View Full Version : JK kwenye zeutamu! - Mipaka imepitwa au ndio Uhuru?
mwanakijiji
04-22-2009, 07:28 PM
Kwenye tovuti ya Utamu kumewekwa picha ya kuunganisha ambapo kichwa cha Rais Kikwete kimewekwa kwa mwanamme ambaye anafanya ngono na mwanamme mwengine, JK anaoneshwa kuwa yuko kwenye receiving end. Nimepata email kadhaa za watu kuhoji inakuwaje kumdhalilisha Rais wetu na kuwa sasa zeutamu imevuka mipaka.
Kati ya hoja ambazo nimekuwa nikizisema ndio mambo haya; kwa kadiri tunaona nguruwe wakitendewa vitendo vya namna hii na kuandikwa katika kila aina uchafu katika kile tunachokiita ni "udaku" itakuwaje siku moja mwanadamu akigeuziwa kibano?
Zeutamu imevumiliwa ikiwadhalilisha watu wasiohusika na jambo lolote na watu wa maisha ya kawaida na hakuna mtu ambaye anaonekana kukerwa. Binafsi ninaamini zeutamu kama tovuti nyingine inayo haki ya kufichua ufisadi wa kila aina lakini inapofika mahali inavuka mipaka ya haki na uhuru wa mtu mwingine basi inajiweka kwenye matatizo.
Lakini kwenye hili la kutumia picha ya JK ni lazima tuoneshe kuwa si jambo sahihi na lina lengo la kumdhalilisha Rais. Kipimo hicho hata hivyo kwangu sikipimi kwa sababu ni Rais tu bali ni kwa sababu ni mtu mwingine. Lakini, tuonekane tunakerwa kwa sababu ni Rais kawekwa lakini wanapowekwa mabinti na vijana mbalimbali tusikerwe? Je hatukusema kuwa binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja!
Au ndiyo yale yale ya shamba la wanyama ambapo wanyama wote wana haki, lakini wapo wanyama wana haki zaidi kuliko wengine?
Nachochea mjadala!
Siafiki na sintokubali kuona mtu wa aina yeyeto yule akikejeliwa na kudahalilishwa kama vile ilivyotokea kwa wengi ndani ya tovuti ya ze utamu na hata vyombo vingine vya kupasahna habari kama magazeti ya udaku nk.
Hakuna sheria ndani ya nchi yeyote ambayo inaruhusu ama kushangilia udhalilishaji kama ambao umeonekana kwenye hii tovuti ya ze utamu
Tulidharau mwanzo na kuona kwamba labda hii ze utamu ni kitu cha kupita na itafikia mahala hata wanaoshabikia hiyo tovuti kutotembelea hapo. Si utamaduni wetu hata kidogo sisi watanzania kufikia pahala pa kuweka bayana na mambo ya ufedhuli kama ngono na hasa kuhusisha viongozi ama watu waliotuzidi umri na hasa inapokuwa mtu huyu ni “Public Figure”.. haijatokea hata mara moja na kulega kwetu kwenye mambo ya sheria katika uhuru wa habari na hakika kwenye uhuru wa habari kupitia teknologia ya kompyuta ya mtandao ndilo jambo ambalo limetufikisha hapa.
Labda itakuwa si rahisi kuwapata waharibifu hawa wa uchafuzi wa hali hewa kwenye mtandao lakini la muhimu sasa hivi ni kufunga mtandao huu usipatikane tena Tanzania (jambo ambalo linawezekana, maana zipo nchi kama uarabuni mitandao yote ya mambo ya ngono imefungwa kwa watu wote). Hili hatuwezi kushindwa na potelea mbali wengi waanze kulalamika na kulalama eti hakuna Demokrasia ya utumiaji na upataji habari kwenye mtandao. (China wapo waliyolalama na mambo bado yapo pale pale lakini hakuna kuingiza taarifa za kupotosha ama kudhalilisha).
Maana ya matumizi mazuri ya mtandao (Internet) ni kujua wapi pa kuenda na ni habari gani ama tovuti gani ni ya uhakika (Authoritative referenced Information) ambayo itasaidia kuelimisha na kujenga maudhui mema yanayokubalika na jamii inayohusika na siyo kwenda kiholela tuu!!!
Kuna mengi ya kuandika kuhusu swala hili, kabla haijawa mlolongo wa maelezo mimi binafis ninashauri kwamba ili kupambana na vita hii ya udhalilishaji kupitia kwenye mtandao, ni lazima sasa katika Tume ya Mawasiliano kuwepo na kitengo maalum ambacho kitakuwa kikishirikiana kwa karibu zaidi na makampuni yote nchini ambayo yanatoa huduma ya mtandao (ISP). Pili, idara ya upepelezi ya Polisi inabidi iwe na kitengo cha kushughulikia ugaidi wa mtandao wakishirikiana na kitengo maalum kutoka Idara ya Usalama wa Taifa.
Katiak utendaji wa siku zote lazima pawepo na Polisi kutoka idara ya ugaidi wa mtandao ambao ni wataalum wa mambo ya “Information Forensic” ambapo raia yeyote yule ambaye anaona hakutendewa haki kimtandao anaripoti kwao na wao wanafanya uchunguzi kisheria na kuwa na vithibitisho (digital) ambavyo vitakubaliwa mahakamani kama uthibitishio thabiti wa tuhuma mbele ya madai ya raia huyo.
Huu ni wakati sasa tunatakiwa kwamba kila mwananchi ana ufahamu mkubwa kwamba kuna kitengo cha Polisi ambacho kitashughulikia ugaidi wa mtandao na kwamba raia wana pahala pa kwenda kupata msaada wa kiutaalam ili sheria ichukue mkondo wake.
Nina fahamu kwamba kuna baadhi ya askari Polisi ambao wamehudhuria mafunzo na hata semina nyingi kuhusu swala hili, ila nina hakika bado hakuna “Information Forensic Laboratory” ambayo ingeanza kushughulikia mambo haya tangu wakati wa sakata la wanafunzi wa Saint Augustine na hao wengine wa IFM.
Elimu tunayo na Wataalam tunao na hata vitendea kazi vipo TUNANGOJA NINI kushughulika na hawa magaidi wa mtandao!!!? Hatuhitaji FBI wala CIA kwa hili sana tutahitaji uzoefu wao na taarifa nyingi ambazo wanazo zitusaidie kupambana na kuvifanya vitengo vyetu vya usalama kuwa na uwezo mkubwa zaidi katika mpambano huu. YOTE YANAWEZEKANA!!
Fingigwe
04-25-2009, 06:47 PM
Mkuu, pamoja na kero zetu zote jinsi mambo yanavyoenda nchini, hii kitu haikubaliki kabisa. IT IS REALLY IN HORRIBLE TASTE! Kwangu mimi ni vigumu sana kuamini kuwa hawa wanaotumia njia ya udhalilishaji wa aina hii kuelezea "hoja" zao dhidi ya utendaji au mwenendo wa mtu au watu SI wabwia unga.
Hao akina ze utamu, magazeti ya global publishers na wengineo waendelee kutoa hizo "burudani" zao kwa wenzetu wenye fikra duni; lakini hawastahili na wasipewe nafasi katika mijadala yetu muhimu hapa. Labda hili litakuwa fundisho kwa wazito Serikalini kuamka na kuanza kufanya kazi zao kwa mpangilio endelevu. Hii kuachia watu wanatumwagia vituko vya ajabu usoni kila siku hatma yake ndio hii - sasa wametinga Ikulu!
Mponjoli
04-28-2009, 12:26 PM
All animals are equal, but osme are more equal than others.
Nasema, nimekuwa nikikerwa sana na magazeti ya global publishers siku nyingi, lakini serikali haijali kabisa. Yale magazeti nicheap, wasichana huyanunua na kuyapeleka nyumbani ambako watoto nao huyasoma. Serikali imekaa kimya. Wanafurahi, wanaangalia watu wakichafuana majina. Mara Amina Chifupa, Mara Maimartha mara ...ili mradi uchafu mtupu. Hakuna anayejali. Kimya. Filamu zetu ni mbaya mno...ukiangalia filam za Nigeria , hata kama imekuwa na maudhui ya kikubwa (18 yrs) , bado hawaonyeshi mapenzi ya waziwazi kama Bongo . Watanzania wanaonyesha wazi, na filamu zetu za Kiswahili. Kwanza zinarushwa na vituo vya television muda ambao watu wengi wapo kazini. Watoto wanaziona. Serikali haijali.Kimya. Wanakurupuka Mwanahlisi likiandika habari, hilo linafungiwa. Lakini hao wa Global publisher " in God They Trust" wanaendelea tu , hakuna anyewauliza. Pengine kwa kuwa ni watu wao chini ya mwavuli wa ulokole.
Nimechukizwa sana na picha ile ya rais wetu, mono kiasi kwamba nilitamani kutapika. Lakini hayo ndiyo waliyoyataka. Waziri wa habari juzi tu katetea vitu hivyo bungeni " uhru wa habari'. Jamani tuwe na Controll. Kiswahili kimeenea sana, magazeti yetu yawe na kikomo! Natamani hata waziri wa habari , utawala bora nk. nao watolewe ili waamke na kuanza kufanya kazi. Japo inakera, lakini " binadamu wote ni sawa" . Amkeni , wekeni grades kwenye filamu zetu, siyo kila filamu inakuja na kuonyeshwa kwenye TV bila onyo lolote ya contents zake! Mwisho unakuta uko na mtoto, mtu anabakwa, mnabaki kugeza uso kwwa aibu, kumbe tungepata warning ya content, usingeruhusu mtoto kuwa naye pale kwenye Runinga. Raisi akemee mwenyewe , hao watu wake hawawezi kamwe, maana wanaposibility kubwa ya kupewa posho wanyamaze.
INAUDHI SANA...
Mponjoli
04-28-2009, 12:29 PM
All animals are equal, but osme are more equal than others.
Nasema, nimekuwa nikikerwa sana na magazeti ya global publishers siku nyingi, lakini serikali haijali kabisa. Yale magazeti nicheap, wasichana huyanunua na kuyapeleka nyumbani ambako watoto nao huyasoma. Serikali imekaa kimya. Wanafurahi, wanaangalia watu wakichafuana majina. Mara Amina Chifupa, Mara Maimartha mara ...ili mradi uchafu mtupu. Hakuna anayejali. Kimya. Filamu zetu ni mbaya mno...ukiangalia filam za Nigeria , hata kama imekuwa na maudhui ya kikubwa (18 yrs) , bado hawaonyeshi mapenzi ya waziwazi kama Bongo . Watanzania wanaonyesha wazi, na filamu zetu za Kiswahili. Kwanza zinarushwa na vituo vya television muda ambao watu wengi wapo kazini. Watoto wanaziona. Serikali haijali.Kimya. Wanakurupuka Mwanahlisi likiandika habari, hilo linafungiwa. Lakini hao wa Global publisher " in God They Trust" wanaendelea tu , hakuna anyewauliza. Pengine kwa kuwa ni watu wao chini ya mwavuli wa ulokole.
Nimechukizwa sana na picha ile ya rais wetu, mno kiasi kwamba nilitamani kutapika. Lakini hayo ndiyo waliyoyataka. Waziri wa habari juzi tu katetea vitu hivyo bungeni " uhru wa habari'. Jamani tuwe na Controll. Kiswahili kimeenea sana, magazeti yetu yawe na kikomo! Natamani hata waziri wa habari , utawala bora nk. nao watolewe ili waamke na kuanza kufanya kazi. Japo inakera, lakini " binadamu wote ni sawa" . Amkeni , wekeni grades kwenye filamu zetu, siyo kila filamu inakuja na kuonyeshwa kwenye TV bila onyo lolote ya contents zake! Mwisho unakuta uko na mtoto, mtu anabakwa, mnabaki kugeza uso kwwa aibu, kumbe tungepata warning ya content, usingeruhusu mtoto kuwa naye pale kwenye Runinga. Raisi akemee mwenyewe , hao watu wake hawawezi kamwe, maana wanaposibility kubwa ya kupewa posho wanyamaze.
INAUDHI SANA...
Fingigwe
05-08-2009, 04:05 PM
Mponjoli
Pamoja na kwamba nimechelewa kuona maoni yako lakini nakushukuru sana sana kwa mawazo ya kina kuhusu ujinga huu ulioruhusiwa kuenea nchini. Mimi siku zote naamini magazeti kama ya Global Publishers na sanaa duni zilizoenea TZ zinachangia si tu katika kuharibu maadili bali hata katika kurudisha nyuma uwezo wa kufikiri katika jamii.
Uwezo wa wa-Tz wengi kuchambua masuala magumu hata ya maisha yao ya kawaida tu unazidi kudidimia. Wananchi hawana budi kujua kwamba masuala ya mahusiano ya kifamilia, kikazi, kiuchumi, mapenzi, n.k. yana mikanganyiko (complexity) yake ambayo badala ya kuchambuliwa ipasavyo katika habari, riwaya na filamu zetu, yanapewa mitizamo ya kishabiki na kidhalilishaji tu (ponography) ili wajinga waendelee kufurahia aibu za wengine bila kuelewa tatizo liko wapi na msaada upi utolewe.
Basi kama serikali yetu imeamua kuendekeza ujinga huo, so well and good, viongozi wakae tayari kukutana na adha zote za kihuni zitakazowapata na familia zao kama ilivyo kwa wananchi wengine. Halafu, viongozi wa dini nao wawe makini; waweze pia kukemea yeyote anayetumia NENO kueneza upumbavu katika jamii vinginevyo wengine tutaanza kuamini kuwa dini nayo imegeuzwa kuwa mkakati mkubwa wa kibiashara kwa kuwapumbaza wasiokuwa na uwezo wa kufikiri - manake siku hizi wapo wengi sana wakiambiwa tu "Bwana asifiwe" hawafikiri tena; mtu anaweza kuwauza wazimawazima na akili zao. I REALLY DO NOT KNOW WHAT HAPPENED TO THIS COUNTRY!
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.