View Full Version : Kwanini sisi ni maskini?
mwanakijiji
04-07-2009, 04:34 PM
Hili swali linanizungusha kichwa. Kuna mtu anaweza kuelelezea rationally kwanini Tanzania ni maskini?
We are in a vicious cycle of povert.Period
>watu(sina hakika kama ni idadi au productivity capability)- Wale wazaliwao katika familia zenye kipato kidogo wamekuwa ni vigumu kwao kupata elimu bora-->tabaka la wajinga.Pia access yao katika huduma za afya ni utata mtupu-->jamii yenye afya duni.Sasa ukijumlisha hayo mawili unaweza pata mwanga kidogo wa nivipi tupo hapa.Lakini nani wa kuhakikisha kuwa elimu bora na huduma za afya zinapatikana kwa wananchi??Ni wananchi wenyewe wakisaidiwa na viongozi(serikali)walioiweka madarakani.Sasa hapa nyumbani hali ipoje nalo linahitaji mjadala mreeefu na lishazungumzwa sana.
>Pia kuna hulka ya watu kutopenda kufanya kazi halazi zitakazowaletea kipato,badala yake wanatafuta short cuts au wakati mwingine hukaa tu vijiweni/vibarazani.Hawa hawazalishi kitu bali wana matumizi,hivyo kujenga tabaka tegemezi.
Steve Dii
04-09-2009, 05:18 PM
Key katika maendeleo ni:
Transparency,
Hardworking,
Innovation,
Responsibility.
Kuna ki-usemi kifuatacho kuashiria yote hayo juu: Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi.
Ukiondoa 'innovation' hapo juu... lolote lile kati ya hayo manne likitendeka kwa asilimia walau 80%, jamii itashika hatamu na kusonga mbele. Ukiongezea innovation na kuipatia kipa umbele pia, jamii hiyo itakuwa kioo cha taswira ya maendeleo.
Ach-F
04-11-2009, 12:59 AM
Hili swali linanizungusha kichwa. Kuna mtu anaweza kuelelezea rationally kwanini Tanzania ni maskini?
Tanzania sio masikini, tungekuwa masikini hakuna hata wageni wowote ambao wangependa kufika Tanzania wala viongozi wetu wasingewajali sana wageni kama wanavyofanya hivi sasa. Swala lingekuwa kwa nini IMF, WB na nchi za magharibi wanawalundikia mapesa viongozi wetu, au kwa nini wanatukopesha kila siku?
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.