View Full Version : Mambo ya "ze utamu"
mwanakijiji
11-13-2008, 09:14 AM
Hivi unachukuliaje tabia ya baadhi ya vyombo vinavyojulikana kama "vya udaku" kutoa picha za watu ambao siyo "public figures" na kuelezea mambo yao ya binafsi? Je vinasaidia kupigana na tabia chafu katika jamii, je zinaingilia uhuru wa watu wengine, au ni haki ya mtu kulinda mambo yake mwenyewe?
Katika jamii kama ya kwetu na hasa penye teknolojia mpya ya mtandao ni kwa kiasi gani watu watarajie ulinzi wa mambo yao binafsi? Je kuna lolote mtu anaweza kufanya kujilinda na kuchafuana hasa kwa kutumia mtandao?
anonymous
11-13-2008, 10:18 AM

Actually sifikiri kama ni jambo la busara kufanya mambo ya namna hii yasiyo na msingi na isitoshe si utamaduni wetu.
Cha kushangaza hakuna jambo jipya walifanyalo wahusika kwani ngono ilikuwepo tangu enzi hizooo hatujazaliwa.
Ila ni kuwa tu sasa hivi katika sayansi na teknolojia hii kuna MACAMERA na vitu kama hivyo, basi waliokosa kazi ndio wanaona dili kuwaharibia watu STAREHE zao.
Huu mtindo umepitwa na wakati na sema tu kwenye nchi zetu hatuna sheria nzuri.
THE UTAMU ungekuta ananyea ndoo na si hivyo tu bali nafikiri hata hali yake ingekuwa mbaya sana.
mwanakijiji
11-13-2008, 04:46 PM
Wapo watu ambao wanaamini kuwa the utamu na site kama hizo zimechangia kuwaumbua mafisadi wa ngono na hivyo kuokoa ndoa au mahusiano yao na kuwarudisha kwenye mstari mzuri.
Na wapo wale ambao wanaona kama ni burudani ya aina fulani kusoma na kufuatilia maisha ya watu fulani ambao ni maarufu au wana ujiko wa aina fulani.
anonymous
11-13-2008, 05:18 PM

Sifikiri kama ile THE UTAMU ilikuwa pilipili ya mafisadi wa ngono. Kwani ukiangalia number ya watu wanaotolewa pale na ni watu wangapi wanaofanya ufisadi wa ngono basi nafikiri ni ratio ya 1:3,000,000
Kwani hata kama mtu hafanyi ufisadi huo ila tu camera imemkuta au amesahau picha zake sehemu then mwendawazimu mmoja akaipata then akaituma kwa kichaa the utamu. Je, na huyu naye ni fisadi wa ngono jamani??
Kwa kweli ni vizuri ile blog imefutwa kwani haikuwa na maana yoyote.
Mpenda amani
11-14-2008, 11:46 AM
Kwa kweli ni vizuri ile blog imefutwa kwani haikuwa na maana yoyote.
Mhh, utamu bwana ina faida na hasara zake. Kama waendeshaji wangekuwa ni watenda haki, nikiwa na maana ya kuwaweka wale tu ambao wana uhakika kuwa ni mafisadi wa ngono na wanatuharibia vi-binti vyetu then ingekuwa sahihi. lakini tabia ya kuweka kila picha wanayoipata bila ya kuwa na uhakika kama ni kweli mafisadi wa ngono au wamekuwa victims tu ndio mbaya, na ndio imeharibu maana nzima ya ile blog..
Pia blog imerudi, sasa hivi wanatumia .com.
Mpita Njia
11-15-2008, 12:25 PM
Hiyo blog is a disgrace, sidhani hata kama inastahili kujadiliwa humu
mwanakijiji
11-16-2008, 12:52 AM
Mpita Njia... unaona wanachofanya ndivyo kinafanywa na uwazi sasa tena hadharani.. angalia habari hii ya Uwazi:
Tayari wabunge wanne wamenaswa na gazeti hili katika skendo hizo, zikiwemo kuzaa nje ya ndoa na kugoma kutoa msaada kwa mabinti waliowajaza mimba, kugonganisha mademu na wengine kuchanganya mtu na dadake.
http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1226729728_2web.jpg
http://www.globalpublisherstz.com/uploads/posts/thumbs/1226729728_3web.jpg
Aliyefungua dimba katika kupata skendo, alikuwa mbunge wa zamani wa jimbo moja lililopo mjini Zanzibar ambaye alifahamika kwa jina la Mohamed Ali, huyo alizaa na msichana mmoja nje ya ndoa na ikawa mbinde katika kutoa matunzo hadi alipopelekwa mahakamani.
Alipoulizwa na waandishi wetu, Mohamed Ali, alikiri kuzaa na binti huyo huku akidai kuwa, yeye ni Muislamu na rijali, hivyo kuwa na mwanamke au kuzaa nje ya ndoa si ?ishu? kubwa kwake.
Wa pili alikuwa Mbunge wa Mufindi Kusini, Benito
Malangalila, huyu alidaiwa kugombewa na wanasichana wawili hadi kufikishana katika Kituo cha Polisi Kawe, jijini Dar es Salaam.
Katika valangati hilo la kugombewa na mabinti, mmoja wa mabinti hao alidai kuwa mheshimiwa huyo ni wake, alipoteza simu yake ya mkononi, jambo lililomfanya mbunge huyo kuhaha madukani kutafuta simu nyingine ili aweze kufidia iliyopotea.
Waandishi wetu walifanikiwa kumpiga picha mbunge huyo akiwa na wapambe wake wakitafuta simu katika maduka yaliyopo eneo la Shule ya Uhuru, jijini Dar es Salaam, (tazama picha ukurasa wa mbele).
Alipoulizwa na Mwandishi Wetu kuhusu madai ya kugombaniwa, Mheshimiwa Malangalila, huku akirekodiwa na kinasa sauti, alikiri kuwafahamu mademu wote hao na kusema kuwa, soo hilo alishalimaliza.
Mheshimiwa aliyefuata, alikuwa Mbunge kutoka Jimbo moja la Pemba
(jina tunalihifadhi kwa vile alilia sana tukaamua kumsamehe), huyo alitongoza msichana wa miaka 16, eneo la Karikaoo jijini Dar es salaam, baada ya kuona anazungushwa akaamua kubadilisha ?gia? na kuanza kumzengea dada wa msichana huyo.
Kuona hivyo, binti huyo mdogo aliamua kumjulisha dada yake na baadaye kuifahamisha timu ya waandishi wetu ambapo waliweka mtego na kufanikisha kumnasa mbunge huyo katika Hoteli maarufu ya Harare Inn, iliyopo Karikaoo, jijini Dar es Salaam.
Mwingine mwenye skendo la ngono alikuwa mbunge mmoja maarufu sana, ambaye jina lake linaanza na herufi S. Mheshimiwa huyo alitelekeza familia yake na kuhamia kwa hawara yake eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Mtoto wake mkubwa ndiye aliyefichua siri hiyo, jambo lililofanya waandishi wetu kwenda katika chumba cha msichana huyo ambapo majirani walikiri kuwa, mheshimiwa huyo kahamia katika maskani ya myange huyo.
Awali, Waaandishi wetu walipompigia simu, mbunge huyo, alikanusha vikali lakini baadaye alijirudi na kusema kuwa anaomba asiandikwe na kwamba angejirekebisha.
Aidha, mbunge huyo alidai kuwa mtoto wake huyo wa kiume aliyefichua soo hiyo ana matatizo ya akili baada ya kukubuhu katika kubwia unga.
?Huyo mtoto ana matatizo, msimwamini hata kidogo,? alisema mbunge huyo kabla ya kuomba msamaha,
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mbunge huyo amejirekebisha na anatoa huduma kwa familia yake jinsi ipasavyo.
Hata hivyo, lengo la kuandika habari hii si kuwachafua waheshimiwa hao, bali ni kutoa tahadhari kuwa hakuna mtu atakayesamehewa atakaponaswa na timu yetu akifanya mambo ya ovyo!.
Mpita Njia
11-27-2008, 07:05 PM
Nashukuru sina munkari wa kusoma magazeti haya
My more
11-30-2008, 12:53 AM
Nashukuru sina munkari wa kusoma magazeti haya
Mpita njia Bongo hii matope kila sehemu, utarukaaa badae utayakanyaga na kuyazoea maana kila mahali ni tope tu. Sasa sijui tuwe tunafunga macho????
makange
12-01-2008, 04:57 PM
Na naona theutamu amerudi hewani tena.
Mpita Njia
12-01-2008, 06:58 PM
Na naona theutamu amerudi hewani tena.
Nawashauri ndugu zangu msiende huko, mnawapa sifa za bure
makange
12-02-2008, 07:58 AM
Nawashauri ndugu zangu msiende huko, mnawapa sifa za bure
Ni kweli Mheshimiwa!!!!
Na naona theutamu amerudi hewani tena.
umesoma ushauri wa Mwenyeji wa Njia??:D:D
makange
12-03-2008, 05:22 PM
umesoma ushauri wa Mwenyeji wa Njia??:D:D
Ambao ni??:confused:
Hivi unachukuliaje tabia ya baadhi ya vyombo vinavyojulikana kama "vya udaku" kutoa picha za watu ambao siyo "public figures" na kuelezea mambo yao ya binafsi? Je vinasaidia kupigana na tabia chafu katika jamii, je zinaingilia uhuru wa watu wengine, au ni haki ya mtu kulinda mambo yake mwenyewe?
Katika jamii kama ya kwetu na hasa penye teknolojia mpya ya mtandao ni kwa kiasi gani watu watarajie ulinzi wa mambo yao binafsi? Je kuna lolote mtu anaweza kufanya kujilinda na kuchafuana hasa kwa kutumia mtandao?
Mwanakijiji, sasa inabidi ufahamu kwamba umeingia kwenye mtandao ama utandawazi. Si jambo zuri wala busara watu kuongea mambo binafsi ya watu wengine na hasa mengi ambayo tunayaona kwenye hiyo ze-utamu. Lakini tukiangalia sana tunakutana na neno demokrasia .. kwamba katika kutoa na kupata habari kila mtu ana "uhuru" wa kutoa ama kupata habari hapo ze utamu ana "sail smoothly" anao uhuru huo kama mwananchi mwingine yeyote yule.
La muhimu hapa la kuongea ni lile swala la "National ICT Policy" ambayo itajenga muelekezo wa yepi yafanywe kama nchi yenye demokrasia ya utoaji na upashaji habari na yepi yasifanye!! Na vile vile ndani ya Policy hii kutajwe ama kufahamishe umma wapi mtu anaweza kulalamika kisheria na kusikilizwa iwapo anaona kwamba hakutendewa haki kwenye technologia ya mawasiliano kama hii.
Hili ni swala zito ambalo litahitaji watu wengi kuchangia toka kwenye taaluma za mambo ya mawasiliano na wanasheria pamoja na wadau wote nchini. Haya si mageni tayari nchi za dunia ya kwanza zina mambo kama haya na hata marekani FBI wana kitengo maalum ambacho mtu anapeleka malalamiko yake kwenye chombo hiki cha sheria kama anaona hakutendewa haki ama kwenye barua pepe, nk.
Mazingira ambayo yahahitajika ni pamoja kuwa na "Law enforcers" wenye ujuzi wa mambo ya Information Forensic na wakawa na uwezo wa kupeleka vigezo vya ushahidi mahakamani kwa jinsi ambavyo vitakubaliwa kwamba ni vigezo vya ushahidi kamili kumchukulia mtu hatua za kisheria.
Bado tuna kazi kubwa kidogo lakini huu sasa ndiyo mwanzo na tutafika na mengine yote haya yatakuwa historia ama kumbukumbu ya tulikotoka.
Karibu kwenye technologia Mwanakijiji:)
My more
12-03-2008, 06:47 PM
...Ambao ni ...
Nawashauri ndugu zangu msiende huko, mnawapa sifa za bure
Mwanakijiji, sasa inabidi ufahamu kwamba umeingia kwenye mtandao ama utandawazi. Si jambo zuri wala busara watu kuongea mambo binafsi ya watu wengine na hasa mengi ambayo tunayaona kwenye hiyo ze-utamu. Lakini tukiangalia sana tunakutana na neno demokrasia .. kwamba katika kutoa na kupata habari kila mtu ana "uhuru" wa kutoa ama kupata habari hapo ze utamu ana "sail smoothly" anao uhuru huo kama mwananchi mwingine yeyote yule.
La muhimi hapa la kuongea ni lile swala na "National ICT Policy" ambayo itajenga muelekezo ya yepi yafanywe kama nchi ya demokrasia na yepi yasifanye!! Na vile vile ndani ya Policy hii kutajwe ama kufahamishe umma wapi mtu anaweza kulalamika kisheria na kusikilizwa iwapo anaona kwamba hakutendewa haki.
Hili ni swala zito ambalo litahitaji watu wengi kuchangia toka kwenye taaluma za mambo ya mawasiliano na wanasheria pamoja na wadau wote nchini. Haya si mageni tayari nchi za dunia ya kwanza zina mambo kama haya na hata marekani FBI wana kitengo maalum ambacho mtu anapeleka malalamiko yake kwenye chombo hiki cha sheria.
Mazingira ambayo yahahitajika ni pamoja kuwa na "Law enforcers" wenye ujuzi wa mambo ya Information Forensic na wakawa na uwezo wa kupeleka vigezo vya ushahidi mahakamani kwa jinsi ambavyo vitakubaliwa kwamba ni vigezo vya ushahidi kamili kumchukulia mtu hatua za kisheria.
Bado tuna kazi kubwa kidogo lakini huu sasa ndiyo mwanzo na tutafika na mengine yote haya yatakuwa historia ama kumbukumbu ya tulikotoka.
Karibu kwenye technologia Mwanakijiji:)
My more
12-07-2008, 02:03 AM
Karibu kwenye technologia Mwanakijiji:)
Sijui amesikia?:rolleyes::rolleyes:
a2faces
02-06-2009, 03:52 PM
]QUOTE=mwanakijiji;191]Hivi unachukuliaje tabia ya baadhi ya vyombo vinavyojulikana kama "vya udaku" kutoa picha za watu ambao siyo "public figures" na kuelezea mambo yao ya binafsi? Je vinasaidia kupigana na tabia chafu katika jamii, je zinaingilia uhuru wa watu wengine, au ni haki ya mtu kulinda mambo yake mwenyewe?
Katika jamii kama ya kwetu na hasa penye teknolojia mpya ya mtandao ni kwa kiasi gani watu watarajie ulinzi wa mambo yao binafsi? Je kuna lolote mtu anaweza kufanya kujilinda na kuchafuana hasa kwa kutumia mtandao?[/QUOTE]
.....Maoni yangu nataka yaegemee zaidi kwenye magazeti, huenda yalianza kwa nia nzuri ya kuirekebisha jamii na ndiyo maana yalikuwa machache lakini baadae nahisi melengo yakabadilika na kuingia kwenye biashara zaidi, ninachotaka kueleza hapa ni kuwa kila mtu ana ana haki yake ya kufanya mabo yake binafsi kama hayakwazi wala kuingiliana na maslahi ya taifa au wananchi. Tena haya magazeti yana nafasi kubwa sana katika KUDUMAZA CHECHE ZA FIKRA ZA WATANZANIA matokeo yake wanakalia kufatilia fulani kafanya nini wiki hii wakati NCHI INAMEGWA KIULAINI NA MAFISADI lakini watu hawana habari masikini..........
Mpita Njia
02-07-2009, 04:13 PM
Tena haya magazeti yana nafasi kubwa sana katika KUDUMAZA CHECHE ZA FIKRA ZA WATANZANIA matokeo yake wanakalia kufatilia fulani kafanya nini wiki hii wakati NCHI INAMEGWA KIULAINI NA MAFISADI lakini watu hawana habari masikini..........
yapo magazeti ambayo yanaandika kwa nguvu zake zote kuwa nchi inaliwa, wananchi hawayanunui. lakini yapo magazeti ambayo yanaandika nani kafanya nini, yananunuliwa kwa wingi na wananchi. hapa ni nani wa kulaumiwa? magazeti, au wananchi?
Kasharu
02-08-2009, 05:48 AM
Any More, ni kweli Tanzania ni matope tu lakini nakushauri usifumbe macho maana usipofumba unaweza kuona matope yanayoelekea kukauka ukakanyaga ama siyo utakanyaga matope yaliyochanganyikana na kinyeshi!!!.
Hawa zeutamu, nadhani ni vijana wadogo tu ambao wameanza kama utani lakini kwa vile wamepata mashabiki wengi wamezidi kukua na kuvimba vichwa. Kwa sasa Bongo kila mtu hataki kabisa kupigwa/kupiga picha, maana inaoneka lolote likitokea basi vijana wamepata deal ya ku-upload picha hiyo kwenye site zao za kijinga.
Cheblack Mpingo
02-11-2009, 02:13 PM
Haya ni mambo yanayo tokea miongoni mwa wanajamii, sioni ubaya wowote kama yanawekwa wazi pale inapotoke imekuwa hivyo.
mwanakijiji
02-11-2009, 05:45 PM
yapo magazeti ambayo yanaandika kwa nguvu zake zote kuwa nchi inaliwa, wananchi hawayanunui. lakini yapo magazeti ambayo yanaandika nani kafanya nini, yananunuliwa kwa wingi na wananchi. hapa ni nani wa kulaumiwa? magazeti, au wananchi?
Unajua wakati mwingine najiuliza kama yawezekana kuwa vipaumbele vyetu tumevigeuza kinyume nyume. Sasa siyo geni watu kupenda udaku kwani hata huko majuu magazeti yenye kuchanganya "uongo njoo na ukweli njoo, utamu kolea" ndiyo ambayo yanauzika sana. La maana ni kwa magazeti hayo kujulikana kama hivyo.
Tatizo kubwa ni kuwa utaona magazeti mengi nyumbani sasa yanabakia kuwa udaku..
Daywell
05-02-2009, 12:47 PM
kwa wale ambao ni kawaida yao kupenda au kuangalia picha za ngono huwezi kuwaambia kitu juu ya ze utamu,lakini ukweli unabakia kuwa ze utamu pamoja na majarida mengine yanayofanana nayo kwa maudhui yake yanakwenda kinyume na maadili yetu watanzania kwa mtazamo wangu hayastahili kuwepo uraiani wala kwenye mtandao!
mwanakijiji
05-06-2009, 11:38 PM
Kuna watu ni lazima waripoti ze utamu maana wasipoangalia wanajikuta siku fulani wanapigiwa simu kuwa wametokea kwenye zeutamu! Sasa, hadi watu wanaogopa kupiga picha pamoja maana huwezi kujua zinaishia kwa utamu.
muwaha
05-12-2009, 10:35 PM
ze utamu afadhali imefungwa, walidhalilisha sana
Powered by vBulletin™ Version 4.0.2 Copyright © 2012 vBulletin Solutions, Inc. All rights reserved.