PDA

View Full Version : Toleo la 35: 2010 Ni mabadiliko tu! & Breaking News



mwanakijiji
04-15-2009, 05:54 PM
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/toleola35_phixr.jpg

Salaam

Kuna habari mbili kubwa ambazo zimeanza kusikika sahihi:

a. Wakuu wa Mikoa wapanguliwa na kubadilishana vituo mbalimbali, hii inaonesha kugusa mikoa ya Tanga, Dar, Iringa, Kilimanjaro, Dodoma n.k Kimsingi siyo habari kubwa inayostahili kwani kilichofanyika ni kubadilishana ofisi tu. Aliyeshindwa eneo moja kumpeleka jingine hakuondoi tatizo ambalo ni yeye! Baadhi ya mabadiliko hayo:

Dr. Ishengoma toka Pwani kwenda Ruvuma
Bi. Hajjat Amina Said toka Iringa kwenda Pwani
Bw. Abdulazziz toka Tanga kwenda Iringa
Bi. Monica Mbega toka Ruvuma kwenda Kilimanjaro (huyu ni yule Mkuu wa Mkoa wa "Kamtumbwi ka Kikwete")
tunaendelea kufuatilia kujua wa Kilimanjaro ameenda wapi na kama Mbeya wamebadilishiwa (maana na siasa zao huko ni vurugu kuwa na Mkuu wa Mkoa ambaye ni mwenyeji wa huko!)

b. Kuna habari kuwa ofisi za DECI zimefungwa au DECI yenyewe imesimamishwa. Utaona katika toleo letu la leo tulitoa wito huo kwani kuiacha kuendelea kufanya kazi katika mazingira ya sasa ni kulea uovu. Kwa hiyo tunasubiri tuone mwitikio utakuwaje kwani tangu makala zetu mbili (iliyotoka kwenye Cheche wiki iliyopita) na iliyotoka leo kwenye Mwanahalisi kuna watu wamechukizwa na wengine wameapa kufanya vitu vibaya endapo DECI itafungwa. Tunatumaini vikosi vyetu vya usalama viko tayari kusimamia haki.

Na hii ni habari ndogo
c. Kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya Ziwa, wiki hii wataanza kuona gazeti jipya la habari na maoni na tunarajia kuwa na makala za Mwanakijiji humo pia. Kaeni chonjo.

Basi na sisi na twende na tuwe "Cheche"!

QUTE
04-15-2009, 09:17 PM
Serikali yetu haina utaratibu wa kuwasaidia wananchi wake hilo kila Mtanzania analijua vizuri sana, na hili la DECI mpaka kuongelewa na waziri mkuu ni kwa sababu kina Mwanakijiji na magazeti mengine yamelipigia kelele sana. Kinachonisikitisha ni kuwa mpaka sasa waziri mkuu anaposema DECI bank wana billion moja na walikusanya kwa wanachama billion kumi na tatu ni kwamba watu wameshapoteza hela kusema kwamba waendelee kuiacha kwani hawawezi kuifunga ghafla ni kuendelea kuleta risk zaidi kwani wananchi wanaendelea kupanda mbegu.
Mwanakijiji Serikali yetu haiwezi kuwalipa watakaopoteza pesa zao itawaruka futi sitini japokuwa uzembe ni wao na watendaji wao ambao kazi yao ni kutoa leseni bila kukagua biashara inayoombewa leseni.

Ach-F
04-15-2009, 10:42 PM
Ngoja tusubiri tuone. Waliochaguliwa kuongoza wameshindwa wanasubiri hadi sisi kwenye mtandao tuseme. Je malengo yao ya kutaka uongozi kwa kila mbinu ni nini? Ilikuwaje DECI wasajiliwe? nani waliwapa kibali kwa muda wote huo na Serikali ilikuwa inafanya nini wakati madudu kama haya yanaendelea. Nani hasa king pin? Je viongozi wa usalama watawajibika? Waziri n.k.

mkandamizaji
04-16-2009, 12:42 AM
jambo hili lahitaji usara ya hali ya juu katika kulishughulikia. pande zote za shilingi zina makosa - DECI wenyewe na mamlaka simamizi (serikali). Majibu na hatua zozote zitakazochukuliwa ziwajibishe wote wanaohusika kutoka pande zote. lakini kwa tunavyoijua serikali yetu wataruka mbali na hakuna mtu atakayeguswa serikalini, sanasana watahamishwa vituo vvya kazi tu!