PDA

View Full Version : Kipaumbele au ndiyo wizi wenyewe huu:?



mwanakijiji
04-07-2009, 07:45 PM
Kuna miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa/itatekelezwa na wizara mbalimbali na taasisi mbalimbali kwa mwaka huu wa fedha. Ukipata nafasi ya kupitia taarifa hiyo ya mipango mbalimbali ya serikali utaweza kuona jinsi gani wakubwa wa nchi yetu wanavyojua jinsi ya kugawa fedha kwa kutuata ?kipaumbele?. Utagundua mara moja kuwa tatizo la Tanzania siyo fedha! Kuna tatizo kubwa zaidi ambalo ni vigumu kuliondoa.

Mojawapo ni mradi wa ?Deepening Democracy in Tanzania Program?. Mradi huu umetengewa fedha nyingi katika sehemu tatu:

Fedha zilizotengwa kwa ajili ya mradi huu (unatakiwa kutekelezwa mwaka huu wa 2008/2009) ziko hivi:

Msajili wa Vyama vya Siasa: zimetengwa kiasi cha Tsh 178,954,200
Mfuko wa Bunge: 355,232,900
Tume ya Uchaguzi: 596,362,400

Unaweza kusoma ripoti zote hizo kwenye ?vielelezo? upande wa Forum juu kulia au hapa kama attachments: