PDA

View Full Version : Mengi mbele ya PAPA



Dalali
04-24-2009, 03:54 PM
]Iliposomwa taarifa ya Mengi akiongelea Mafisadi kwa majina nilipata ganzi kwani nilifikiria huyu Mzee antafuta nini?
Nilidhani 1-Mzee anatafuta umaarufu siku za mwiso mwisho 2-Anamkumbusha DPP kuwa mafisadi wengi amewaacha. 3-Mzee katumwa kusafisha njia ya mafisadi wazalendo 4-mzee amechoka kuishi 5-Anatumia haki yake kusema linalomsibu kama raia mwema tena Tajiri. Nafikiri sababu ya tatu imechota fikra nyingi kwa vile tulipo tu njia PANDA ki-Siasa mambo yanakoelekea ni kule watawala hawakutaka tuende ile wamejikuta wanaenda tena kwa kasi ya ajabu.Muda wa kufikia kipenga ni mfupi kulikospeed yetu na kwa kuwa breki hazifanyi kazi mti unatafutwa na dereva kugotesha hili lori ili usalama upatikane.
Papa waliotajwa ni Waasia watu wa kuja nasi tu malaya wa kujiuza kwao na nchi tunayo tunapokwenda kwao tukiwahakikishia usalama kwa lolote baya na pesa wanzo kwa nini wasivune?
Nadhani JK anaona upepo uvumao si salama kwa jahazi na ana nadhiri na mafisadi kwani ilifaa sana waachie madaraka yao yote kwa harufu hii mbaya iliyowakumba.Kutafuta fabricated justification inatia shaka.Naogopa umaarufu wa huyu mzee kutumika vibaya.Issue zote ziko Mahakamani tuone zinafanyikaje huko na nani anatengenezewa daraja avuke mto.Hii ni njia ya kusafisha chama kilichojaa watu waovu.Mengi hajataja jina hata moja la Mswahili je hawapo, au wao ni nafuu.Huwezi kuoga taulo ukiwa nalo kiunoni.
Mapapa ni sisi kwa vile tulishafikaia hatua tunasaini mikataba mizito nje ya nchi tena umalaya huu papa akuache.Mzee Mengi awataje waswahili walio nusu papa tuwajue na kila mmoja amehusikaje! ukifikia hatua ya kutetea mikataba ya kuibia wananchi bila aibu ni ideolgy za mapapa
Takari
dalali

hofstede
04-24-2009, 09:41 PM
Hii movement sasa iwe kwa wananchi wote. Unajua hawa mafisadi aliowataja Mengi wanatumiwa na mafisadi wa Serikalini na katika chama, Mfano watu kama kina Makamba wenye volume ndogo ya ubongo wao wanafikiria misaada tu ya hawa jamaa katika chama ili washinde wanashindwa kujua kuwa hela hizo ni zetu.

Mengi ni mzalendo halisi na anahitaji kuungwa mkono na watanzania wenye nia njema na nchi hii bila ya kuogopa kitu. dawa ya hawa watu ni kuwatimua nchini tu mbona Chavda walimtimua?. Serikalini watu wanaiba na kuwatumia hawa "Corruption sharks" ili ionekane ni wafanya biashara kumbe ani wezi watupu, Tumeanza na hawa mapapa sasa kuna wanaowalinda hawa mapapa nao ni kama wafuatao.
1. Makamba

2. Lowassa

3. DPP

4. Mkapa

5. UWT

7. Kingunge (Huyu anatumia influence ya ushauri wa siasa kumtisha JK asiwachukulie hatua hawa watu)

8. Inner circle wa IKULU, wanamzunguuka JK, hawa wote ni wezi. Kikwete Timua wote tuanze mwanzo Mjomba, umezunguukwa na wachumia tumbo lawama zote zinakuja kwako. Kiongozi mzuri hukumbukwa kwa Huduma kwa wananchi na si kuendeleza mshikamano wa chama cha mafisadi.6

Ach-F
04-25-2009, 01:17 AM
Tunasubiri waanze kutoana ngeu.

Fingigwe
04-25-2009, 01:51 PM
Kama alivyosema Dalali hata mimi nilijiuliza mengi. Nilisema huyu mzee sasa kachoka kuishi. Lakini kubwa zaidi ambalo sina budi kukiri siku zote huwa namuona Mzee Mengi kuwa mtu wa kutafuta sifa. Hata hivyo nakubaliana naye katika hizi harakati zake za kumulika mafisadi ingawa, kwa upande mwingine, naamini inatokana zaidi na mapambano yake binafsi katika uwanja wa biashara ambapo mafisadi hasa wenye asili ya kiasia wameudhibiti na kuhakikisha hakuna mswahili anayeweza kuwika.

Kwa usemi mwingine, ni kwamba katika nchi yetu ambapo biashara makini na halali hazipewi mwanya, bila kuwa fisadi hufiki mbali. Na kwa upande huo, kuna mpaka ambao huwezi kuvuka kirahisi. Ma-mafia wenye asili ya kiasia wamehakikisha kuwa si rahisi kwa mswahili kuifikia heshima ya kuwa "fisadi papa".

Pamoja na hayo, Mzee Mengi angetenda haki na kuonyesha kwamba anaongozwa na mantiki zaidi kuliko jazba kama pia angewataja washiriki wakuu wanaowatumia au kutumiwa na mafisadi papa. Shilingi haiwezi kuwa na upande mmoja. Aidha, kwa kuwataja wenye asili ya kiasia tu huku ukiwaacha waswahili tuliowakabidhi madaraka ya kusimamia rasilimali zetu (kwa ujinga wetu sijui?) basi unaififisha dhana nzima ya "mafisadi papa" na hata kutoa mwanya kwa wengine kudai kuwa unachomeka hoja ya ubaguzi wa rangi kinyemela kama alivyofanya Hitler kwa Wayahudi miaka ya 1930.

Kwa upande mwingine, nitashangaa sana kama waliotajwa kuwa "mafisadi papa" hawataenda mahakamani kumdai Mzee Mengi awaombe radhi kwa kuwachafulia "heshima zao kubwa" walizozijenga kwa miongo mingi katika taifa hili. Wakikaa kimya basi itabidi tujue si tu kwamba waswahili tunaibiwa, bali pia tumedharauliwa kabisa - yaleyale ya dua la kuku.

mwanakijiji
04-27-2009, 08:42 AM
unajua wakati mwingine pia tujiulize kwanini hadi mzee Mengi aseme? wengine wako wapi? kama anavyosema Fingiwe hapo juu kama Mengi hakuwataja wote na sisi wengine tunawajua hao wengine kwanini sisi tusiwataje? Nadhani hatuwezi kumuangalia Mengi kusema kila kitu yeye wakati sisi wengine tunashabikia tu.

Mimi nadhani yeye kaanza sisi wengine tufuate! Sasa kwa kuanza kuangalia rangi peke yake mwisho tutajiuliza mbona walioatajwa ni waswahili wa pwani tu je hakuna mafisadi wa kutoka bara? Na wakitajwa na wa bara huko tutajiuliza hakuna mafisadi ambao ni warefu n.k


Hii sensitivity ya kutaka kuonekana kutowapendelea mafisadi au kuwaonea tunaitoa wapi. Kama kuna mafisadi 20 wachagga wasitajwe hadi wachanganywe na wamakua? Na kama wapo mafisadi ambao ni wa dini moja kwenye sehemu fulani inabidi tuwe fair kwa kuwatafuta mafisadi wa dini nyingine?

fisadi ni fisadi tu haijalishi rangi yake, kabili yake au dini yake!