PDA

View Full Version : Mafuriko kyela : Balaa au baraka?



Mponjoli
04-03-2009, 05:41 PM
Kyela, wilaya iliyoko kwenye bonde la ziwa Nyasa, hukumbwa na mafuriko kila wakati. Mafuriko haya ambayo huja taratibu hutokana na mvua nyingi zinazonyesha katika milima ya Livingstone, na Rungwe ,na milima ya Mlanje huko Malawi.Mvua hizi hugharikisha mito Mikuu minne ya wilaya ya Kyela: mto Kiwira, Songwe, Mbaka na Lufilyo.
Kila mafuriko haya yakitokea,huacha janga kubwa la makazi, njaa na milipuko ya magonjwa.
HOJA:.
Je Kuna mipango yoyote madhubuti ya kudhibiti mafuriko haya kwa kutunza hayo maji yanayozidi kwenye mabwawa na kuyatumia kwa kazi ya umwagiliaji maji wakati wa kiangazi?
Siyo siri kwamba Wilaya hii hukumbwa na njaa karibu kila msimu na ndio soko kuu ya mazao toka Mbeya, Rungwe ,Makete na Malawi. Kinachosikitisha ni kwamba kuna mito mikuu minne iliyo na umbali usiozidi km 20 kati ya kila mmoja. Sijui kama kuna mikakati yoyote ya kutumia utajiri huu kuondoa baa hili la njaa, na pia kudhibiti mafuriko ya kila mwaka.
Nadhani imefika wakati wanasiasa wetu watuonyeshe ni jinsi gani wanakerwa na hali hii na waonyeshe uthubutu wa kupambana na hali hizi.

Ach-F
04-03-2009, 10:30 PM
Hakuna anayekerwa, WTZ wameweka viongozi wanaowajali wageni, unakumbuka ahadi za Jakaya ...ajira kwa vijana n.k. Subiri tumbo lake lijae kwanza.

Mponjoli
04-06-2009, 11:55 AM
Ach-F,
Kwa JK ni mbali sana, je wabunge wetu, ma DC an wakurugenzi wana mikakati gani? Maana hii hali huwa inategemewa kila mwaka, na kwa kuwa bonde hili lina rutuba sana ,ni vigumu kuwahamisha watu kwenda sehemu za miinuko. Bado swali langu ni moja: Kuna mipango yoyote ya kuyavuna maji haya na kuyatunza kwa umwagiliaji? Pengine Waziri wa maji na umwagiliaji ,Prof. Mark Mwandosya analo jibu. Au Dk Harrison Mwakyembe analo jibu. Ningeomba ufafanuzi. Hali hii pia iko Rufiji. Sijaona mikakati yoyote ya kudhibiti hii hali.....Sana sana niliwahi kusikia "mwanye uchungu" mmoja akipendekeza kuleta watengeneza mvua wa Thailand kwenye eneo lenye mvua la Nyanda za juu kusini, na si Shinayanga kwenye ukame! Very funny

Matigari
04-07-2009, 06:41 PM
Mponjoli,

Nashukuru sana kwa kuleta hii mada. Kama kuna kitu kinachonikera ni jinsi ambavyo Kyela ( hasa vijijini ) ilivyotelekezwa. Ninazungumzia Kyela vijijini, watu wana shida ya chakula, huduma za afya, mapato yao ni madogo. etc. Kitu kinachoudhi zaidi ni kuwa wilaya ina good agricultural potential. Unaweza zalisha minazi, michikichi, korosho cocoa, na matunda ( mananasi, machingwa, maembe na mafenesi) hivi jamani hakuna mtu anayeona kama hapo tunaweza hata tukaanzisha manufacturing? Wenzetu wa dabaga wanasindika matunda, hivi tunashindwa kujifunza wanafanyaje? Mwe

Huduma ya elimu Kyela vijijini hairidhishi kabisa. Yaani kitu kinachonikatisha tamaa kuhusu Mwakyembe ni hicho haielekea kama analeta bacon nyumbani. Mwakyembe kama unasoma hii tafadhali wasaidie wanantebela kukiwa na mipango mizuri watajiendeleza tu, ni watu wanaochapa kazi.