mwanakijiji
04-15-2009, 08:21 PM
Wanaotaka Kikwete agombee 2010, wanaogopa nini? (MwanaHalisi Aprili 15, 2009)
http://www.mwanakijiji.com/images/stories/habari/other/kikwetekampeni.jpg
Kuna kundi la watu waoga wanajitokeza ndani ya CCM. Kundi la watu wasiojiamini na wasioamini kuwa Rais Kikwete anaweza kuchagulika tena 2010. Kundi hili lina hofu kuwa Rais Kikwete anaweza kuamua kutokugombea tena 2010 na hivyo kubadilisha kabisa mwelekeo wa kisiasa katika chama hicho na bila ya shaka nchi nzima. Kundi hili limeanza kuonesha dalili ya kutetemeka na kama wapambe wanaoogopa kupoteza ujiko wao limeanza kujitokeza na kuimba wimbo wa ?Kikwete mgombea tena 2010 ndani ya CCM?.
Ninajiuliza hawa ndugu zetu wanaogopa nini? Ni kitu gani kinawatia hofu hivi kiasi kwamba mapema mwaka huu (miezi mingi tu kabla ya uchaguzi) wameanza kutishwa na sasa wameamua kujionesha wazi kuwa chaguo lao ni Kikwete? Je kwa kujitokeza kwao kusema ?chaguo lao ni Kikwete? kunamsaidia Kikwete au kunaonesha udhaifu wake uliopo kuelekea 2010?
Kinachonishangaza ni kuwa hawa ndugu zetu wanaonekana wanatambua kitu ambacho wengine hatukitambui; yaani, ndani ya CCM kuna mtu zaidi ya Kikwete ambaye anatamani kugombea Urais mwakani. Mtu huyo nina uhakika si Shibuda kwani Shibuda alifanya hivyo hata mwaka 2005 na sidhani kama anawatisha hivyo. Kitendo cha mtu aliyekuwa Waziri Mkuu, kitendo cha mtu aliyewahi kuwa Spika na jumuiya mbalimbali za CCM mikoani kuanza kujitokeza na kusema Kikwete ndiye atakuwa mgombea wao kunatudokeza jambo moja kuwa kuna mtu mwingine ndani ya CCM anataka kuwania nafasi hiyo ya Urais.
Mtu huyo ni nani? Sitaki hata kumdhania ni nani lakini kama yupo mtu huyo ana nguvu na ujiko wa kiasi gani hadi kuwafanya watu wazima na akili zao kutetemeka katika majumba yao, kusababisha wakongwe ambao majina yao tulishayasahau kutoka katika maficho yao? Mtu huyo ana ubavu gani wa kushindana na mtu aliyeshinda nafasi ya Urais kwa asilimia 80 ya wapiga kura?
Kama kuna mtu huyo ndani ya CCM basi ina maana ya kuwa mwaka 2005 Watanzania walifanya makosa kumchagua Kikwete. Kwa sababu kama kuna mtu ambaye anaweza kumshinda Kikwete leo hii ina maana mtu huyo tulikuwa naye 2005 na hatukumpa nafasi!
Tulifanya makosa?
Jinsi ambavyo watetezi wa uteuzi wa Kikwete wanavyozungumza ni kana kwamba wako tayari kuendelea na makosa yale yale 2010 bila kuyasahihisha hata kama wakipewa nafasi hiyo. Waoga hawa wanaamini kuwa ni bora kuendelea na kosa lao kuliko kulisahihisha na hivyo wao hawajali jingine lolote isipokuwa hawako tayari kumuona mtu mwingine yoyote akigombea nafasi ya urais zaidi ya Kikwete.
Hapa hatuna budi kujiuliza kama kweli tulifanya makosa 2010 kwa kumchagua Kikwete kama Rais wetu? Hivi tulimchagua kwa sababu tuliona nini? Alikuwa na rekodi gani ya uongozi kumlinganisha na mgombea mwingine yoyote? Alikuwa na uwezo gani wa kiuongozi tukimpima na mtu mwingine? Yawezekana wengi waliopiga walipiga kura kwa sababu ya kuangalia ile sura ya ujana na tabasamu lake? Yawezekana wengine walipiga kura kwa sababu waliamini kuwa yeye kweli ni ?chaguo la Mungu??
Sasa kama wananchi leo wamegundua kuwa walifanya makosa na wanataka kuyasahihisha hawa waoga wa CCM wanataka kuwanyima wananchi nafasi ya kubadilisha uamuzi wao kwa njia ya kura? Kwa ubavu gani walionao?
Kikwete sasa anarekodi!
Mwaka 2005 Kikwete hakuwa na rekodi ya kuonesha uongozi wake na kama ingekuwa katika nchi nyingine kuna mambo ambayo angetakiwa kutolea maelezo ndio maana walimkwepesha kufanya midahalo na wagombea wengine ili watu wampime. Kulikuwa na masuala ya IPTL na tuhuma za kupokea fedha toka Iran na Oman. Bahati mbaya waandishi na wana CCM wengi walikuwa wamepigwa ganzi ya mapenzi kiasi kwamba hakuna aliyethubutu kumhoji maswali magumu na hivyo tukampitisha kwa kufaraha kwa kuangalia vile ambavyo si vya msingi.
Sasa hata hivyo ana rekodi ambayo yeye mwenyewe anaweza kuisimamia. Watetezi hawa wa Kikwete wanatuambia kuwa anaongoza mapambano ya ufisadi wakitolea mfano wa kesi uchwara zilizofikishwa mahakamani (ndiyo nimesema uchwara). Hawa wanataka tumaini kuwa watu kufikishwa mahakamani (tusiangalie mashtaka yenyewe ni yapi) basi mapambano dhidi ya ufisadi yanaendelea chini ya Kikwete.
Lakini rekodi yake sasa ni kubwa zaidi na ambayo mwana CCM yeyote anayo haki ya kuipa changamoto, kuihoji na kumpa nafasi Rais Kikwete kuitetea. Je Rais Kikwete anahusika vipi katika kuwaleta Dowans? Je alihusika vipi katika suala la Richmond pale ambapo baadhi ya watumishi walipotaka mkataba huo usitishwe? Je Rais Kikwete alihusika vipi na kuwaacha watoto wa Kitanzania wasote ugenini na kupigwa baridi kwa kitu kimoja cha kuomba elimu na kuwalazimisha kuwarudisha kwa aibu na kwa nguvu Tanzania toka Ukraine? Kwanini hadi leo serikali yake haijaomba radhi kwa hilo?
Rekodi yake ipo na ninaamini hawa waoga walioibuka siku hizi wanajua hawezi kuitetea! Lakini uzuri ni kuwa kwa kumpambanisha na MwanaCCM mwingine basi tunampa nafasi Rais wetu kuona makosa yake, kukiri makosa ya wazi lakini pia tunampa nafasi ya kujipanga upya. Kumnyima nafasi hiyo ni kuendeleza utamaduni wa woga na sera za unafiki.
CCM siyo Rais!
Mojawapo ya utamaduni mbovu ambao ndugu zetu watetezi wa Kikwete wanataka uendelezwe ni ule wa ?kumwachia Rais aliyeko madarakani mihula yake miwili?. Dhana hii ni potofu, ya kibabe na aina mfanano wowote na utawala wa demokrasia. Kama hili lingekuwa zuri wao CCM si ndiyo wana Bunge na wana Rais kwanini wasiamua kubadilisha Katiba na kuweka awamu ya Rais kuwa ni muhula mmoja wa miaka kumi! Maana kama tayari wanataka Kikwete awe mgombea wao 2010 na mtu mwingine yoyote CCM asigombee basi waamue tu kufanya uchaguzi wa wabunge na ule wa Urais uahirishwe hadi Kikwete atakapomaliza awamu yake 2015!
Vinginevyo, CCM hawaodhi nafasi ya Urais wa Tanzania na aliyeko madarakani hana ubia na nafasi hiyo. Nafasi hiyo Kikatiba inashindaniwa kila baada ya miaka 5 na hakuna garantii kuwa ukiwa Rais basi mhula wako wa pili utapewa kwa dezo. Kikwete ni lazima apambanishwe ndani ya CCM kama tulivyofanya 2005 na kabla yake, ni lazima arudishe fomu za kugombea pamoja na watu wengine wanaotaka kufanya hivyo, na ni lazima atetee nia yake hiyo kama alivyofanya 2005. Nje ya hapo, CCM itangaze kuwa Tanzania ni nchi ya Udikteta wa chama cha Mapinduzi!
Wanaotaka kugombea wasitishwe
Utawala wa Demokrasia unatutaka tutoe nafasi sawa kwa mtu yeyote anayetaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi. NI kwa sababu hiyo naamini mojawapo ya mambo ambayo yafanyike mwaka huu ni pamoja na Bunge hatimaye kubadilisha sheria ili kuruhusu mgombea binafsi wa nafasi yoyote ya uongozi. Haya mambo ya kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama usichokubaliana na nacho hayana msingi! Katika taifa la watu milioni 40 ninaamini kuna watu wa kutosha wenye akili timamu wanaoweza kufikiria jinsi gani ugombea binafsi unawezakufanyika bila kuweka mzigo mkubwa kwa mgombea yeyote kulinganisha na yule wa chama.
Hata hivyo ndani ya CCM kama kuna watu wanaamini wanaweza kuliongoza Taifa letu vizuri zaidi, kwa kuthubutu zaidi na kuliamsha kuelekea mafanikio na maendeleo ya kweli (ya watu siyo vitu) basi watu hawa wako huru kujitokeza bila kuona haya kama alivyofanya Shibuda. Watetezi wake hawana uhodhi wa CCM na wasitumie jina la CCM kuwatisha watu wengine ambao wako ndani ya Chama hicho.
Kama wao wanaogopa kuwa Kikwete asipochaguliwa tena 2010 basi utakuwa ni mwisho wao na madudu yao yatajulikana basi hayo ni matatizo yao. Ni wao waliokaa kimya bila kujitokeza wakati nchi yetu inapitia wizo mkubwa kabisa wa mabilioni ya fedha, lakini linapokuja suala la hamu zao wanajitokeza huku wakitingisha vidole vyao!
Mtanzania yoyote ndani ya CCM anayetaka kugombea nafasi ya Urais ni lazima apewe nafasi sawa.
Vinginevyo, kama waoga hawa wanajua kuwa Kikwete hawezi kushinda akipambanishwa na mtu mwingine CCM basi ushauri wangu ni kuwa wawatimue wale wote ambao wanaonesha nia ya kutaka kupambana na Kikwete! Wawatimue na kuwafukuza katika Taifa la Tanzania! Na wawanyang?anye na uraia kabisa ili wasirudi.
Wakishafanya hivyo, waamue kufuta sheria inayoruhusu vyama vingine ili tuwe na chama kimoja chenye mgombea mmoja tu wa CCM ili Taifa zime limpigie kura za Ndiyo au Hapana. Na kama akipata kura nyingi za Hapana, basi wamuapishe kuwa ni Rais kwani atakuwa bado amepata kura nyingi!
Vinginevyo, wamuache Rais Kikwete afanye kazi yake na akitaka kugombea mwakani agombee akiamua kupumzika apumzike na kuwapisha wengine. Alipotaka kugombea ilikuwa ni kwa miaka 5 na kama kwa sababu zake zozote akiamua kutokugombea basi asijisikie shinikizo la kugombea ili kuwaridhidha watu fulani ambao muda wao wa kisiasa umeshapita!
Lakini akitaka kugombea basi asitumie vyombo vya dola au hawa wapambe kutuma ujumbe wa vitisho kwa watu wanaompinga au ambao wanaamini wanaweza kufanya bora zaidi ndani ya CCM bali awe tayari kusimama na rekodi yake na hoja zake kugombea tena nafasi ya Urais.
Kwa kufanya hivyo Rais Kikwete atathibitisha kuwa yeye ni mwanademokrasia na ambaye hana hofu ya kushindana na mtu yeyote kwenye sanduku la kura. Iwe ni mwana CCM mwenzake au nje ya CCM. Lakini endapo Kamati Kuu au chombo kingine rasmi cha Chama kikitoka na kusema kuwa Mgombea wa CCM atakuwa ni Kikwete tu basi lile shimo la kifo cha demokrasia tuliongezee kina chake ili ndani yake wa kwanza kutumbukizwa atakuwa ni Chama cha Mapinduzi!
Vinginevyo, mwana CCM anayetaka kugombea na kushindana na Kikwete asiwaogope waoga hawa mambo leo na asione haya kuonesha nia yake hiyo na wala asionekane adui bali asimame kama mwanademokrasia na mwanamapinduzi wa kweli kugombea nafasi hiyo na kutoa changamoto hiyo kwa Kikwete. Yeyote ambaye hapendi akimbilie baharini ajitose!
Niandikie: mwanakijiji@mwanakijiji.com