PDA

View Full Version : Zaidi ya kulalamika tunafanya nini?



mwanakijiji
04-01-2009, 09:37 PM
Nini kingine unaweza kufanya kuleta mabadiliko unayoyataka kwenye nchi yako? Ni kitu gani unaweza kufanya ukitumia uwezo wako (wa hali, mali, na vipaji) kuweza kushiriki katika mabadiliiko unayoyataka?

Je ni kwa muda gani utakaa pembeni na kuangalia wengine wanafanya kitu au kuombea wafanye kitu fulani ili uwe na hima ya kutoa maoni yako jinsi gani kitu hicho kingepaswa kufanywa? Je uko tayari kwenda mbele zaidi ya kulalamika na kuanza kuhamasika?

- Je waweza kujiunga na chama cha kisiasa ambacho unaamini kinawakilisha matamanio yako na njozi zako na hivyo uko tayari kukisaidia kujiandaa kwa ushindi?

- Je uko tayari kushirikiana na wenzako wenye mawazo sawa kuanzisha matawi/tawi la chama hicho cha siasa huko uliko (iwe nyumbani au ugenini).

- Je uko tayari kurudi/kuingia ndani ya CCM ukijua ya kuwa nafasi ya kweli ya mabadiliko bado iko ndani ya CCM na humo unaweza kuibadili CCM kutoka ndani kwani upinzani hauna nafasi?

- Je uko tayari kuunga mkono kwa fedha na vipaji vyako chama kile ambacho unaamini kinaweza kuwa katika mazingira ya kushinda uchaguzi?

- Ni kitu gani kinachoweza kukufanya uamini na hatimaye kujiunga na upinzani? Viongozi wabadilike, sera zao zibadilike? Ziwe vipi?

-Je uko tayari kuungana na Watanzania wenzako kuanzisha a "movement for change 2010) na siyo kuungana kwa porojo bali kuungana kwa mali, vitendea kazi, muda, vipaji na uwezo?

- Je uko tayari kutenga sehemu ya muda wako kushiriki kuanza kuleta mabadiliko kwa namna ambayo haitaacha utata wowote wa wapi unasimamia?

- Ni kwa kiasi gani na kwa namna gani uko tayari kupambana na ufisadi (na yale yote ufisadi huo unawakilisha) badala ya kubakia mlalamikaji na mkosoaji wa kitu ambacho tayari karibu wote tunajua ni tatizo?

- Je wewe ni mlalamikaji, mkosoaji, au mwanaharakati? Mlalamikaji na mkosoaji ni watu ambao wanatumia maneno tu kuonesha kuwa wanachukizwa au hawapendi kitu fulani, mwanaharakati (activist) anatenda kubadilisha kitu hicho asichokipenda. Wewe ni nani?

- Je kama hushiriki kubadilisha ubovu unaouona au kushiriki kujenga kitu kipya unachokitamani, kulalamika na kunung'unika kwako kuna maana gani zaidi ya kufurahisha genge, kuonesha umahiri wa maneno na kutambia ubingwa wa akili na kuonesha majivuno ya usomi (intellectual pomposity)?

Je vijana wetu under 18 wanahusishwa vipi katika mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea nchini. Je watoto wako, au wadogo zako wakianza kuonesha mwamko wa kisiasa unawaambia nini? Je mtu akianza kuwavuta kwenye siasa na kuwa washirika wa mabadiliko ya kitaifa, utafurahishwa, utaona fahari, au utakuwa wa kwanza kuwaambia "achaneni na siasa?"

Kwanini nauliza haya yote!? Kwa sababu as long as we continue talking, and debating, and exchanging ideas, and what have you.. we will continue to be irrelevant to the process of change we so much desire. Unless individuals will step up and participate fully (in tangible ways) most of us will remain pure critics of the change we don't want to effect.

I'm reminded of the Obama's company to the presidency of the United States. Most people who were fed up of GWB's regime did not sit and complain endlessly, hawakubakia kulalamika daima na kuonesha ni kwa jinsi gani hawapendi utawala wa Rais Bush au chama cha Republikani. They DID SOMETHING.

They got off their comfort zones, they registered to be part of "change" and they knew that together they "CAN". Nyumbani kwangu walikuwa watoto wawili (ambao hata kupiga kura hawajaanza) kumpigia kampeni Obama, na a week later mama yao naye akapitia. Sikuona hata mtu mmoja wa McCain licha ya mlango wangu kuwa na bonge la banner la "Country first!".

Ninachosema ni kidogo tu, if WE DON'T participate to bring the CHANGE we so desire and demand; we have NO RIGHT WHATSOEVER TO criticize those who do. SO, what DO WE DO?