PDA

View Full Version : Kupika Vitumbua



mwanakijiji
11-12-2008, 04:02 PM
Mapishi ya Bi. Aziza yanaendelea hivi:

MAHITAJI


mchele nusu kilo
Tumia nusu ya robo ya unga wa ngano
Sukari unavyopenda
vijiko 2 vya cha Hamira
vikombe 2 vya chai tui la nazi
Mafuta ya kupikia
Iliki



MAPISHI:

MATAYARISHO
-Osha na kuroweka mchele ndani ya maji ya baridi masaa manane au siku moja.
- Mimina vifaa vyote ispokuwa sukari, ndani ya blender na usage mpaka mchele uwe umesagika kabisa.
- Mimina sukari ndani ya mchanganyiko na usage tena kidogo tu.
- Mimina mchanganyiko ndani ya bakuli na ufinike. Weka bakuli mahali penye joto ili mchanganyiko uuumuke.
- Mchanganyiko ukisha umuka, weka karai kwenye moto.
- Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia kila kitumbua.
- Mimina mchanganyiko kiasi kwenye karai kulingana na kikarai unachotumia.
- Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
- Panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.

Kepa
11-12-2008, 05:37 PM
Mbona sasa hilo pishi linatisha? kwa nini limewekwa neno VITUMBA rangi nyekundu? au vinawekwa pilipili pia? Siye tusiotumia pilipili inakuwaje hapo. Hebu tusaidie kumuuliza huyo Aziza vizuri

mwanakijiji
11-13-2008, 08:08 AM
Unaona rangi nyekundu wapi tena?

Kepa
11-13-2008, 11:11 AM
Unaona rangi nyekundu wapi tena?

Leo haipo tena, ila niliiona the dai nimepita hapa. Msatali wa mwisho neno neno vitumbua lilikuwa limeandikwa kwa wino mwekundu. Nikashangaa sana, kulikoni msisitizo mwishoni???