PDA

View Full Version : Apson naye?



mwanakijiji
11-13-2008, 09:06 AM
Hivi tunajua nini kuhusu huyu bvwana aliyewahi kuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa wakati wizi mkubwa wa fedha za nchi yetu unafanyika? Kuna mtu anaweza kumhoji...? Yawezekana kuwa ndio sababu ya timu ya kina Mwanyika kwenda kama wanapapasa ukuta wakiwa wamefungwa vitambaa machoni?

Tunaweza kuelewa wizi wa Kagoda bila kumhoji huyu bwana maana nakumbuka sababu iliyotolewa na Balali kuhusu malipo ya Kagoda ni kuwa ilikuwa ni kwa shughuli ya Usalama wa Taifa na hadi leo hii siyo Apson, wala RO ambao wamekanusha kuwa taasisi yao haihusiki.. nani atanyosha kidole?

Mpita Njia
11-13-2008, 01:28 PM
Upo uwezekano kuwa kazi iliyofanywa na akina Mwanyika, ilihusisha pia kuficha kuhusina kwa Usalama wa taifa kwenye sakata hili.

mwanakijiji
11-13-2008, 04:44 PM
Lakini kwanini hawa Usalama wa Taifa hawaulizwi maswali?

Mpita Njia
11-13-2008, 05:49 PM
naamini upo mkakati, wa makusudi na wa chinichini wa kuwatenganisha UWT na hili jambo. Si ajabu kuwa Deloite walitishwa (au walikuwa compromised?) walipolibaini hili mapema. Si ajabu kuwa baada ra Ernst % Young kutoa ripoti, ambayo ilionyesha kila kitu wazi, ikaundwa kamati kufanya uchunguzi.
Si ajabu kuwa baada ya kamati ilipomaliza kazi, ikaandika ripoti na kusisitiza kuiwasilisha kwa rais wakati haikuagizwa hivyo. Lakini ukumbuke kuwa hili (la kuandika ripoti) ni kama lilishinikizwa na vyombo vya habari. Yupo anayejua chanzo hasa cha habari hiyo?

mwanakijiji
11-14-2008, 04:31 PM
Sasa unapokuwa na usalama wa Taifa ambao uko compromised namna hiyo, taifa linakuwa salama kwa kiasi gani? Na ni nani ambaye atakuwa na ujasiri wa kuhoji kinachoendelea huko?

Mpita Njia
11-14-2008, 06:09 PM
Ni vigumu kujua kama usalama wa taifa upo kwa ajili ya hao jamaa wa usalama wa taifa kwa sababu niliwahi kuelezwa na watu wa ikulu kuwa kuna wakati haya mkuu mwenyewe huwa anasita kuzikubali kwa asilimia 100 taarifa kutoka uwt akihisi kuwa huenda ni za kupikwa.
Kwa kiasi fulani ninaamini habari hizi kwa sababu yeye mwenye anajua kuwa aliwatumia hawa watu wakati akitafuta kuingia madarakani, anafahamu kuwa na wengine waliwatumia pia lakini yeye akacheza karata zake vema. Anajua kuwa katika hali kama hiyo, lazima kuna some elements ambazo bado zipo loyal kwa wapinzani wake na ni rahisi kumchomekea mambo.
tatizo lilianza pale uwt walipokubali kutumika kisiasa

mwanakijiji
11-14-2008, 07:07 PM
Nasikia mtoto wa Apson na yeye yumo kwenye hii EPA na ndiyo sababu inakuwa ngumu kweli kushughulikia Kagoda..

Mpita Njia
11-16-2008, 10:55 AM
Kagoda ni ngumu sana kwao, licha ya mtoto wa Apson, basically nionavyo mimi, Kagoda is CCM kwa sababu ndiyo iyotumika kupata sehemu kubwa ya fedha za kampeni