mwanakijiji
05-15-2009, 02:55 AM
Rais Mkapa aliwahutubia wananchi katika mwaka mpya 2005, Januari 31. Hotuba ile ningeipa jina la "Uaminifu na maadili ya Taifa" ilinivutia wakati ule na niliipenda. Ukweli wake bado ni kweli hata leo hii. Kama ingetolewa na mtu mwingine basi bila ya shaka ingekuwa ni mojawapo ya hotuba zenye kugusa fikra na hisia za watu kwa mantiki yake, hoja zake na mahitimisho yake... Jisomee mwenyewe:(msisitizo ni wangu)
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM
MKAPA, KWA WANANCHI, 31 JANUARI 2005
Ndugu Wananchi,
Katika salamu zangu za mwaka huu mpya kwenu, pamoja na mambo mengine, nilijenga hoja kuwa wakati umefika Watanzania tuweke mkazo mpya, na umuhimu unaostahili, kwenye maadili ya kitaifa. Maadili ya kitaifa, yanayotutambulisha kama Watanzania, yanayotupa sifa ya U-Tanzania, ni ya aina nyingi. Mwezi uliopita nilizungumzia zaidi maadili ya kisiasa na kiutawala, nikawalaumu zaidi viongozi wa kisiasa na kiutawala kwa dalili za mmomonyoko wa maadili yetu ya asili. Nilikuombeni, Ndugu Wananchi, mniunge mkono kuwakatalia viongozi wa kisiasa, kidini na kiutawala ambao, kwa kauli zao au vitendo vyao, wanachangia kumomonyoa sifa za U-Tanzania, ikiwemo maadili ya uhuru, umoja, amani, utulivu, upendo, kuvumiliana na mshikamano. Nilikuombeni tusaidiane kuwaambia HAPANA viongozi wanaotuletea mambo ya udini, ukabila, umajimbo, ubaguzi, visasi, chuki na fujo, maana mambo hayo kwa hakika ni kinyume kabisa cha U-Tanzania wetu.
Leo nitaelekeza maneno yangu kwa wale wananchi wenzetu wachache ambao, kwa tabia na mienendo yao, nao wanahatarisha sifa za kijamii za Watanzania, ambazo nazo ni sehemu muhimu ya U-Tanzania wetu sote. Na leo nitazungumzia sifa moja tu ya maadili ya UAMINIFU. Maana, huko tulikotoka, Watanzania kwa ujumla tulisifika kwa uaminifu, hasa tukilinganishwa na mataifa mengine barani Afrika. Ingetazamiwa wengine wajifunze uaminifu kutoka kwetu. Lakini naona wapo baadhi ya Watanzania ambao sasa wanataka kutufikisha mahali ambapo na sisi tutaonekana hatuna tofauti na hao wengine.
Ukweli ni kuwa sifa ya U-Tanzania si sifa itokanayo na maadili ya kisiasa na kiutawala peke yake; ni sifa itokanayo pia na tabia za raia, na maadili mengine ya kijamii, ikiwemo uaminifu. Kamusi ya Kiswahili Sanifu inaeleza kuwa Uaminifu ni ?tabia ya mtu kuweza kuaminika, kama vile mtu kupewa amana za watu aziweke mpaka watakapokuja kuzitaka.?
Ndugu Wananchi,
Katika miaka ya 1970 na 1980, nchi yetu iliwekeza sana mikopo, misaada, rasilimali, amana na akiba za taifa letu katika mashirika ya umma. Zipo sababu nyingi zilizofanya mashirika hayo yadhoofu kiutendaji, na hatimaye mengi kufa kabisa. Lakini mojawapo ya sababu hizo ni kukosa uaminifu kwa baadhi ya wenzetu tuliowakabidhi kazi ya kusimamia na kuendesha mashirika hayo, yaani wenzetu tuliowakabidhi amana za taifa letu. Kweli, wengine walikuwa na elimu au ujuzi usiotosha, na pengine mazingira ya kibiashara na kiutawala wakati huo hayakuwa mazuri sana. Lakini, kwa baadhi yao, ukosefu wa uaminifu nao ulikuwa mojawapo ya sababu ya kudhoofika na hatimaye kufa kwa mashirika ya umma.
Hayo yalikuwa mashirika ya umma, na yalipokufa waliopata hasara kwa kweli ni ninyi wananchi. Leo uchumi wetu, siku hadi siku, unazidi kuwa wa soko, na hivyo unakuwa uchumi wa ushindani. Ni uchumi utokanao na uwekezaji wa sekta binafsi, wa amana za watu binafsi. Serikali haiwekezi tena kwenye viwanda, huduma za kibiashara, makampuni, mabenki na asasi za fedha. Wanaowekeza amana zao katika nchi yetu ni watu au makampuni binafsi, ya ndani na ya nje ya nchi. Hawa, kwanza hawawezi kukubali kupata hasara kama ile ambayo Watanzania waliipata kutokana na mashirika ya umma. Na pili, wanafanya kazi katika mazingira ya ushindani, ndani na nje ya nchi, ambapo sifa ya uaminifu ni kivutio kwa anayetaka kujenga mahusiano ya kibiashara ya muda mrefu. Tujiulize Watanzania: Je, bado tunayo sifa ya uaminifu ya kutosha kuvutia amana za wawekezaji?
Zipo nchi hapa barani Afrika ambapo hata raia wa nchi hizo wanaweka amana zao, na rasilimali zao, nje ya nchi hizo kwa vile tu hawaziamini asasi zilizopo nchini mwao, au kwa vile hawawaamini wananchi wenzao. Katika mazingira hayo inakuwa vigumu kuwavutia wawekezaji kutoka nje, isipokuwa kwa maeneo ambayo wawekezaji hao hawana hiari ya kuwekeza kwingine. Na pale inapobidi wawekeze, basi watatafuta faida kubwa mno ili kujihami pindi wakiibiwa au kupata hasara; na pengine, kwenye nyadhifa fulani fulani, watang?ang?ania kuajiri watu kutoka nje ya nchi inayohusika. Kisa? Hawawaamini raia wa nchi wanamowekeza amana zao na rasilimali zao.
Ndugu Wananchi,
Katika soko huru la uwekezaji, biashara na ajira, mwekezaji anazingatia mambo mengi anapoamua amuajiri nani kati ya raia wa nchi anamowekeza, au anapofanya uamuzi wa ama kuajiri kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi. Elimu ni sifa muhimu. Ujuzi ni sifa muhimu. Mtazamo ni sifa muhimu. Bidii ya kazi nayo ni sifa muhimu. Lakini zaidi sana uaminifu ni kigezo muhimu. Na sifa ya uaminifu ni kama maji, ambayo yakimwagika, hayazoleki.
Asiye na elimu ya kutosha anaweza kusomeshwa akapata elimu na ujuzi. Asiye na mtazamo sahihi anaweza kupelekwa semina, akapigwa msasa, na kisha kubadilika. Asiye na bidii naye anaweza kubadilika na ikaonekana dhahiri kuwa huyu sasa ana bidii ya kazi. Lakini mtu akishakosa uaminifu, akawa bazazi, haaminiki tena. Hata wewe mwananchi unayenisikiliza unajua kuwa mtu akishakuibia mara moja, na hata akitubu na ukamsamehe, ni vigumu kumuamini tena kwa asilimia mia moja. Maana uaminifu, tofauti na elimu au bidii ya kazi, mizizi yake imo ndani ya nyoyo za wanadamu. Haiwezekani kujua kilicho moyoni mwa mwanadamu. Hivyo, japo kidogo, utakuwa na shaka kuwa siku moja mtu huyo anaweza kushawishiwa tena akakosa uaminifu.
Zamani nilikuwa nafarijika nikisikia kuwa Tanzania inaitwa ?Bongoland?. Nilidhani kuwa ilimaanisha Watanzania wameamua kutumia bongo zao kwa mambo ya ubunifu wa mikakati ya maendeleo na ujasiriamali. Leo nilichodhani faraja kimegeuka karaha. Maana bongo inayozungumzwa si ya kutafuta maendeleo, au kupanua ujasiriamali, bali ni ujanja-ujanja, ubazazi, udanganyifu, ulaghai, na kutafuta mali bila kazi. Na ugonjwa huu umezidi sana mijini ambapo ukimwamini mtu, kisha akakuingiza hasara, unaambiwa eti ?utajiju!?, au ?utalijua jiji.? Ni kama vile badala ya kuionea haya hali hii ya mmomonyoko wa uaminifu, tunaitukuza.
Ndugu Wananchi,
Nayasema haya kwa vile siku hadi siku nasikia, kama bila shaka nanyi mnavyosikia, vitendo vya Watanzania wenzetu wachache walioajiriwa katika makampuni, mabenki, asasi za fedha, migodi ya madini na kadhalika wakituhumiwa au kupatikana na hatia ya wizi, ujambazi na udanganyifu, ikiwemo kwa kushirikiana na raia wa nchi nyingine zenye raia waliokubuhu kwenye mbinu za wizi na ujambazi. Badala ya kuwa funzo na mfano wa uaminifu kwa wengine, sisi sasa tunakuwa wanafunzi wa uhalifu, ubazazi na kukosa uaminifu.
Ndugu Wananchi, ninatoa tahadhari. Tuwe macho tusije tukafika mahali zikawepo kazi ambazo nikiuliza wawekezaji kwa nini hawaajiri Watanzania watanijibu kuwa: Rais, watu wako wana elimu, wana ujuzi, lakini si waaminifu. Na sote tunajua kuwa si kweli, katika hali halisi, kuwa samaki mmoja akioza wote kweli wameoza; lakini kwa bahati mbaya hivyo ndivyo binadamu tunavyohisi. Akishaoza mmoja hatuwaamini waliosalia. Hivyo kwa wachache wetu kukosa uaminifu, tutajikuta sote hatuaminiki tena. Na siwezi kuwalaumu wawekezaji watakaosita kuwaamini Watanzania iwapo sisi wenyewe tutajijengea sifa ya kukosa uaminifu, au tutawahifadhi na kuwaonea haya wanaoharibu sifa ya uaminifu wa Watanzania.
Ndugu Wananchi,
Tumeanza mwaka mpya. Sijui kila mmoja wetu ameazimia nini kwa mwaka huu. Lakini naomba mwaka huu kila mmoja wetu awe makini zaidi kulinda sifa ya uaminifu ambayo, tukilinganishwa na wengine, tulionekana tunayo kwa asili yetu, kwa miaka mingi. Maadili ya Kitanzania tunayoyataka yawe pia maadili ya uaminifu katika maisha yetu binafsi, na katika sehemu zetu za kazi. Tusiwafikishe wawekezaji, wa ndani na wa nje, mahali ambapo watasema kazi hii siwezi kumpa Mtanzania maana Mtanzania haaminiki.
Mtanzania afanyaye kazi benki, akiiba, hajikoseshi yeye tu sifa ya kuajiriwa, anawapaka matope wafanyakazi wenzake Watanzania na kuwafanya nao watiliwe mashaka. Na vivyo hivyo katika sehemu zote za ajira. Na tukiendelea kuwafumbia macho, au kuwaonea haya, hatimaye sisi sote na vizazi vyetu vijavyo tutaonekana mababazi, watu wasioaminika, na hivyo kukosa ajira. Na kama Watanzania hao ni wawekezaji au wafanyabiashara, basi watakosa wabia. Ni kweli waajiri wana wajibu wa kuchuja vizuri wanaoomba kazi, na pia wana wajibu usiokwepeka wa kuwa na taratibu na mifumo bora zaidi ya ulinzi. Lakini nasi Watanzania, kwa ajili ya kulinda U-Tanzania wetu, tunao wajibu wa kuwa waaminifu na kukataa kutumiwa kwa malengo ya kihalifu.
Ndugu Wananchi,
Mtu anayekosa uaminifu sehemu ya kazi ni wa kusutwa, si wa kusifiwa; ni wa kufichuliwa si wa kufichwa. Na uhalali wa raia wema kufanya hivyo ni kuwa tabia za watu hao hazikubaliki, maana huo si U-Tanzania.
Siku chache zilizopita, wakati akifungua tawi mojawapo la Benki ya Stanbic jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha, Mhe. Basil P. Mramba, Mb., alilaani vikali hii tabia inayoenea sasa ya wizi kwenye benki nchini ambapo baadhi ya watuhumiwa ni waajiriwa wa benki zinazohusika.
Hivi sasa zipo kesi kadhaa mahakamani kuhusiana na wizi, ikiwemo ujambazi, katika baadhi ya benki zilizopo nchini. Tuna imani na mahakama zetu kuwa hatimaye maamuzi yao yatakuwa ya haki, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Lakini, narudia. Tuchunge sana sifa ya uaminifu wa Watanzania. Vyovyote vile mahakama zitakavyoamua, tuhuma za wizi na ujambazi unaohusisha waajiriwa zinaharibu sifa ya nchi yetu kama mahali pa uwekezaji, na hasa zinaharibu sifa ya Watanzania kama watu wa kuaminiwa sehemu ya kazi. Hasara ya kukosa sifa hiyo ni kwa Watanzania wote. Hivyo, kila raia mwema lazima alaani na kupinga tabia hiyo.
Ndugu Wananchi,
Namalizia kwa kuzidi kusihi kuwa tuchukulie sifa ya uaminifu kuwa ni kigezo muhimu sana cha U-Tanzania wetu. Na kwa wale waliokosa uaminifu ? iwe hao wanaotuhumiwa kushiriki kuiba kwenye mabenki, au wanaoiba fedha za Serikali, na wabadhirifu wengine wote, tuwaambie HAPANA, huo si U-Tanzania. Tukiwa wazazi, marafiki au wake na waume, kamwe tusikubali kupokea zawadi na mapato yatokanayo na ukosefu wa uaminifu. Nawaomba viongozi wa dini nao wasaidie kukataa tabia hii inayojipenyeza katika nchi yetu. Tunapiga kelele sana kuhusu rushwa. Lazima tuendelee kuikataa na kuipiga vita rushwa. Lakini, wakati umefika pia wa kuipigia kelele, na kuikataa, tabia hii ya kukosa uaminifu ambayo ni miongoni mwa nguzo kubwa za rushwa. Kwa pamoja tujenge na kulinda uaminifu kama sura na sehemu muhimu sana ya U-Tanzania wetu. Na tusisahau. Maadili ya Kitanzania, na sifa ya U-Tanzania, ni jukumu la kila raia, kwa kushirikiana na Serikali. Inawezekana. Timiza wajibu wako.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
My Take:
Wazo atakuwa amelipata wapi? Kwenye kitabu cha "We must run, while they walk" Nyerere ananukuliwa kusema hivi katika majibu yake ya mwaka 1962 Bungeni katika mjadala wa Katiba mpya "the ultimate safeguard of the people's freedom is the ethic of the nation." What was needed he said, was a national ethic that enabled the government to say, "We can not do this, this is un-Tanganyikan" and the people to say, "that we cannot tolerate, that is un-Tanganyikan". Without such an ethic, said Nyerere, "no constitution , however framed, could insure that the people would not become victims of tyranny."
Kwanza najiuliza, hotuba ya Mkapa resemble very much hiyo ya Nyerere. Tunaweza kuweka katika level ya plagiarism?
Pili, what is wrong with the premise of the speech?