PDA

View Full Version : Jakaya Kikwete ameshindwa kuongoza



Ach-F
04-13-2009, 09:10 PM
Jakaya Kikwete uongozi umemshinda, hivi sasa Kenya na Uganda wana-team up kutaka kuhalalisha mikataba haramu ili waweze kuingia Tanzania na kufanya wanalotaka. Je, kama ziwa Victoria litakuwa halina mipaka wavuvi wa Tanzania wataweza kuendelea kupata ajira wanazozipata?

Jakaya alipoingia madarakani alisema ajira kwa wazawa, Je ametimiza hiyo ahadi? Ni ajira ngapi anaweza kuonyesha kwamba ame-create tangu aingie madarakani?

Ufisadi unaoendelea hadi leo kutoka kwenye mbuga za wanyama hadi kwenye madini ni Watanzania wangapi wanalipwa kihalali kutokana na kazi wanazozifanya? Au ndio wageni wanarundikiwa mali kama vile ni ya mjomba wao. Je, sakata la DECI ambalo inasemekana kwamba lina mtaji mkubwa hata kupita baadhi ya banking sector - benki kuu inaweza kweli kuhimili usimamizi wa pesa za walipa kodi? Je huo mtaji upo kwa Tanzanian shillings au dollars? Wanaweka wapi pesa zao?

Tunafahamu vyama vya upinzani hawawezi kusema lolote lile kwa sababu pesa za ruzuku zimewafanya wawe wehu wasiojali tena maslahi ya walipa kodi, Jakaya aliahidi kumaliza matatizo ya muungano lakini baada ya kujaza mifuko ya CUF na vyama vya upinzani kuneemesha matumbo yao anaonekana kutokujua anaelekea wapi kwani Wazanzibar hata uwalishe vipi hawashibi, Je ni hatua gani anazichukua kuona kwamba hatuingia katika matatizo mengine ambayo ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi? Je, ni lini ataanza kufanya kazi aliyoomba na kuanza kuonyesha kwamba kweli tuna serikali inayofanya kazi na sio porojo na longo longo?

Dua
04-13-2009, 09:43 PM
http://img230.imageshack.us/img230/7914/dsc08041.jpg






http://img230.imageshack.us/img230/4183/dsc08042.jpg

Jobs promised by JK.

mwanakijiji
04-14-2009, 10:52 PM
Sasa wenzako mbona wanasema amefanya kazi nzuri kweli na wanampiga mkwara mtu yeyote anayetaka kuonesha nia ya kutaka kugombea dhidi yake kupitia CCM 2010? Kuna watu ambao wanaapa kuwa Kikwete anafanya kweli! Utawaambia vipi uongozi umemshinda?

Kuhusu ajira, sidhani kama alibanwa wakati wa kampeni kuelezea ni ajira za namna gani alizoahidi kwani kusema kuwa ajira zitakuwepo milioni tatu anaweza kua alimaanisha hizo za kwenye picha!