mwanakijiji
04-16-2009, 08:48 PM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 16 Aprili 2009
SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA KWA PROF. LIPUMBA
Ripoti za vyombo za jana usiku na leo nzima zimearifu kutokea kwa ajali ya jahazi lililokuwa likisafiri kutoka Tanga kwenda Pemba hapo jana kushika moto. Kwa mujibu wa ripoti hizo, zaidi ya watu 20 wanahofiwa kwamba watakuwa wamepoteza maisha yao na wengine kadhaa ni majeruhi. Hao ni wale waliorikodiwa tu kwenye kumbukumbu za usafiri, kwa hivyo uwezekano ni kuwa maafa hayo yanaweza kuwa yameondoka na roho nyingi zaidi.
Kwa niaba ya Chama changu cha Wananchi (CUF) na mimi mwenyewe, natuma mkono wa rambirambi kwa ndugu na jamaa wote walioondokewa na watu wao katika msiba huu mkubwa. Mwenyezi Mungu awape subira wafiwa hao na awape nguvu za kupambana na wakati huu mgumu wa maombolezo. Vile vile Mwenyezi Mungu awapokee wenzetu hao waliotangulia mbele ya haki akiwa ameshawasamehe makosa yao. Tunatoa pole pia kwa majeruhi wote na tunawaombea wapone kwa haraka ili wajiunge na wenzao katika shughuli za ujenzi wa taifa letu.
Pamoja na salamu hizi za rambirambi, tunaamini ni wajibu wetu kuikumbusha Serikali yetu ambayo ina dhamana ya kulinda uhai wa raia na usalama wa mali zao, kwamba hali ya usafiri wa baharini baina ya Tanga na Pemba ni mbaya sana. Hii si mara ya kwanza kwwa majahazi yanayopakia mizigo na watu kupatwa na maafa yakiwa safarini ama kutokea Tanga kwenda Pemba au kutoka Pemba kwenda Tanga. Haya yamekuwa ni matukio yanayojirejearejea. Karibuni kila mwaka, roho za makumi ya Watanzania na mali zao humezwa na bahari na hivyo kuleta misiba na hasara zinazoendelea.
Kwa hivyo, umefika wakati wa Serikali yetu kuingilia kati na kuanzisha usafiri wa kudumu na uhakika baina ya Tanga na Pemba ili wananchi waondokane na usafiri usio na uhakika na unaohatarisha usalama wao na wa mali zao. Tukiwa chama cha kiliberali, bila ya shaka, hatukubaliani na Serikali kujiingiza yenyewe katika biashara hiyo ya usafiri, lakini tunaamini kwamba serikali ina wajibu wa kuweka misingi ya kuiendesha na kuisimamia vyema.
Kwa wananchi wote wanaotumia vyombo vya baharini baina ya Tanga na Pemba, tunawaomba wawe waangalifu sana wakati wa kutumia vyombo hivyo. Waepuke kila sababu inayoweza kuleta maafa, kama vile kujazana sana kwenye chombo kimoja. Kwa hakika, ingawa mwanaadamu hawezi kuepuka ahadi yake pindi siku ya kuondoka duniani ikifika, lakini anaweza kuepuka ajali inayochochewa na mkono wa mwanaadamu mwenzake.
Haki Sawa kwa Wote
Imetolewa na
Prof. Ibrahim Lipumba,
Mwenyekiti
The Civic United Front (CUF ? Chama cha Wananchi)