PDA

View Full Version : Tamko la Mkuchika lilikuwa na ulazima?



mwanakijiji
05-12-2009, 11:04 AM
Hili la serikali..

BREAKING NEWS!!! TAMKO LA SERIKALI
JAMHURI VA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICfIEZO


TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MALUMBANO KATI YA MWENYEKITI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA IPP, BWANA REGINALD MENGI, NA MBUNGE WA IGUNGA, MHESHIMIWA ROSTAM AZIZ
1. Takribani wiki mbili sasa, kupitia vyombo mbalimbali vya habari, Taifa limegubikwa na malumbano makali kati ya wafanyabiashara wawili, Bwana Reginald Mengi, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, na Mheshimiwa Rostam Aziz, Mbunge wa Igunga, malumbano ambayo yamejikita katika suala la Ufisadi na Mafisadi.
2. Wafanyabiashara hawa wawili, Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Aziz, kwa nyakati tofauti, wametumia vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo wanavyomiliki huku kila mmoja akimtuhumu rnwenziwe kuwa fisadi.
3. Kwa mfano, tarehe 23 Aprili, 2009, Bwana Reginald Mengi aliandaa Mkutano wa Waandishi wa Habari (Press Conference) ambapo aliyataja makampuni na wafanyabiashara watano wa hapa nchini, akiwamo Mheshimiwa Rostam Aziz, akiwaita kuwa ni "MAFISADI PAPA" na kuwaornba wananchi kuungana nave iIi kupambana na "mafisadi" hao.
4. Sikuchache baadaye.mmoja wa waliotajwa kuwa "Mafisadi Papa", Mheshimiwa Rostam Aziz, alijibu taarifa ya Bwana Mengi kupitia mkutano wa waandishi wa habari, akikanusha tuhul11a hizo. Aidha, alimtaja Bwana Reginald Mengi kuwa ni "FISADI NYANGUMI" na kuorodhesha tuhuma kadhaa za ufisadi zilizofanywa na Bwana Mengi.
5. Serikali imeyatafakari malumbano ya wafanyabiashara hawa na kubaini kwamba yanalipeleka Taifa letu mahali pabaya, kwani malumbano have yana mwelekeo wa uvunjaji wa amani kama yataachiwa kuendelea.

6. Ni Kweli kwamba Katiba ya Nchi yetu inatoa uhuru wa kila mwananchi kuongea, kutoa na kupokea habari; lakini I
7. Serikali imebaini kuwa malumbano ya Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi yamewagawa wailanchi katika makundi mawili; ya wale wanaounga mkono kauli ya Mheshimiwa Rostam Aziz, na wale wanounga mkono kauli ya Bwana Reginald Mengi.
8. Aidha, Serikali imebaini kwamba katika malumbano haya kumekuwepo na "matumizi mabaya" ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Bwana Mengi, (televisheni, magazeti na radio), na kwa Mheshimiwa Rostam Aziz, (magazeti). Kila mmoja ametumia vyombo vya habari anavyomiliki kwa manufaa yake binafsi kinyume na maelekezo ya Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003, inayobainisha wazi kwamba:-
? Chombo eha habari kisitumiwe kwa manufaa binafsi ya mmiliki au mtendaji bali kitatumiwa kwa manufaa ya umma;
? Chombo eha habari kiongozwe na maadili ya taaluma na jamii husika; na
? Chombo eha habari kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, kabila, dini, jinsia au ulemavu au kuehoehea uhasama.
9. Katika hali hiyo malumbano ya Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi yakiachiwa kuendelea yanaweza kulitumbukiza Taifa letu katika uvunjaji wa amani.
10. Kutokana na hali hiyo basi, Serikali inawataka Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi kuacha mara moja malumbano kupitia vyombo vya habari, na badala yake wawasilishe madai na vielelezo vyao kwa mamlaka husika ili hatua zinazofaa zichukuliwe,na wananchi wapewe taarifa na vyombo hivyo.

11. Serikali haitakubali kusikia malumbano ya Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi ambayo yanaweza kuleta uvunjaji wa amani nchini, yakiendelea. Serikali pia haitavumilia kuona vyombo vya habari nchini vikichangia kliligawa Taifa katika makundi, na kudumaza maendeleo.
12. Aidha, Serikali inawataka Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Aziz kuvitumia vyombo vyao vya habari kwa manufaa ya Wananchi wote wa Tanzania, na si kwa manufaa yao binafsi. Wakumbuke kwamba malumbano yao hayo kwa kutumia vyombo vyao binafsi, na wakati mwingine kuonekana kana kwamba wanalihutubia Taifa, ni kutowatendea haki watu wengine ama kampuni/mashirika ambayo yametajwa katika malumbano hayo, lakini hawana vyombo binafsi (redio, televisheni, rnagazeti) ambavyo wangeweza kuvitumia kujieleza na kujitetea kama walivyofanya Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Azizi.
13. Serikali imesikitishwa na kitendo eha Bwana Reginald Mengi eha kuzungumzia kesi ambazo tayari ziko Mahakamani. Sheria za nchi zinakataza mtu, watu kuzungumzia ama klljadili suala ambalo tayari liko Mahakarnani. Kwa kufanya hivyo, Bwana Reginald Mengi arnewahukumu watuhumiwa l1ao na kuwatia hatian; bila wao kupewa fursa ya kusikilizwa ("They have been condemned unheard''). Kwa mujibu wa Sheria za nehi, Mal1akama peke yake ndiyo inayoweza kumtia hatiani mtuhurniwa.
14. Aidha, Serikali inawatahadharisha Wahar;,.i wa Wanahabari kwa ujurnla kuwa makini katika kutirniza wajibu wao kwa weledi na kuzingalia maadili ya taalurna yao, badala ya kuandika au kutangaza habari kulingana na matakwa ya mmiliki wa chombo kinachohllsika.
15. Hivyo basi kuanzia sasa, Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wamiliki wa vyombo vya habari ambao hawatazingatia weledi (professionalism), Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na Sheria ya Utangazaji ya Mwaka 2003, katika kutekeleza kazi zao za I

16. Mwisho, Serikali kwa mara nyingine inasisitiza kwamba mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi bade yanaendelea, na inawahimiza wananchi wote wenye taarifa za vitendo kama hivyo watoe taarifa hizo kwenye vyombo vya dol a vilivyopewa majukumu hayo, iIi hatua ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo basi, Serikali inawataka wananchi wote kufuata taratibu na Sheria za nchi yetu katika kuwasilisha hoja zao, iIi kuendelea kudumisha amani ya nchi yetu.
Kapt. (Mst) George H. Mkuchika (Mb) WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO
11 Mei,2009

Fingigwe
05-12-2009, 05:21 PM
Shukran Mkuu kwa swali lako maridhawa.

Hapa inabidi tuikumbushe tu serikali kuwa inapaswa kuwa SERIKALI. Kauli ya Mh. Mkuchika inazidi kudhihirisha udhaifu wa Serikali. Hatutegemei watu (binafsi) wakivunja sheria basi serikali "itoe tamko". Mengi na Rostam ni akina nani? Kama Serikali inaamini mdahalo wao una vielelezo vya jinai basi hatua zichukuliwe! Eti serikali inatoa tamko? Hawa wana dhamana gani nzito ya kisiasa katika nchi hii? What's going on?

Halafu, ukweli usemwe; kwanza, suala la kutumia vibaya vyombo vinavyomilikiwa na "mapapa na manyangumi" hao halipo wala halikuwepo. Kikao alichoitisha Mengi kutangaza mafisadi papa, ndiyo ilikuwa habari namba 1 kwenye taarifa ya habari ya TBC1 ya saa 2 usiku wa siku hiyo. Aidha, karibia vyombo vyote viliichangamkia na vimeendelea kuchangamkia habari hiyo. Kwa Mh. Rostam, vivyo hivyo. Vyombo vyote vina access na kauli za malodi hawa - hakujawa na exclusivity kwa vyombo vyao tu.

Kama ni msimamo wa vyombo vya habari kumponda nani na kumpandisha chati nani hilo ni suala la kawaida: kwa kifupi tu soma Uhuru au Habari Leo uone mlengo ukoje kwa akina Slaa and Co. Aidha, angalia ITV na/au soma Nipashe n.k. uone hisia kwa akina Manji, Masha na wenzao zikoje. Usiishie hapo tu pitia pia media za CNN na Fox News uone wanavyowapima Republicans na Democrats huko Marekani. Serikali isijidanganye, kamwe vyombo vya habari havitakosa mwegemeo. Cha maana ni je, kuna jinai? Basi chukua hatua; usiishie kutoa kauli kama kuku aliyelowa.

Pili, hivi ni kweli kwamba wananchi tumegawanyika kwa mada zinazotolewa na hawa wakulu? Serikali iseme ukweli au iendelee kula kobis. Kama ni kugawanyika, kinachotugawa ni utawala mbovu unaojenga na kuimarisha matabaka ya mabwana na watwana nchini. Huu mdahalo wa akina Mengi na Rostam ni kibwagizo tu katika hili. Hata ukiisha, mpasuko huo utaendelea kama Serikali haitaamua kwa dhati kuachana na uswahili na kufanya kazi yake na, zaidi ya yote, kuwaaminisha Watanzania kuwa iko makini.

Ninachokiona ni kwamba homa iko katika ufa unaojitokeza ndani ya Chama tawala (hawa wote ni makada wa CCM). Mgongano ulipokuwa kati ya "Chama" na wapinzani, mambo yalikuwa rahisi; sasa hoja zilezile zimekuwa agenda rasmi ndani ya Chama basi inshakuwa taabu. Watanzania wa kawaida wana dhiki na adha nyingi sana wanazokabiliana nazo kiasi kwamba hayo malumbano hayamo kabisa katika vipaumbele vyao. Labda kwetu sisi wachache sana tunaojidai wachambuzi wa mambo.

Kwa kifupi, serikali ifanye kazi yake; iache kutia huruma kwa kuwaogopa Watanzania wenzetu sijui wenye mapembe au kwato?

mwanakijiji
05-12-2009, 07:34 PM
umesema kweli kabisa.. lakini nafikiri serikali inaonekana kutumia nguvu sana kulazimisha hoja dhaifu!