mwanakijiji
04-09-2009, 04:40 PM
Vitu unavyohitaji:
- Nyama ya ng'ombe, mbuzi, au kondoo iliyokatwa vipande vipande
- Mafuta ya zeituni (vijiko kama vitatu hivi vya mezani)
- Vitunguu (Kitunguu kimoja kikubwa kitatosha)
- Viungo mbalimbali kwa kadiri ya ladha yako
- Nyanya zilizokatwakatwa
- Njegere na karoti za vipande vipande
- Paprika na ukipenda binzari ya njano
- Munyu
Mapishi:
Njia ya Haraka (kwa mtu single)
- Tengeneza kama mchanyato. Weka vitu vyote hivyo kwenye kikaangio kikubwa; kwanza nyama, na viungo vingine isipokuwa nyegere na karoti). Viweke motoni kwa muda ukigeuza geuza hadi nyama igeuke rangi na kuwa kahawia. Kisha ongeza njegere na karoti na funika kwa muda; ongeza munyu kwa kadiri unavyohitaji. Kama ni mpenzi wa limau unaweza kuminyia upande mmoja wa limau. Enjoy!
Njia ya Taratibu kuvuta ladha yote.
- Kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka rangi na kuungua kidogo
- Weka nyanya na uzikaange na vitunguu (wengine wanapenda kukaanga nyama pembeni na kuvileta pamoja wakati huu)
- Weka nyama na kaanga pamoja na vitunguu na nyanya hadi nyama zigeuke rangi na kuwa kahawia
- Nyunyiza viungo mbalimbali
- Weka njegere na karoti na munyu kidogo
- Acha vichemke kwa muda
- koroga na ipua
Enjoy kwa wali wa nazi!