PDA

View Full Version : Mlipuko wa Mabomu Mbagala, Uchunguzi na Hatua..



WANDERER
04-29-2009, 03:26 PM
BREAKING NEWS: MABOMU YALIPUKA MBAGALA!! photos


Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyoko Mbagal Kizuiani, inalipuka na nyumba zilizopo jirani na kambi hiyo zimeshika moto!! Habari kutoka kwenye eneo la tukio zinasema kuwa, mabomu hayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye ghala la silaha la kambi hiyo na yamekuwa yakiripuka kila baada ya sekendu chache na yanendelea kulipuka hadi wakati huu tunawaletea taarifa hii. Kishindo cha milipuko ya mabomu hayo, ambayo yameleta hofu kubwa katika jiji la Dar es salaam, hasa maeneo ya Mbagala, Mtoni kwa Azizi Ally na maeneo ya Temeke, kimekuwa kikisikika hadi maeneo ya Mwenge.

Kwa mujibu wa habari za Radio One, mtu mmoja hadi sasa ameripotiwa kufa katika kadhia hiyo ya aina yake baada ya bomu moja kuangukia ndani ya nyumba yake na kuiteketeza na kwa sasa barabara ya Kilwa imefungwa, magari kutoka Kongowe kuja Mbagala, yamezuiwa. Waandishi wetu wako eneo la tukio na tutawajia baadae na picha za tukio hili la kwanza na la aina yake kutokea nchini.

mwanakijiji
04-29-2009, 07:57 PM
Ghala la silala lalipuka; Dar yatikisika

Milipuko mikubwa ya mabomu imetokea leo huko Mbagala katika ghala ya silaha ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, milipuko ambayo imesababisha wasiwasi mkubwa kwa wakazi wa Jiji la Dar na vitongoji vyake. Habari za awali zinasema kuwa milipuko hiyo siyo jambo la mazoezi bali ni ajali.

Hadi hivi sasa idadi taarifa za awali zinasema watu watatu wamekufa na wengine wengi kujeruhiwa na kukimbizwa kwenda hospitali ya Temeke na hospitali nyingine za jirani. Taarifa za awali za kijeshi zilitoa wito kwa wananchi walioko ndani ya usawa wa kilomita 25 kuhama maeneo yao na muda mfupi uliopita Naibu Waziri wa Ulinzi Bw. Emmanuel Nchimbi amerudia wito huo kupitia ITV na kuwataka watu waliokuwa kwenye majengo marefu kuteremka.

Milio na mtikiso wa mabomu hayo umesikika hadi maaeneo ya Msasani upande mwingine wa Jiji la Dar huku maofisi na maeneo ya makazi baina ya pande hizo mbili yakiwa katika hali ya wasiwasi, na watu wakipata na mshtuko.

Kufuatia mlipuko huo Polisi wametoa maelekezo kuwa mtu yeyote akiona kifaa cha chuma ambacho kimeangukia kwenye nyumba yake au eneo lake asijaribu kukihamisha bali kutoa taarifa Polisi kwani kuna mabomu mengine yamerushwa katika mlipuko huo lakini bado hayajlipuka.

Vivyo hivyo, serikali imeahidi kuwahudumia bure wale wote ambao wamejeruhiwa katika mlipuko huo na kusaidia katika kukarabati makazi ya wale ambao nyumba zao zimeharibiwa kufutia mlipuko huo mkubwa. Vyanzo mbalimbali vya habari vinadokeza kuwa wengi wa waliojeruhiwa ni pamoja na watoto wa shule ya Msingi ambayo iko jirani na eneo hilo na wakazi ambao nyumba zao zimelizunguka ghala hilo.

Juhudi za uokoaji na udhibiti wa hali zinaendelea kukiwa na ushirikiano kati ya Jeshi la Wananchi, Polisi na vyombo vingine vya usalama pamoja na vyombo binafsi vya uokoaji kama Ultimate Security.

Jiji la Dar ambalo lina wakazi karibu milioni tatu lina kituo kimoja tu cha Uokoaji na haijulikani kama Jeshi la Wananchi wa Tanzania linakituo chake cha Zimamoto kwani katika eneo la Dar na Pwani Jeshi hilo lina kambi mbalimbali, mahospitali pamoja na vikosi vingine mbalimbali.

Kwa upande wa JWTZ, kuna wanajeshi ambao wamekufa kishujaa katika jitihada za kukabiliana na mlipuko huo ili kuzuia mabomu yasidhuru jamii zaidi. Kwa hesabu yoyote leo itakuwa ni siku ya majonzi makubwa kwa Taifa kwani idadi ya waliokufa inaweza kuwa kubwa sana na ya wale waliojeruhiwa kupita hata ukadiriaji wa haraka. Madhara kwa nyumba na vitu mbalimbali inakadiriwa kupitia mabilioni. Tunaombea hilo halitakuwa hivyo vumbi zima likishatulia.

KLHN na wasomaji wake wote tunaungana na serikali kutoa wito kwa wananchi kufuata maagizo yote yanayotolewa na vyombo vya usalama wakati huu na kuhakikisha kuwa wakati kama huu kama kitu kimoja tunaweka tofauti zetu pembeni na kuhakikisha tunasaidiana. Tusimame pamoja na kuzuia uporoji wowote ambao unaweza kutokea kwenye nyumba za wale walioathirika na tusikubali watu wachache watumie tukio hili kama nafasi ya kufanya uhalifu.

Tunatoa taasisi mbalimbali ambazo zinauwezo kuanza mara moja kutoa misaada ya kiutu kusaidia wale wote walioathirika, kujeruhiwa au kupoteza vitu mbalimbali kwani tukio hili japo tutajua zaidi chanzo chake hapo baadaye ni msiba wa taifa letu na kimguse kila mmoja kama tulivyoguswa na mambo ya kipuuza ya zeutamu!

Hili ndilo tukio la kutuunganisha Watanzania wote wakati huu na mambo ya nani awajibike au asiwajibike yaje baada ya kuhakikisha kuwa hali imerudishwa katika usalama, waliojeruhiwa wanajulikana na hatua madhubuti zimechukuliwa kuhakikisha usalama wa eneo hilo. Kutoka hapo, ndipo sauti zetu zipae juu ya jinsi gani tukio hili lingeweza kuzuiliwa kwani wengine tuliandika mambo haya karibu mwaka mzima kwa sababu tunaamini Jiji la Dar limekaa katika hali ya majanga makubwa sana. Na hili yawezekana ni dokezo tu.

Tutasema zaidi baadaye.

Tunawaombea rehema wale waliopoteza maisha yao, unafuu na uponyi wale waliojeruhiwa na ujasiri na moyo wa kujitoa zaidi kwa wale ambao wanasimama kuhakikisha usalama wa Taifa letu.

Mpita Njia
04-30-2009, 10:54 AM
Mabomu yaliripuka wakati yakihamishwa-mengine yalikuwa yapelekwe Shinyanga na mengine yalikuwa yanaandaliwa kwa ajili ya safari ya Darfur pamoja na kikosi cha kulinda amani kutoka TZ.
Lakini jeshi halitaki kusema kulikuwa na askari wangapi ndani ya ghala wakati mlipuko unatokea

mwanakijiji
04-30-2009, 10:56 AM
Kwa namna fulani tunaamini kuwa sisi tuna upendeleo wa aina fulani kwa Mwenyezi Mungu, kwamba nchi yetu kwa sababu upendeleo wa pekee basi haitapata majanga. Hatujajifunza kwa ajali zinazotea mara kwa mara za mabasi, hatujajifunza kwenye ajali za majini, hatujajifunza kwenye milipuko ya mabomu na kwa hakika tuko kama tumepigwa ganzi ya aina fulani hivi.

Pamoja na kutoa pole na rambirambi, ni lazima tujiulize tutaendelea mpaka kulini kwa kutegemea rehema za Mungu? Sitoshangaa leo tutaambiwa katika Hotuba ya Rais kuwa haya yalikuwa ni mapenzi ya Mungu na ya kuwa wanaunda tume kuchunguza kitu gani kilisababisha na wananchi wasiwe na wasiwasi hali ni shwari na halikuwa tukio la kighaidi..

Katika wazimu wetu tutasema Amen.. na kusahau kabisa mlolongo wa kutojiandaa na majanga ambao serikali ya CCM imeuendeleza kwa miaka kadhaa sasa na kutuacha tuishi kwa bahati!

Jana, tumeikwepa risasi! Huko mbeleni (na itakuwa hivyo kwani majanga yataendelea kutokea hata kama tunaombea yasitokee, ndiyo kanuni ya ulimwengu!) tutakuja kulia kama tulivyolia kwenye MV. Bukoba na Bahi! (wengine wanajiuliza "Bahi?"! wameshasahau!

I have more to say.. listen..

Sikiliza:Mlipuko 511KJ Mbagala: Majanga na kuishi kwa kudra! (http://mwanakijiji.podOmatic.com)

Update: Nasikia hadi hivi sasa waliokufa wamefikia 10

Mpita Njia
04-30-2009, 11:11 AM
Nina hamu ya kufahamu ni kipi kilikuwa cha kwanza kujengwa kwenye eneo lile-kambi ya jeshi au makazi ya wananchi

mwanakijiji
05-09-2009, 11:34 PM
Na Frederick Katulanda, Busanda



WAKATI joto la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda likizidi kuongezeka, vyama vya siasa vinavyowania kiti hicho vimebadili mbinu za kampeni, ikiwa ni pamoja na kuwaita wabunge na viongozi wake wa kitaifa ili kujiimarisha.

Kwa upande wa CCM mbali ya kumtumia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, John Malecela wamelazimika kumwondoa mjumbe wake wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Anthony Diallo ili kuliingiza kundi la mmoja wa wagombea aliyeshindwa kura za maoni kwa nia ya kuziba mpasuko unaokisumbua chama hicho.

Habari za ndani ya CCM zimeeleza kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kampeni zao kupata upinzani mkali ikiwa ni pamoja na kuzomewa na watu wachache kujitokeza kwenye mikutano yao; wameamua kuunganisha makundi yanayohasimiana kwa kumuita aliyeibuka mshindi wa pili, Doanard Max ili asaidie kumnadi mgombea wao.

Diallo ametajwa kuwa hasimu mkubwa wa Max kutokana na kudaiwa kumsaidia mmoja wa wagombea kwa nia ya kumuengua (Max), jambo ambalo liligawa kura zake na kumfanya mgombea wa sasa kuibuka wa kwanza. Max alishika nafasi ya pili huku Sostenes Kulwa anayedaiwa kuungwa mkono na Diallo kuambulia nafasi ya tatu.

Sambamba na hatua hiyo, pia CCM imeamua kuwaita wabunge wake wote wa Mkoa wa Mwanza kwenda jimboni humo kusaidia kampeni za uchaguzi huo na wamepangiwa kata mbalimbali za jimbo hilo.

Mbali na wabunge hao pia CCM katika kuhakikisha inalikomboa jimbo lililoachwa na aliyekuwa mbunge wake, Kabuzi Rwilomba, imepunguza mikutano ya kampeni ya nje na kuimarisha ile ya ndani ili kuepuka kuzomewa.

Lakini Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Rajabu Kundya amekanusha kuondolewa kwa Diallo ili kumuita Max, bali ameondoka Busanda baada ya kutumwa Dar es salaam kwa ‘masuala mengine ya kichama’.

Kundya alisema chama chake kimewapangia kazi wabunge wake katika jimbo hilo na kufafanua kuwa kila mbunge amepangiwa kata kusimamia kampeni hadi wakati wa upigaji kura.

Hayo yakijiri, kampeni za wapinzani wa chama hicho, hasa Chadema, zinazidi kunoga na mikutano yake kupata idadi kubwa ya watu, ikilinganishwa na chama hicho kikongwe.

Kama CCM, pia inaelekea mambo ni mazito kwa chama cha CUF, kwa kuwa nacho kimeweka mkakati wa kuongeza nguvu kwenye kampeni zake kwa kuwaita wabunge wake kwa ajili ya kusaidia kumnadi mgombe wake, Oscar Ndalawah.

Katibu wa timu ya uchaguzi ya CUF, Maole Kuchilungulo aliwataja wabunge kuwa ni Magreth Sakaya, Savelina Mwijage, Nuru Bafadhiri na Zaharani Mwanakwetu, wote wakiwa wa viti maalumu. Wengine ni Omari Ally Mzee, Salum Abdallah na Mohamed Mnyaa wote wa Pemba.

Kwa mujibu wa katibu huyo, lengo la kuwaita wabunge hao ni kusimamia kampeni katika kila kata kwa kile alichosema, baada ya kubaini kuwa CCM imeleta wabunge wake na kuwatawanya kila kata kufanya hujuma ambayo hata hivyo hakuitaja.

“Awali CCM walitudharau, walijua kuwa mshindani wao ni Chadema, lakini baada ya kufanya mikutano wamegundua kuwa mgombea wetu ana nguvu zaidi ya kwao na wa Chadema; wamepanga mkakati wa kutuhujumu na baada ya kubaini hilo tumeamua kuwaita wabunge wetu ili kuja kuchuana na wenzao wa CCM katika kila kata,” alieleza.

Chadema

Kwa upande wa Chadema wakiwa bado wanaendelea na kampeni za nje na zile za ndani walisema wameamua kumuita Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kwa ajili ya kuongeza mashambulizi ya hoja na kufafanua kwa nini jimbo hilo limekuwa nyuma kimaendeleo.

Afisa Habari wa Chandema, David Kafulila alisema wao wamejipanga na kwamba kwa kuanza wameamua kumuita Kabwe ambaye atawasha moto katika kampeni hizo na baadaye kufuatiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

“Hatuna wasiwasi, tuna mikakati mingi lakini naweza kusema tu tumeamua kumuita Zitto Kabwe ambaye sasa atakuwa akiambatana na mgombea katika mikutano hiyo kumnadi kwa wapiga kura,” alieleza.

Green Guird’ walilia posho

Katika hatua nyingine, Vijana 24 wa kikundi cha ulinzi cha CCM (Green Guard), wamelalamikia kupunjwa posho zao na kulipwa Sh800 kwa siku badala ya Sh2,000 walizoahidiwa.

Barua yao ya Mei 5,mwaka huu iliyoandikwa na kusainiwa na David Azaria ilieleza kuwa posho ambayo walistaili kulipwa jumla ya vijana 30 ni Sh 5,000 kwa wageni na Sh2,000 kwa wenyeji wa wilaya hiyo lakini wote wamekuwa wakilipwa Sh800 huku wakielezwa kuwa pesa hakuna.

“Maisha katika mji wa Geita ni magumu, lakini unalipwa Sh800, wanasema chakula tutakula huko. Hivi sasa hali ya maisha yetu ni ngumu sana, lakini tumejaribu kulalamika kwa Katibu wa CCM wilaya amesema tupokee na wasiotaka waondoke,” alieleza mmoja wa vijana hao ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Akijibu malalamiko hayo, Kundya alisema tatizo hilo kwa sasa limemalizika baada ya yeye kufika na watu wote waliopo katika kampeni wanalipwa kulingana na taratibu za fedha za chama.

“Tatizo hilo halipo, kuanzia nilipowasili wanalipwa kwa staili na taratibu za chama,” alieleza Kundya.

Misimamizi wa uchaguzi

Vile vile CUF kimemtaka Msimamizi wa Uchaguzi kufuta zoezi la kuajiri makarani wa uchaguzi kutokana na kuchelewesha kutoa tangazo lake.

Afisa Uchaguzi wa CUF, Hussein Mmasi alisema kuwa tayari chama chake kimemlima barua msimamizi huyo kikieleza kuwa zoezi hilo limegubikwa na utata mkubwa, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa limefanywa makusudi kwa ajili ya kuisaidia CCM.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi jimboni hapa, Jackson Sombe amekiri kupokea malalamiko yao, lakini alikanusha kuwa matangazo hayo yalibandikwa siku ya mwisho.

“Nimepata malalamiko yao, lakini siwezi kubatilisha zoezi hilo, kwa sababu matangazo hayo hayakutolewa siku ya mwisho kama wanavyoeleza wao; yalibandikwa mapema kabisa, nimewaomba kwa kuwaandikia waje hapa ofisini kwangu kuhakiki majina ya makarani hao ili kama kuna mtu wana mashaka naye waseme aondolewe hawajaja,” alisema Sombe.

Katika hatua nyingine, msimamizi msaidizi wa uchaguzi imevionya vyama vyote vya siasa kujiepusha na uvunjifu wa amani katika mikutano yao ili kuepuka vurugu kama za Tarime.

Sombe alisema vyama vote vinapaswa kuzingatia muda wa kuanza mikutano na kumaliza na kufuata ratiba ya mikutano ili kuepuka migongano.

“Niwaombe tu viongozi wa vyama kuzingatia haya, muda wa kufanya mikutano na kumaliza na kuwazuia wanachama wao kuwazomea wengine na kurushiana maneno,” alieleza.

Uchaguzi wa Busanda unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Faustine Kabuzi Rwilomba.

Katika uchaguzi huo vyama ambavyo vimeweka wagombea ni CCM, Chadema, CUF na UDP lakini mchuano mkali umekuwa kati ya wagombea wawili wa CCM na Chadema.

Ach-F
05-16-2009, 11:03 PM
Wakati Walipa kodi wanateketea na mabomu viongozi wa CCM wamekuwa mstari wa mbele kuhujumu kila aina ya pesa kutoka kwa walipa kodi na hivi sasa wamehamia NSSF baada ya soo la BOT.