mwanakijiji
11-11-2008, 08:33 PM
Hati ya mashtaka ya Kubenea iko tayari, wasema wanasheria
Na Exuper Kachenje (Mwananchi)
HATI ya mashtaka dhidi ya Saed Kubenea na gazeti la MwanaHalisi ipo tayari na atafikishwa mahakamani siku yoyote wiki hii, Mwananchi limeelezwa.
Akizungumza na Mwananchi, mwanasheria wa kampuni ya uwakili ya Amicus, Abul Kitururu alisema: ?Hati ya mashtaka ipo tayari tumeshaiandaa, na siku yoyote ndani ya wiki hii tutamfikisha Kubenea mahakamani.? Alisema kwa sasa hati hiyo ipo Dodoma ili kutoa nafasi kwa wenyeviti waliokuwa wakihudhuria mkutano wa Halmashauri |Kuu ya CCM (NEC) kuisaini kabla ya kuirejesha jijini tayari kwa kufungua kesi hiyo.
?Unajua lazima hati hiyo isainiwe na wateja wangu, wenyeviti wote nane wa CCM mikoa ndipo tufungue kesi, siku yoyote kuanzia leo itarudishwa nasi tutaanzisha kesi,? alisema Kitururu. Alisema walimpa Kubenea siku saba kuanzia Oktoba 30, 2008, ili aombe radhi na kulipa fidia ya Sh500 milioni kwa kila mwenyekiti wa mkoa, jambo ambalo Kubenea na Mwanahalisi hawakutekeleza hadi jana.
Kampuni hiyo ya uwakili ndiyo iliyopewa jukumu na wenyeviti nane wa mikoa nane kumchukulia Kubenea hatua za kisheria kwa madai kuwa gazeti lake la MwanaHalisi, toleo la Oktoba 8, liliandika habari iliyowadhalilisha.
Katika maelezo yao wenyeviti hao walidai Kubenea kupitia gazeti hilo toleo namba 118, aliandika habari iliyokuwa na kichwa kilichosomeka ?Njama za kumg?oa Kikwete zafichuka? zikiwahusisha wenyeviti hao, jambo ambalo walisema si kweli.
Oktoba 30 mwaka huu wenyeviti hao wakiongozwa na John Guninita, ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoani Dar es Salaam, aliyefuatana na mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, wakiwa na wanasheria wao Amicus waliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza azma ya kumshitaki Kubenea na gazeti la MwanaHalisi.
Katika mkutano huo uliofanyika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam, wenyeviti hao walisema kuwa kuanzia tarehe hiyo wameamua kuzungumza suala hilo kisheria zaidi na kuwa wameanza rasmi mchakato wa kumfikisha Mhariri Kubenea kwenye vyombo vya sheria, wakiongeza kuwa suala hilo litakuwa chini kampuni ya Amicus Attorneys. Tayari Kubenea ameshaeleza kuwa hataomba radhi na kuwaambia wenyeviti hao akisema: "Tukutane mahakamani."
Wazo:
Hivi kuna ulazima gani kutuambia kuwa hati iko tayari? Kwanini wasiamue tu kufanya kama alivyofanya Mwendesha Mashtaka? Fungua kesi wakutane huko huko mahakamani.. M.M.