View Full Version : TLP Kunani?
mwanakijiji
03-31-2009, 04:36 PM
Jamani TLP ya Mrema inakaribia uchaguzi wake mkuu na kwa mara nyingine kuna mizengwe kama nini. Kuna matatizo gani? Hivi vyama hivi haviwezi kufanya uchaguzi bila rabsha na mizengwe.
dickabudi
03-31-2009, 04:50 PM
Mwanakijiji niliyazungumza kwenye thread yangu ikakosa majibu, naomba kama unaweza ile picha ilionyeshwa na ITV, muombaji mwingine anataka kurudisha fomu anakataliwa na Mwenyekiti wa sasa anacheza rhumba kufurahia mwanachama mwingine asirudishe fomu inatoa taswira gani??? kama unaweza tuwekee kwenye mtandao kituko hicho
mwanakijiji
03-31-2009, 05:00 PM

yeah nimeiona kule ulikoileta ngoja nijaribu kuunganisha hapa maana sijui nini kinaendelea; labda tutamtafuta Mrema.
dickabudi
03-31-2009, 05:14 PM
Ningependa awaelezee watanzania kama kurudisha fomu za nafasi ya uenyekiti taifa wa TLP ni mbinde hivyo kweli atang'atuka kama walivyofanya kwa hiari, uelewa na kujua kwamba Tanzania ni ya watanzania kama alivyofanya Marehemu Baba wa Taifa, Mzee Edwin Mtei, Ndugu Msobi Mageni ambao hawa waliona mbele.
Pia wapo ambao taratibu za vyama vyao ziliwalazimu kung'atuka kama Komandoo Dr Salmin Amour?
TLP ina mkakati gani kuona kupinga na kupingwa ni suala la kawaida katika chaguzi mbalimbali na post zote ziwe na mfumo huo
mwanakijiji
04-01-2009, 04:53 PM
Sasa Mrema anawalaumu Chadema.. na huko mbeleni Chadema itamtafuta mtu mwingine wa kumlaumu, CCM inawalalamikia wapinzani n.k hivi kuna mtu atakubali kuwajibika kwa matendo yake mwenyewe?
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.