PDA

View Full Version : Mtanzania aliyebadili jinsia: Mawazo yako..



mwanakijiji
05-20-2009, 07:00 PM
NA JOSEPH BURRA

UMATI ulifurika jana katika hospitali ya Mwananyamala, mjini Dar es Salaam kumwona mgonjwa aliyefikishwa hospitalini hapo anayesadikiwa kubadili jinsia kutoka ya kiume kuwa ya kike.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya hospitali hiyo, mgonjwa huyo alifikishwa hapo saa 11.00 alfajiri ya jana akiwa hajitambui, baada ya kuokotwa na polisi maeneo ya Mbezi Beach.

Chanzo cha habari kilisema iliwawia vigumu wauguzi kutokana na mgonjwa huyo, ambaye kimtazamo anaonekana mwanaume lakini alitambulishwa kwa jina la mwanamke.

"Alipokaguliwa alikuwa na jinsia ya kike iliyoonekana ni ya bandia, aliyowekewa kwa njia ya operesheni kwa sababu kuna mishono ya nyuzi kwenye sehemu za siri,? kilidai chanzo hicho cha habari na kuongeza kuwa alikuwa amevaa hereni.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari, baada ya ukaguzi huo, mgonjwa huyo alipelekwa wodi namba tatu ambayo ni ya wanawake.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Suleiman Mtani, akizungumza na Uhuru hospitalini hapo alikiri mgonjwa huyo kulazwa katika wodi ya kinamama.

Alisema kimaadili kazi yao ni kuhudumia wagonjwa bila kujali jinsia wala historia ya maisha yao.

"Ni kweli tuna mgonjwa wa aina hiyo aliyeletwa na polisi alfajiri ya leo lakini hatuwezi kuwaruhusu mkamwone kwa kuwa hajielewi na kimaadili kazi yetu ni kumtibu mgonjwa apone na aendelee na shughuli zake, hatujali alikuwa jambazi, shoga au mwizi, sisi tunatibu mengine ni yake," alisema Dk. Mtani.

Aliongeza: "Kwa sasa hajielewi sisi ndio tunatunza siri zake mpaka apate fahamu na kama mtataka kuzungumza naye kwa ridhaa yake akikubali mtazungumza naye lakini leo hatutawaruhusu.

?Kwa kuwa huyu aliletwa na polisi ili atibiwe ni vyema mkaulize habari zake polisi watawaeleza ni wapi walimkuta na mazingira waliyomkuta? watawapeni maelezo kamili".

Kutokana na hilo, uongozi wa hospitali ulilazimika kubandika tangazo kuzuia watu kuingia ndani ya wodi hiyo.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kawe, Hendry Mwaibambe, alisema kwa mujibu wa taarifa walizonazo mtu huyo anadaiwa kuwa shoga.

Alisema jana alfajiri aliokotwa eneo la Mbezi Beach akiwa hana fahamu na kuamua kumpeleka Mwananyamala ili akatibiwe.

Kwa mujibu wa Mwaibambe, shoga huyo (jina linahifadhiwa) ni mkazi wa Kawe, ambaye aliuza nyumba yake ili akabadilishe jinsia nchini Thailand, ili apate soko ambalo hakupata.

Kamanda Mwaibambe alisema kutokana na hilo, alichanganyikiwa na inasadikiwa alikunywa sumu ili ajiue.

mwanakijiji
05-20-2009, 07:10 PM
Nasikia huyo mgonjwa kafariki jamani. Mungu ampumzishe kwa amani.

Daywell
05-20-2009, 09:02 PM
kama kafariki amepata haki yake mwache atangulie mbele za haki huenda mwisho wke ungekuwa mbaya zaidi kwani kuna habari kuwa kuna kikundi kilikuwa kinajiandaa kumfanyizia tena!

Mpita Njia
05-21-2009, 09:43 AM
Nasikia huyo mgonjwa kafariki jamani. Mungu ampumzishe kwa amani.

Ni kweli, niemsoma kwenye magazeti yaleo kuwa kafariki
Mungu amrehemu

mnyilula
05-21-2009, 11:53 AM
Ni kweli, niemsoma kwenye magazeti yaleo kuwa kafariki
Mungu amrehemu


Aliyebadili jinsia afariki dunia



na Asha Bani




MGONJWA aliyebadili jinsia na kuwa ya kike, Victoria Armu ?Aluu?, amefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Habari cha kuaminika kutoka chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo, zinaeleza kuwa Victoria alifariki dunia jana asubuhi baada ya kuzidiwa ghafla. Hata hivyo hakuna aliyekuwa tayari kueleza ugonjwa uliosababisha kifo chake.

?Ni kweli mgonjwa huyo amefariki leo (jana) asubuhi kutokana na hali yake kuwa mbaya baada ya kuhamishiwa hapa akitokea Hospitali ya Mwananyamala,? kilisema chanzo chetu cha habari.

Victoria alikuwa akitibiwa chini ya ulinzi mkali wa askari na inaelezwa kuwa hakuna ndugu yake hata mmoja aliyejitokeza kuamjulia hali alipokuwa akiugua kutokana na utata wa jinsia yake.

Inaelezwa kuwa, baada ya kufariki, ndugu mmoja wa marehemu huyo alijitokeza na kujitambulisha ingawa Tanzania Daima haikufanikiwa kupata jina lake.

Aidha, Tanzania Daima ilipofika chumba cha maiti katika hospitali hiyo, ilikuta watu wengi kila mmoja akiwa na shauku ya kuona maiti ya mtu huyo.

Hata hivyo, watu hao walishindwa kuiona kutokana na kuhifadhiwa kwenye jokofu la kuhifadhia maiti na kufungwa na kufuli tofauti na jinsi zinavyohifadhiwa maiti nyingine.

Juzi, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa, Victoria aliwahi kupata watoto wawili wakati akiwa na jinsia ya kiume, alipokuwa akiishi Kimara, Dar es Salaam kabla ya kuuza nyumba yake na kisha kwenda kubadili jinsia nchini India ambako aliwekewa viungo bandia vya kike.

Victoria, amefariki akiwa ana umri wa miaka 50 na kabla ya kukutwa na ugonjwa uliosababisha kifo chake, alikuwa akiishi na mzungu mmoja katika eneo la Mbezi Beach kama mumewe.

Mwishoni mwa wiki, Victoria aliokotwa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Mbezi akiwa hajitambui na kudaiwa kuwa alikuwa amebakwa.

Akajase
05-22-2009, 06:50 PM
Nasikia huyo mgonjwa kafariki jamani. Mungu ampumzishe kwa amani.

Mkuu, ni vigumu sana kupumzishwa kwa AMANI na Mungu huyu tunayesoma habari zake katika vitabu kama muhusika hajafanya TOBA YA KWELI.
Hebu angalia alivyofanya:-
[1] Alikuwa shoga.... ufiraji na ufirwaji Mungu anachikua
[2] Akaamua kujibadilisha jinsi ..... Mungu aliyemuumba mwanamume alikuwa amekosea ila yeye ndiyo yuko sahihi sana.
[3] Akaanza kuishi na mwanamume (libeneneke la ufirwaji na kuingiliwa katika uke-bandia likaendelea)..... ndoa hii nayo ni halali machoni pake Mola Mwenye enzi?
[4] "Akaamua kujiua" baada kuona nini hatujui......... Kuua ni dhambi mbele zake mungu mwenye enzi yote.

Mungu hadhihakiwi,apandacho mtu ndicho atakachovuna.