pangamawe
04-22-2009, 09:43 AM
Jana kama kawaida yake limeanza na mjadala wa kipuuzi ambao umetokana na swali la kipuuzi lililoulizwa na siraju kaboyonga ambaye dhamira inanizuia kumwita mheshimiwa mbunge wa Tabora. Katika swali lake ninaloliita la kipuuzi alitaka kujua serikali inachukua hatua gani kupambana na "wezi" wa nyaraka za serikali wakiwemo wabunge. Katika majibu yake ya kipuuzi vilevile hawa ghasia kasema hatua kali zitachukuliwa kwani wabunge hawana kinga dhidi ya nyaraka za siri za serikali.
Haya ni mambo ya ajabu sana viongozi wengi wa serikali wamejikita kwenye ufisadi huku watumishi wa ngazi za chini wakiteseka kwa mishahara isiyokidhi mahitaji halafu inategemea eti nyaraka za ufisadi huo zisiibiwe. Nilitegemea serikali itoe tamko kama hilo ili kutisha watu wasiibue nyaraka za ufisadi mwingi tarajiwa kwani tunajua CCM inatafuta pesa za kununulia shahada za kupigia kura katika uchaguzi mkuu mwakani hivyo kila aina ya ufisadi unafanyika kuelekea lengo hilo. Watu kama Kaboyonga ambao ni wengi sana miongoni mwa wabunge wa CCM wanachowaza ni nkujipendekeza ili wateuliwe kuwa mawaziri ungetegemea kaboyonga aonyeshe kukerwa na tabu za kimaisha za wapiga kura wake badala yake eti anakerwa nauvujaji wa nyaraka za serikali zinazohusu ufisadi.
Wabunge wengi wa CCM ni tatizo kubwa sana Dr Slaa kashambuliwa kwa vile kataja hadharani kipato cha wabunge, nampongeza sana dr slaa kwa hilo maana wengi wa wabunge wa CCM wako busy na kuji-identify na serikali ili wapewe uwaziri ndiyo maaana nadhani wakati umefika mawaziri wasitokane na wabunge ndipo watu wa aina ya kaboyonga ,nyalandu hawataingia bungeni.
Nwapa shime wazalendo wenzangu waendelee kufichua hila za ufisadi zinazoratibiwa na serikali kwaajili ya uchaguzi mwakani kwani hazina tija yoyote kwa watanzania bali kuwaimarisha madarakani watawala wetu mafisadi. Hivi sasa kuna ufisadi mkubwa sana unaandaliwa na serikali kwa lengo hilohilo la uchaguzi mwakani. Ni mradi wa kurusha live uhamaji wa nyumbu katika hifadhi ya serengeti, mradi huu wa kitapeli utakaogharimu mabilioni ya shilingi unaratibiwa na tapeli mmoja wa kitanzania aishiye nchini marekani aitwaye Dr Tenende ukiwa na baraka zote za ikulu. Huu mradi ni white elephant na unapingwa vikali na wataalamu wa uhifadhi lakini kwa vile lengo ni kukusanya pesa za uchaguzi wakubwa hawataki kusikia kitu. Nitaleta details na nyaraka za mradi huu wa kitapeli unaoitwa WILD BEASTS MIGRATION LIVE BROADCAST