINI!
NI HATARI KUWA NA WATU WA AINA HII AMBAO WAPO JUU YA SERIKALI.......NA WANAFANYA UOVU WA KUTISHA!
NATAMANI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS K.NYERERE ANGELIKUWA KUWA HAI KWANI KILA MTANZANIA MWENYE UCHUNGU NA UZALENDO NA NCHI HII ANJUA NI HATUA GANI BABA WA TAIFA ANGELIMCHUKULIA MTU WA AINA YA aziz rostam..
MNAKUMBUKA HATUA ALIZOPATA CHUKULIW YULE GIRIKI ALIYETANGAZA KUW SERIKALI YA MWALIMU IPO MFUKONI MWAKE??

Akajase
05-01-2009, 07:29 PM
Wakati hali inazidi kuwa mbaya na wananchi kuzidi kuchoshwa na hali iliyopo REDT wanakuja na ripoti yenye data za kutengenezwa [kwenye gest house,basi au nyumba ya mtu hilo ni swali lingine].

Ukiowanisha na mada REDET wamefanya hivi kwa maslahi ya nani? Je! huyu RA katia mkono kinamna hawa jamaa watoe ripoti ovyo kama hiyo?

Au ni maandalizi ya wizi wa kura mwakani kwamba ukutokea ushindi mkubwa watu waamini kuwa hata REDET walisema toka 2009?

Kunjombe
05-06-2009, 05:59 PM
Mimi naungana nanyi wakuu hapa but mimi nasisitiza tu kuwa Watanzania sasa tuseme NO kwa ufisadi. Tuseme No kwa viongozi wanaochaguliwa kwa kulipana fadhila, tuseme NO kwasababu sasa inatosha, it is too much! Things must change, iwe ni kwa njia yoyote, lakini jambo la msingi Wananchi ni lazima tubadilike tuache kupiga kura kwa kupewa T-Shirts na Khanga, maana ni kwa kutojua nani ni kiongozi anayefaa ndipo tunakimbilia kuwapigia kura mafisadi nao wanaendelea kutunyonya, kutuibia na kutukandamiza. NO it is enough sasa.

mwanakijiji
05-06-2009, 11:35 PM
Na. M. M. Mwanakijiji (MwanaHalisi)


Sasa najua kwanini waliliua Azimio la Arusha kule Zanzibar na kulizika bila kuliswalia dua za mwisho wala kulifanyia ibada ya mazishi. Sasa najua kwanini jina lake azimio hilo limefutwa milele kwenye vinywa vyao. Mwenzenu sasa nimetambua ni kwanini kabla ya kuanzisha wizi wao mkubwa wa mali na utajiri wa nchi yetu na kugawana wao kwa wao na watoto wao ilibidi kwanza kabisa wakiondoe kizuizi pekee kilichokuwa kati yao na urithi wa wana na mabinti wa taifa hili. Sasa najua, kwanini vita hii dhidi ya ufisadi ni vita ya kugombania hatima ya taifa letu!

Azimio la Arusha lilipotangazwa lilikuwa na lengo la kuhakikisha kuwa utajiri wa nchi yetu unagawanywa kwa wananchi wa taifa hili. Lengo la Azimio halikuwa kugawana umaskini bali kugawana utajiri. Leo hii, wao wanagawana utajiri sisi tunatakiwa kugawana umaskini. Na wakati wowote tutakapojaribu kutaka kugawana utajiri wetu wao (wetu) ndivyo hivyo hivyo mapambano haya yatakuwa magumu zaidi.

Kinyume na watu wengine wanavyoona, ninaliona sakata la Mengi na wale aliowaita kuwa ni ?mapapa wa ufisadi? kuwa ni mapambano ya kugombania urithi wetu. Alichofanya Mengi na Mwakyembe kabla yake na wale waliochapisha ile taarifa ya ?Tanzania?s Mafia? iliyoanzisha sakata hili la kwenye mtandao wa Jamiiforums.com ni kutukumbusha kuwa hatuwezi kamwe kuuachia urithi wa nchi yetu mikononi mwa kikundi cha watu wachache.

Ni kile kile kilichofanywa na Dr. Slaa na kundi la wapinzani pale Mwembe Yanga walipotangaza ile Orodha ya Aibu ya mafisadi. Ni kile kile kilichopigiwa kelele Bungeni na kina mama Kilango na kina Mkumba. Ndiyo, ni sehemu ile ile ya mapambano ya kugombania urithi wetu. Kama watu wanafikiria hili ni suala la Mengi na Manji au Mengi na Rostam basi wanakosa kuiangalia picha nzima. Wanaona sehemu sehemu tu.

Kwani, Mengi akikaa kimya, mama Kilango akifunga kinywa chake na kina Mwakyembe wakisalimu amri, haitakuwa mwisho wa mapambano. Watakuwa wamekubali kama walivyokubali wabunge wengine na watumishi wengine wa serikali kuwa sehemu ya utawala wa himaya ya kifisadi inayoongozwa na watu wanaokula kwa mikono miwili bila kunawa, na wanakula siyo minofu tu ya kuku, bali wanakula miguu na firigisi pia, tena wanakula bila kutaka waulizwe! Tukiwauliza wanatuelekeza kwenye kula utumbo!

Ndugu zangu, yawezekana kuna mgongano wa kibiashara, yawezekana kuna chuki au kinyongo cha mambo fulani lakini hayo yote hayaondoi ukweli kuwa hatima ya taifa letu inashikiliwa na kundi la watu wachache; kundi ambalo halitaki kuulizwa, halitaki kuhojiwa na kwa hakika halitojitolea hata siku moja kutoa majibu zaidi ya kutisha watu na kutufanya tuishi kwa wasiwasi.

Wapo watu wengi na wenye nguvu ambao majina yao yanajulikana, uwezo wao unazidi makisio na nafasi yao katika jamii ni sawa na wana wa mfalme fulani. Watu hawa wamechukulia kuvunjwa kwa Azimio la Arusha kama kibali cha wao kutunyonya kama wana akili fyatu. Na wanatufyonza kama mtu anayefyonza ganda la muwa na kuliacha kapi.

Katika watu ambao wanaunda kundi hilo, kundi ambalo naamini lina nguvu kuliko inavyofikirika wapo wengi. Watu hawa hawana rangi, kabila au dini, ni wanyonyaji wa hali ya juu (nafahamu neno ?mnyonyaji? kwa wengine ni geni). Wamejikita katika siasa na utendaji wa nchi yetu na katika kufanya hivyo wamejitengenezea himaya yao ya ufisadi. Chini yao wana watu ambao nimewaita makuwadi wa ufisadi na hivi karibuni tumeona siyo makuwadi tu wa ufisadi waliopo bali pia wametengeneza vikaragosi vya mafisadi!

Miongoni mwa watu hao ambao wamechota utajiri wetu kama kutoka kisimani huku wakiturishia vimifupa kama mwizi anavyomrushia mbwa nyama ili asibweke sana wapo watumishi wa umma, wanasiasa na wafanyabiashara. Watu hao wana mtandao unaotisha, mtandao ambao ni imetengeneza pembetatu ya ufisadi (the triangle of corruption). Pembetatu hiyo inahusisha wafanyabiashara, wanasiasa na watendaji serikalini.

Katika pembetatu hiyo kuna watu watatu ambao ni lazima niwataje hapa, yupo Sir. Andy Chande, yupo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na yupo Mbunge na mfanyabiashara maarufu Mhe. Rostam Abdulrassul Aziz (Igunga ? CCM). Hawa watatu ndio naamini wanaunda mhimili wa ufisadi Tanzania (the axis of corruption). Chini yao kuna makumi na mamia ya watu ambao wanatekeleza majukumu yao mbalimbali kuhakikisha kuwa pembetatu hiyo ya ufisadi haivunjiki.

Chini ya hawa watatu wapo ambao tunaweza kuwaita makuwadi wa ufisadi. Hawa ni watendaji serikalini ambao wamekubali kuuza haki yao na utu wao na uhuru wa Taifa letu kwa bei. Hawa ni wasomi waliokubuhu na watu ?wazito? tu lakini kutokana na ahadi ya utajiri wa haraka haraka wamekubali kupinda sheria, kuvunja sheria na wakati mwingine kuiharibu sheria ili kurahisisha uporwaji wa mali za taifa letu. Ndiyo hawa waliorahisisha wizi wa Benki Kuu, ndiyo hawa waliofumba macho wakati nchi inabakwa na ndiyo hawa hawa ambao leo hii wengine wamefikishwa kizimbani. Lakini wengi bado wapo katika maofisi na taasisi mbalimbali.

Hawa si watu wenye vyeo vya chini bali ni Wakurugenzi, Wenyeviti wa Bodi na watu wazito kwenye baadhi ya taasisi zetu nyeti. Wengi wa hawa waliteuliwa na kupewa nafasi zao za juu kutokana na maamuzi au mapendekezo ya mhimili wa ufisadi. Hawa sasa hivi wameshibishwa neema ya nchi yetu.

Pamoja na hawa serikalini kuna makuwadi wengine kwenye siasa ambapo baadhi ya Watanzania wenzetu walikubali kununuliwa kwa bei ya chini ili waweze kupewa nafasi ya kushinda uchaguzi. Wengi wa hawa ni wanasiasa walionufaika kwa namna moja au nyingine na fedha za Mhimili.

Katika kuwafikia watu hawa hakuna mtu mwenye nguvu kubwa kama Rostam. Rostam ametoa ufadhili kwa wanasiasa mbalimbali na kuwasaidia kushika nafasi zao walizonazo sasa. Katika kufanya hivyo amejihakikishia kundi kubwa la watu watiifu kwake. Watu hawa ambao amewasaidia wengi wamesainishwa misaada hiyo (kama alivyomfanyia Mtikila) na hivyo kujikuta hawana uwezo wala ubavu wa kusema kitu chochote dhidi ya Rostam.

Katika kufanya hivyo utaona kuwa Rostam amepanga mojawapo ya safu ya makuwadi wake ambao siyo tu wana nafasi lakini pia wana nguvu kubwa mno. Tukumbuke kuwa aliyekuwa Meneja wa kampeni ya Urais wa Rais Kikwete ni Bw. Rostam Aziz (wakati huo akiwa pia mweka hazina wa CCM).

Kwa nafasi yake hiyo Rostam alijua kila senti iliyokuwa inaingia na kutoka kwenye kampeni ya Kikwete. Ni yeye ambaye alihusika kwa kiasi kikubwa katika kuchangisha fedha za kampeni hiyo. Tunapojiuliza fedha za kampeni za Urais wa Rais Kikwete zilizotoka wapi jibu analo Rostam!

Kwa watu wanaokumbuka (kama mzee wenu hapa) Rostam alihusishwa na kutajwa na gazeti maarufu la Africa Confidential kuwa alipokea kiasi cha dola milioni 2 kutoka Oman kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi. Kiasi hicho ni kingine ya kila kilichotajwa na Christopher Mtikila kuwa kilitoka Iran (kupitia kwa Rostam) na ambacho kilitumiwa katika mchakato wa kumtafuta mgombea wa CCM.

Vyanzo vyangu vya karibu kabisa vimenidokeza kuwa kiasi kilichotoka Oman kilitolewa na mfanyabiashara maarufu aitwaye Gen. Suleiman Al-Adawi ambaye alikuwa ni kigogo na msaidizi wa karibu wa Sultani wa Oman. Gen. Al-Adawi ni mzaliwa wa Zanzibar ingawa si raia wa Tanzania.

Wakati huo Kikwete alitishia kulifungulia mashtaka gazeti hilo lakini hakufanya hivyo. Ukweli ni kuwa Kikwete hakujua fedha zimetoka wapi kwani alimuamini Rostam na hivyo hakukuwa na kesi siyo dhidi ya hilo gazeti tu bali hata Mtikila hakushtakiwa na hivyo kuwapa nguvu kuwa madai yao ni ya kweli.

Hata baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani tunawaona watu mbalimbali waliohusiana na Rostam wakishika nafasi mbalimbali za utendaji na tena kwenye sehemu nyeti. Aliyetaka kugombea jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM ambaye alikuwa ni mtumishi wa Wizara ya Nishati na Madini Dr. Peter Kafumu aliyekuwa anaonesha kutoa ushindani mkubwa kwa Rostam alijikuta anakaa pembeni na kumpisha Rostam kwenye kiti hicho. Inadokezwa kuwa kwa kufanya hivyo atakumbukwa katika awamu mpya. Rostam akawa hana mpinzani kwenye kura za maoni!

Baada ya kuchaguliwa Rais, Kikwete alimkumbuka Bw. Kafumu kwa kumteua kuwa Kamishna wa Madini. Hili inadaiwa lilikumbushwa na Rostam.

Barua iliyotoka kwa Salva Rweyemamu (alikuwa mhariri wa Habari Corporation) kwenda kwa Rostam ilivujishwa karibu wiki mbili zilizopita. Katika barua hiyo ambayo imewafungua watu wengi macho inaonesha ni jinsi gani Rostam (RA kwa kifupi) amekuwa na nguvu mno. Katika barua hiyo ambayo sehemu kubwa ni jinsi gani Rostam aliacha kampuni aliyoinunua kufanya kazi kinyume cha sheria (bila kusajiliwa)) ilikuwa na sehemu ya mambo binafsi pia ambapo kimsingi Salva anaonekana akimkumbusha Rostam juu ya ahadi yake/zake kwake.

Inaonekana katika barua hiyo Salva alikuwa hajakumbukwa na awamu hiyo mpya na akawa anashangaa inakuwaje baada ya jitihada zote (kwenye vyombo vya habari wakati wa kampeni) yeye hajakumbukwa. Akamhoji Rostam kama ndivyo wanasiasa wanawatenda wale watu walio karibu nao na waliowasaidia kushika madaraka. Wiki chache baadaye Salva Rweyemamu akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Rostam alimkumbuka tena.

Aliyekuwa Wakili wa Vodacom (Mkuu wa kitengo cha sheria) na ambaye alisaidiwa na Rostam kuingia kampeni ya uchaguzi wa Ubunge kule Sengerema ni Bw. William Ngeleja. Wakati akiwa Vodacom mmoja wana hisa wa kubwa alikuwa (bado ni) Bw. Rostam Aziz. Baada ya uchaguzi wa 2005 ambapo Ngeleja alishinda Sengerema, Kikwete hakumsahau kwani alikumbushwa na Rostam. Kwanza kama Naibu Waziri na baada ya matukio ya mwaka jana kuupata Uwaziri kamili.

(Hadi hapa tunawaona watu wawili wanaohusiana na Rostam wakiwa wizara moja).

Mtu mwingine ambaye tunamkuta ni Bi. Badra Masoud ambaye aliwahi kuwa mhariri wa Habari Corporation (pamoja na kina Salva). Huyu alitoka Habari na kupata ajira kule DAWASCO na baadaye Tanesco kama Afisa Mawasiliano. Akiwa DAWASCO wengi watakumbuka ndiye aliyetangaza kukatiwa maji kwa wadeni sugu akiwemo Dr. Mwakyembe. Habari hizo zilikuja wiki chache tu baada ya ripoti ya Richmond Bungeni. Lengo lilikuwa kumchafua Dr. Mwakyembe kitu ambacho kilishindwa baada ya kuonekana kuwa jaribio hilo limeshindwa.

Siyo yeye tu pale Tanesco bali pia Mkurugenzi wa Tanesco Dr. Idris Rashid ambaye naye ametoka huko Vodacom. Tukumbuke kuwa huko Vodacom Rostam ana hisa kubwa tu na hivyo kuwa na mtu kule Tanesco pia ni jambo la kuangalia sana kwa karibu.

Katika sakata la Richmond na Dowans jina la Rostam linatajwa. Kinyume na taarifa yake ya juzi kuwa ripoti hiyo haikumtaja kwa jina. Tukumbuke vizuri kuwa katika mkutano wake wa waandishi wa habari mwaka jana Bw. Rostam alizungumza kana kwamba haijui kabisa kampuni ya Dowans na kuwa aliacha tu kadi yake tu na kuwa alienda tu kuomba kazi.

Alinukuliwa kusema ?Mimi ni mkandarasi. Nina kampuni inaitwa Caspian. Sina uhusiano na Dowans ingawa niliomba kupatiwa kazi ya ukandarasi.. Nilipoomba kazi kama mkandarasi, nilitakiwa kuacha anuani, unapoomba kazi lazima uache anuani? Maneno yake ya wakati ule yaliwaaminisha watu wengine kuwa Rostam haijui Dowans!

Ukweli (ambao sasa tunaujua zaidi) ni kuwa Rostam ndiye aliyefanikisha ujio wa mmiliki wa Dowans na kumsaidia kuweza kuanzisha kampuni hewa ya Dowans Holdings SA ya Costa Rica. Mmiliki huyo ambaye nyaraka za BRELA zinamuonesha si mwingine bali ni rafiki wa karibu na mshirika wa karibu wa Rostam Gen. Suleiman Al-Adawi ambaye ana undugu na mahusiano ya karibu ya kifamilia na Watawala wa Falme za Kiarabu. Rostam hakuwa mkweli wakati ule na kama angetaka kuwa mkweli angesema wazi mapema mahusiano yake na watu wa Dowans!

Naweza kuendelea kuandika mifano mingine mingi na watu wengine ambao Rostam amewasaidia katika kampeni za uchaguzi (nina majina karibu ya wabunge 40 ambao ?wako mfukoni? mwake). Wabunge ambao ninawaita kuwa ni makuwadi wa ufisadi. Hawa msitegemee hata siku moja kuwaona wanapiga vita ufisadi au kupiga kelele juu ya uporaji wa mali zetu.

Jinsi ya kuwagundua wabunge hawa ni pale wanapozungumzia ufisadi. Wao wanasikika wakisema ?vita ya ufisadi ni vita yetu sote?. Utawasikia wakisema ?mtu asitumie vita ya ufisadi kujinufaisha kisiasa?. Kamwe hata hivyo hutawasikia wakipigia kelele Kagoda, EPA au kutaja majina ya watu ambao wanahusika na ufisadi. Watasikika kwa haraka kumlaani Mzee Mengi kwa jina lake lakini hawatasika kumtuhumu Rostam au vigogo wengine kwa majina yao.

Chini ya hao (makuwadi wa ufisadi) utawakuta vikaragosi vya ufisadi. Hili ni kundi kubwa la waandishi wa habari, na watendaji wa ngazi za chini wa CCM na wapambe wengine au mashabiki ambao kila mabwana zao wanapoguswa hufanya haraka kuwasafisha na kuwatetea. Wengine hufunga safari toka mikoa ya mbali ili waje wasikike. Vikaragosi hawa wapo hadi kwenye timu zetu za mpira na ambao ?mfadhili? wao akiguswa wanakuja na kelele kuwa anaonewa ingawa wengine tunajua yaliyotokea Mbagala wiki iliyopita yawezekana kabisa kuhusishwa na biashara za mfadhili huyo!

Vikaragosi hawa wa ufisadi ni wale ambao bila haya wala soni wako tayari kuuza utu wao, hadhi yao na heshima yao ili wafadhiliwe. Ndiyo watu wa hatari pia katika mapambano haya kwani bei yao inajulikana. Ujumbe wetu kwa hawa wote (Pembetatu ya ufisadi, Mhimili wa ufisadi, makuwadi wa ufisadi na vikaragosi vya ufisadi) ni kuwa sasa imetosha iachieni nchi yetu! Mmeishikilia vya kutosha na sasa mnataka kututumikisha milele. Mmeuza urithi wetu na utajiri wetu mmegawana; leo mnataka sisi tugawane umaskini wetu wakati nyinyi mnamegeana utajiri wetu. Sasa yatosha!

Labda niwakumbushe mbiu ile ya Azimio la Maskini!

?Tumeonewa kiasi cha kutosha, Tumenyonywa kiasi cha kutosha,
Na tumepuuzwa kiasi cha kutosha; Unyonge wetu ndio umetufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge wetu ili tusionewa tena, tusinyonywe tena?!

Ni mimi: Mwanakijiji@mwanakijiji.com

mnyilula
05-07-2009, 12:15 PM
ukiangalia msururu wa watu aliowaweka[RA]madarakani unaona ilivyo vigumu[angalau kwa sasa]kumshikisha adabu mtu huyu,aliaza kuwekeza kwenye hizo nguvu zake muda mrefu sana,na sasa ameota mizizi ambayo ili kuing'oa inahitajika nguvu kubwa kwelikweli,je nguvu hiyo ipo?kama ipo ipo tayari kufanya kazi hiyo?maana wenye nguvu ya kushughulikia wanaweza wakawepo,lakini utashi wa kufanya hivyo wakawa hawana,
ila ni suala la muda tu,hakuna marefu yasiyo na ncha,na sasa angalau mwanga unaweza kuaza kuonekana kwa mbaliiiiiiii.

Atubonekisye Massapa
05-07-2009, 02:06 PM
Mwanakijiji,
Asante sana kwa habari zako. Pamoja tutashinda. Ni swala la muda

flein
05-07-2009, 07:03 PM
Asante kaka Mwanakijiji,
Mimi nafikiri tunachotakiwa ni kuwamwaga CCM hilo tu itamaliza kelele zote hizi. Sijui kama mnajua kashfa nyingi za ufisadi tunazosikia sasa ni hizi za karibuni yaani JK alipoanza kazi? Ninyi mnajua JK aliwahi kuwa waziri wa Fedha je hamwoni kuwa hata yeye ameshasaini EPA? Hawa CCM hawana msafi hebu tuwapumzishe kwanza.
Nasema hivi kwakuwa mtu hachezi dili pekeyake anawashirikisha walioko kwenye barabara ya hela, mfano Lowasa, msabaha, karamagi. Hivyo unaweza mweka Sam Sita eti raisi halafu tukajuta, maana kama ni msafi asingembana DK. Slaa kuwasilisha hoja binafsi ya mafisadi.
Kwa ufupi ndo hivyo, tuache kulalama eti hawa akina RA, PATEL ETC, tujadili namna gani tunawamwaga CCM, tupeane mbinu tuelimishane namna ya kuhamasisha wenzetu maana watz wengi wanajua siasa dhambi ila wanalia maisha magumu.

Kaka mwanakijiji hebu anzisha mjadala wa namna gani tutawamwaga hawa CCM, tuanze kupeana mbinu za kuwahamasisha watu jamani tukiendelea na mafisadi tutahamaki uchaguzi huo lakini sisi wanyonge hatutokuwa na umoja na mtazamo ulio sawa.

flein
05-07-2009, 07:13 PM
ukiangalia msururu wa watu aliowaweka[RA]madarakani unaona ilivyo vigumu[angalau kwa sasa]kumshikisha adabu mtu huyu,aliaza kuwekeza kwenye hizo nguvu zake muda mrefu sana,na sasa ameota mizizi ambayo ili kuing'oa inahitajika nguvu kubwa kwelikweli,je nguvu hiyo ipo?kama ipo ipo tayari kufanya kazi hiyo?maana wenye nguvu ya kushughulikia wanaweza wakawepo,lakini utashi wa kufanya hivyo wakawa hawana,
ila ni suala la muda tu,hakuna marefu yasiyo na ncha,na sasa angalau mwanga unaweza kuaza kuonekana kwa mbaliiiiiiii.

Sawa kaka lakini swala la msingi ni uelewa tu hapa, hapo ndipo tunapoanguka watz wengi, watu hawafuatilii habari wanaishi kama kuku, ni juu yangu mimi na wewe na wengine wanaoweza kuingia kwa mwanakijiji kuwaelimisha wengine wahamasike wasizarau kura yao hata kama ni moja tu waweze ona thamani ya uamuzi wao.

Kumbuka tukiamua tutashinda, hakuna lisilowezekana. Mbona marekani na ubaguzi wao wamechagua raisi mwafrica?tushindwe kuwang'oa ccm kwani wao wana nini??
Hebu watumie jumbe mbalimbali watu uliosoma nao sekondari,chuo unaofanyanao kazi na rafiki wengine.

Mafisadi watashindana lakini hawatashinda

flein
05-07-2009, 07:16 PM
Mimi naungana nanyi wakuu hapa but mimi nasisitiza tu kuwa Watanzania sasa tuseme NO kwa ufisadi. Tuseme No kwa viongozi wanaochaguliwa kwa kulipana fadhila, tuseme NO kwasababu sasa inatosha, it is too much! Things must change, iwe ni kwa njia yoyote, lakini jambo la msingi Wananchi ni lazima tubadilike tuache kupiga kura kwa kupewa T-Shirts na Khanga, maana ni kwa kutojua nani ni kiongozi anayefaa ndipo tunakimbilia kuwapigia kura mafisadi nao wanaendelea kutunyonya, kutuibia na kutukandamiza. NO it is enough sasa.

Sawa ndugu nimefurahi kukerwa kwako, lakini tuwe more practicle rather than political. Tuanze kusema tunafanyaje kusema NO kwa mafisadi?? kila mmoja wetu awe ana sema kitu kulingana na ufahamu na uzoefu wake

mwanakijiji
05-08-2009, 12:45 AM
Leo hii kama vile Watanzania tuna usahaulifu wa kudumu Peter Noni (mshirika wa Rostam kwenye Vodacom) na kigogo wa EPA anasimama leo kuwa shahidi dhidi ya watumishi waliokuwa chini yake mahakamani! Huku akiendelea na utumishi Benki Kuu.!!!

Atubonekisye Massapa
05-08-2009, 12:52 PM
TUSICHOKE. hII VITA NI NGUMU. hATA JAMBAZI AKIVAMIWA HUPIGANAn ili asiuawe. Kwa maana nyingine ni kwamba jambazi hapendi kufa, tena akiambiwa huona ni haki yake kuiba. Kuna wakati mtu mwizi anasema anaiba kwa sababu hata hao anaowaibia waliiba mahali. Hii ndiyo humfganya impe uhalali wa kufanya uhalifu. Kikubwa hapa ni kwamba, hawa CCM wanaona ni halaili "kujilipa". Kama alivyosema Flein haopo juu, CCM wote ni waovu , ila makucha yao yalifupishwa na Nyerere. Mwinyi angeuza nci, bahati yake Nyerere alikuwa hai, hivyo aliweza kumkemea kila alipokosea. Hata Mkapa wakati wa Nyerere aliweza kudhibitiwa. Lakini, alipokufa Nyerere tu mwaka 1999, ndipo walipofungua vinywa vyao kama vile watu waliotoka Jangwani na kiu. Ndipo tukaona akina Mr. Clean wakibadilika na kuwa mbwa mwitu. Tukaona sura halisi za akina Kingunge. Tumewaona akina Makamba, na akina Lowasa. Miaka mitano tu , imetosha kutuonyesha jinsi tulivyo na hulka ya unyama. Sasa, tuna furahi kwa sababu , mwanzo wa kupiga uovu, NI KUUJUA UOVU uko wapi. Tumeuona. Na tupambane sasa, tusije tukwa kama wa Kenya ambao huchagua mtu kwa vile tu ni kabila lao, bila kujua kwamba hata nchi ingekuwa na kabila moja, bado kungekuwa na tofauti. Sasa hawana ardhi. Na ndicho kinachokuja TZ. Zawadi zinatolewa kwenye mbuga za wanyama, na kwenye ardhi. Tumekaa kimya. Tunachojua ni EPA tu. Jamai tupambane, hali si nzuri. Kwa walio Arusha wanayajua haya.

mwanakijiji
05-08-2009, 08:16 PM
Nadhanni ukiangalia vizuri utaona kuwa tunachojaribu kufanya ni kujaribu kumnyang'anya simba ndama wetu.. sasa simba hatumuachia kwa urahisi na ni sawa na kumnyang'anya mbwa chakula kisicho chake kwa vyovyote ataunguruma kututisha.. ninatarajia hawa jamaa kuja na mashambulizi makubwa zaidi kama ya kulipiza kisasi..