PDA

View Full Version : Nawauliza wachumi!...



mwanakijiji
11-11-2008, 11:42 PM
Nilipojifunza Uchumi 101 kuna kitu tuliambiwa kuhusu majukumu ya benki kuu na hasa pande mbili za Fiscal Policy na Monetary Policy (sijui kwa Kiswahili ni madudu gani). Kwenye suala la monetary Policy tukajifunza mambo mengi lakini jambo ambalo bado najaribu kulielewa ni suala zima la mzunguko wa fedha na kwa jinsi gani kiasi cha fedha kinachozunguka katika matumizi kinachangia katika mfumuko wa bei ya vitu (inflation).

Hivyo tukaambiwa kuwa jukumu la Benki Kuu mojawapo ni kuhakikisha kiasi cha fedha kinachozunguka kinaendana na mahitaji halisi na shughuli za kiuchumi za ndani ya hiyo nchi. Na ya kwamba kuna wakati Benki Kuu inalazimika kuongeza kiasi cha fedha nyingi sana lakini kutokana na shughuli zakiuchumi zinazoendelea basi huwezi kuona mfumuko mkubwa wa fedha na wakati mwingine pia inaweza kuziondoa fedha kwenye mzunguko huo.

Sasa najiuliza maswali machache:

a. Kwanini serikali ya Marekani ilipoamua kutoa kile kinachoitwa kama "Stimulus Package" ya karibu dola mia tano kwa kila mlipa kodi (wengine walipokea 1200) haikuongeza mfumuko wa bei kwani ilikuwa ni kuongeza fedha kwenye mzunguko?

b. Kwa taifa kama la Tanzania ambapo kuna shughuli nyingi za kiuchumi yawezekana kwa serikali kuamua kutoa kiasi cha fedha kama "stimulus package" zikilenga biashara ndongondogo zenye kutoa ajira ya watu wawili au zaidi na wasiozidi 20 kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wake?

c. Ni kwa kiasi gani vitu kama hivi vya kumwaga mapesa kwenye uchumi toka serikalini vinaathiri kwa uzuri au ubaya shughuli za kiuchumi na kama kweli ni suluhisho zuri katika uzalishaji mali wa bidhaa na huduma?

Naomba shule..

Kepa
11-12-2008, 01:24 PM
Naona wachumi wanakuna vichwa kwanza ili waje na majibu ya uhakika ndio raha ya kuwa na mazunguzo ya pamoja na watu wa fani mbalimbali. Wachumi kila la heri kwenye hayo maandalizi.

mwanakijiji
11-12-2008, 04:59 PM
Na miye nasubiri kwa hamu maana tunaweza kupiga porojo ya hali ya uchumi lakini tukiweza kuelewa nini kinaendelea basi ni rahisi kweli kuchangia.

kurutamatata
11-21-2008, 01:54 PM
Katika suala kama hili mara nyingi huwa naogopa kulijibu au kulitolea ufafanuzi bila ya kuwa na kinga ya takwimu(statistical data base to substantiate the truth).Swali lako MM ni simple yet very complex!Simple kwa maana ya kwamba economic theory is so rich to be able to explain what would happen to any one dependent economic variable if several independent economic variables were to change! Na ni Complex in a sense kwamba Mfumo wa uchumi wa Marekanini so complex and so advanced kwamba jinsi unavyojiendesha ni tofauti kabisa na jinsi uchumi wetu wa Tanzania unavyo jikongoja.

Wenzetu wana "Kioo" cha kuangalia kila siku uchumi wao ukoje,unafanyaje,unaelekea wapi,nini tatizo,tatizo liko wapi,na hatua zipi muafaka zichukuliwe haraka na mara moja na hatua zipi zichukuliwe katika masafa ya muda mrefu.Kioo hicho ni Soko Lao La Hisa.Kwa mfano DOW JONES INDUSTRIAL ni soko la hisa lililo anza kufanya kazi kuanzia mwaka 1928!Just Imagine!The Dow Jones Industrial Average is a price - weighted average of 30 Blue - Chip Stocks that are generally the Leaders in their Industry.

It has been a widely followed indicator of the stock market since October 1st, 1928! Makampuni mengi makubwa yamo humo kama vile Walt Disney Co.,Wal - Mart Stores,Micro Soft Corp.,CocaCola Co.,Caterpillar Inc.,Bank of America,Citi Group Inc.,Boeing Co.,General Electric,IBM,General Motors na mengine kadhaa.NIKKEI 225 ya Japan inayosimamia mielekeo ya Makampuni Makubwa 225 ya Kijapani nayo inasemekana ilianza shughuli zake kunako May 16th.,1949!Nyingine kubwa zilianza kazi zake katika miaka ya 1941 -43!

Unaweza kuona wenzetu wametoka mbali na wamejifunza mengi sana katika kuendesha na kuongoza nguzo muhimu za uchumi kwa njia za kisasa kabisa tofauti na huku kwetu.Kwa kifupi tu,ni kwamba,ukianzia na classic definition ya Inflation,kwamba Its Too Much Money Chasing Too Few Goods!Pesa zikizidi mno katika mzunguko basi utarajie kupanda kwa kasi katika bei za bidhaa mbalimbali ambazo zitachukuliwa kuwa adimu kulliko uwezo mkubwa wa watu kifedha bila ya kuongezeka kwa uzalishaji mali.Kwa Marekani hilo ni tofauti kwasababu ya Nguvu na Uimara wa uchumi wao.

Uzalishaji wao ulizidi mahitaji yao nyumbani kwa makusudi kabisa ya kuweza kuziuza bidhaa zao nje ya mipaka yao katika soko la kimataifa.Tatizo kwao halkuwa uhaba wa bidhaa au upatikanaji wa mahitaji muhimu. Kwao tatizo kubwa lilikuwa ni Kipato kisicho tosheleza ongezeko la mahitaji ya kila Mmarekani.Kwa maana hiyo, bado lilikuwepo pengo la kutumbukiza zaidi Pesa Mpya katika mzunguko bila ya kuathiri mfumuko wa bei za vitu na huduma.Lakini vilevile,licha ya ongezeko hilo la Pesa katika mzunguko bado bidhaa za vitu mbalimbali zilishushwa na wauzaji.

Huku kwetu bei za bidhaa lazima zingeongezeka.Licha ya bei za bidhaa kushuka nchini Marekani lakini bado watu hawakuzipapatikia bidhaa hizo kwa kuzinunua kwa wingi ambavyo ilitarajiwa kwasababu watu walipata nyongeza hiyo ya Pato.Watu hawakujitokeza kwa wingi kufanya manunuzi zaidi baada ya bei za bidhaa nyingi kupungua kwasababu kubwa moja kwamba kila Mtu alikuwa katika hali ya tahadhari iwapo angekumbwa na Punguzo la Wafanyakazi linaloendelea hivi sasa katika Makampuni mengi nchini Marekani.

Kwa hiyo ni tatizo kubwa kwa kweli kuweza kulielezea kwa ufasaha katika nafasi hii.Kwa hapa kwetu Tanzania hali kama hiyo ingetokea,kwa serikali yetu kutoa Stimulus Package kama hiyo ungetarajia kuona mara moja kupanda kwa bei za vitu na gharama ya maisha kwa ujumla.Na pengine hata ubadhirifu katika matumizi ya pesa hizo katika Makampuni yaliyopata msaada huo.Na pengine hata zoezi zima la Stimulus Package lisingeleta manufaa yaliyokusudiwa kwasababu Viwanda vyetu havifanyi kazi ya uzalishaji kwa Malengo ya Pamoja Kitaifa na hayana mahusiano ya ndani kwa ndani katika kupeana malighafi na matumizi ya pamoja katika teknolojia na nishati(absence of forward and backward industrial inter - linkages and economies of scale)!

Hapa Tanzania itatuchukua pengine miaka mingine 50 ijayo angalau kuweza kutengeneza mkeka wa kiuchumi na soko la hisa na mitaji lililo sahihi(the foundations of the economy to be on track) ndipo safari yenyewe ianze kuelekea huko tulikokukusudia(pre conditions for economic take off to sustainability).This is not being too pessimistic!It is about being fairly Realistic.Hapa kwetu Tanzania bado Serikali ina jukumu kubwa sana la kusaidia na kuongoza mageuzi sahihi ya kiuchumi na siyo kujitoa kwa kisingizio cha kujenga mazingira muafaka ya uwekezaji!Mara nyingi serikali yenyewe ndiyo iliyo onekana kuwa Mchafuzi Mkubwa wa Mazingira hayo muafaka ya uwekezaji kutokana na A Very Poor Fiscal Policy!

Kama nilivyosema swali lako MM siyo rahisi sana kulijibu katika mkupuo mmoja.Its a Complex of Sophisticated Economic Wrangles and Issues!Just where would you start is the mother of all Questions in this particular scenario!Sijui kama nimejibu hata Robo ya Swali Lako.Not Sure!

mwanakijiji
11-21-2008, 04:35 PM
Asante sana.. naamini umejibu kwa kiasi kikubwa sana na umenipa mwanga ambao ni "tofauti" ya jinsi chumi za nchi kama Marekani na ya kwetu katika uendeshaji na upimaji wa Uchumi wao.

John lihawa
05-13-2010, 12:37 AM
Sina cha kuongeza...jamaa(kurutamatata) amemaliza kilakitu..aisee ni shule nzuri hasa kwa up caming economist,ina2tengenezea uwezo wa kucompare chumi za nchizinazoendelea na zilizoendelea.. . . .

John lihawa
05-13-2010, 01:10 AM
Sina cha kuongeza...jamaa(kurutamatata) amemaliza kilakitu..aisee ni shule nzuri hasa kwa up caming economist,ina2tengenezea uwezo wa kucompare chumi za nchizinazoendelea na zilizoendelea.. . . .