PDA

View Full Version : Tatizo la Benki Kuu hasa ni nini?



mwanakijiji
05-10-2009, 11:42 PM
Mambo yaliyotokea Benki Kuu kama yangetokea mahali ambapo kweli kuna utawala wa sheria na viongozi wenye kuthubutu kuna watu wangekuwa Segerea siku nyingi kweli. Madudu yaliyotokea hapo yananifanya nijiulize hasa tatizo lililokuwepo na bado lipo ni ninii hasa?

Iliwezekana vipi karibu shilingi trilioni moja kuchotwa kama kisimani na hadi leo hakuna mtu aliyefungwa au kushtakiwa kwa kuhujumu uchumi?

Ach-F
05-16-2009, 10:51 PM
Mwanakijiji

Hao ndio Chama Cha Majambazi wakiongozwa na mafisadi wakuu ambao fedha ya walipa kodi imewekwa alama yao. Wameweka pamba masikioni wakifikiri WTZ wote ni wenda wazimu wanachota kama wapendavyo na hakuna wa kuwawajibisha. Ungefikiri 2010 Watanzania wangeweza kubadilika.

Mpita Njia
05-19-2009, 07:53 PM
hayatokei kwa bahati mbaya, na ndio maana unaona kuwa hakuna anayechukuliwa hatua