PDA

View Full Version : Barua toka mwana CCM-Busanda



mwanakijiji
05-21-2009, 08:42 AM
BARUA TOKA MWANA-CCM BUSANDA
?HII NI KURA YA MAONI?
Salaam!

Nikiwa ni mwanachama mwaminifu wa Chama cha Mapinduzi ninaamini uchaguzi uliopo mbele yetu ni uchaguzi ambao ni sawa kabisa na kura ya maoni juu ya mwelekeo wa jimbo letu na hasa hali ya uongozi katika jimbo hili. Ni kura inayohusu hasa kuridhika na uongozi uliowahi kuwepo kwa muda mrefu na ambao unataka kuendelea kuwepo. Hii ni kura ya maoni yetu kuhusu wapi tunataka Busanda iende na ifike chini ya Mbunge ajaye. Uchaguzi uliopo mbele yetu basi ni uchaguzi unaozidi mtu, watu, chama au mwelekeo wa kisiasa. Ni uchaguzi unaotuhusu sisi na watoto wetu na wajukuu zetu. Ni uchaguzi ambao kwa mapenzi ya Mungu umetokea wakati huu na ni wajibu wetu kutambua maana yake.

msolo
05-21-2009, 10:11 AM
Your doin a great Job.. Be blessed alwayz.

mugerezi
05-21-2009, 12:01 PM
Aisee hii barua kama ni kweli inatoka kwa mtu wa CHAMA CHA MAFISADI kwanza ongera zake lakini pia naomba atoke huko kwenye uchafu aende kwenye nuru. Ni kweli kama watawapa CHADEMA watakuwa wametenda haki kwani jamaa kweli walipigana kupigia kelele mikataba ya madini.

Hivyo kama haya mawazo niya wengi kule bisanda CHADEMA wanadeni la kuwaonyesha kuwa wao ni wana DEMOKRASIA hivyo wafanye kazi ili wakienda huko wawaeleze kama sisi tumeweza katika mwaka mmoja na kitu JE HAWA MLIOWAPA THAMANA KARIBIA NUSU KARNE WAMEFANYA NINI?

MAPAMBANO YAENDELEE MPAKA WATZ WOTE WAELEWE KUWA MATENDO NDIYO YANAYOTAKIWA KUANGALIWA SI MANENO TU

mnyilula
05-21-2009, 12:20 PM
barua ina maoni ya wazi na yanayoonesha sasa watanzania tumeaza kuelewa maana ya uchaguzi haswaaaaaaa,uchaguzi ni zaidi ya kumpigia kura mgombea flani wa chama flani,
uchaguzi ni katika sera na uwezo wa/au nia thabiti ya mgombea kutekeleza sera hizo,uchaguzi sio mazoea, uchaguzi ni uamuzi wa majaaliwa yetu ya baadae,na wenzetu wa busanda wamepata nafasi ya kuwaonesha viongozi[watawala?]wetu kile tunachokifikiria,wakituangusha tutawalaumu afu tutawaonesha mwaka ujao.
kwa sisi wanachama wa ccm tudhamilie kwa dhati kabisa kuwapunguza wanaotuharibia taswira yetu katika jamii hata ikibidi kuwanyima kura,tutawapaje wakati wametugeuka na wanachumia tumboni mwao tu badala ya kututumikia?
ipo siku tutafika, hatujachelewa kuaza safari ya maisha bora,itachukua muda lakini tutafika,
ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA,LAKINI MSINGI WAKE ULIKUWA IMARA

flein
05-22-2009, 04:14 PM
Kama kweli ni barua ya mwana CCM basi tumshukuru Mungu kuwa walau watu wameanza kutafakari uhalisia wa hali iliyopo nakuelewa. Ni vema watu wakajua kuwa huu ni wakati wa mabadiliko makubwa, tunatakiwa kuwasupport sana CHADEMA maana ndo chama walau chenye mwelekeo huku bara, tusiogope kikoje maadam kinaweza saidia kuwatoa CCM basi wate tupande gari hilo tutafika tu tuendako

flein
05-22-2009, 04:16 PM
Samahani wajumbe na wanakijiji wenzangu, hivi kuna mtu anayejua hali halisi ya busanda ikoje?vipi mwitikio wa watu japo kwa kupima mahudhurio ya mikutano ya kampeni?

Akajase
05-22-2009, 07:22 PM
BARUA TOKA MWANA-CCM BUSANDA
?HII NI KURA YA MAONI?
Salaam!

Nikiwa ni mwanachama mwaminifu wa Chama cha Mapinduzi ninaamini uchaguzi uliopo mbele yetu ni uchaguzi ambao ni sawa kabisa na kura ya maoni juu ya mwelekeo wa jimbo letu na hasa hali ya uongozi katika jimbo hili. Ni kura inayohusu hasa kuridhika na uongozi uliowahi kuwepo kwa muda mrefu na ambao unataka kuendelea kuwepo . Hii ni kura ya maoni yetu kuhusu wapi tunataka Busanda iende na ifike chini ya Mbunge ajaye. Uchaguzi uliopo mbele yetu basi ni uchaguzi unaozidi mtu, watu, chama au mwelekeo wa kisiasa. Ni uchaguzi unaotuhusu sisi na watoto wetu na wajukuu zetu. Ni uchaguzi ambao kwa mapenzi ya Mungu umetokea wakati huu na ni wajibu wetu kutambua maana yake.

Nafarijika sana kuona watu wana moyo wa uzalendo kwa kiasi hiki. Unapokuja katika kulikabili jambo lililohalisi ushabiki na umaamuma inabidi uwekwe kando, mtu halisi aonekane.

Mkazi huyu wa Busanda [Ndg mashibya] nampenda, nimetokea kumpenda kwa dhati kwa kauli zake alizotumia katika barua yake hiyo. Amechoshwa, hajaridhishhwa, kaumizwa hata akatambua kuwa katika uchaguzi huu, ni yeye na wapiga kura wenzake ndiyo wanaoitegemeza hatima ya jamii iliyochoka ya watu wa Busanda.

Ndiyo, ni wao watakao amua hatima ya Busanda ambayo matokeo yake ama ni athari chanya au athari hasi kwa jamii yote bila kujali chama rangi, jinsi au kabila la wenyeji. Waliumizwa na wanaendelea kuumizwa na maamuzi yaloyofanywa na ama wazazi wao au wakubwa zao hapo kabla, mpaka kupata BUSANDA YA LEO.

Mashibya, katika hili nakupenda kwa dhati. Natamani hata wanavijiji wa majimbo mengine wangelielewa hili na kuamua kama wewe. Ndiyo! Zipo tarafa ambazo nazijua zina access nzuri ya internet lakini hawajatumia fursa hizo katika kuona wanajikwamua katika uduni kwa sababu ya kuogopa kufanya maamuzi yanakubali kuiponya jamii nzima. Wanadanganywa kwa nguo na chakula cha siku, na kukuza matatizo ya jamii nzima.

mwanakijiji
05-22-2009, 08:11 PM
Nadhani huku tunakokwenda kuna mwamko mkubwa kuliko tunavyofikiria. Tatizo kubwa naamini haliko kwa wananchi, liko kwa wanasiasa wa upinzani zaidi.

mugagagigikoko
05-30-2009, 06:27 PM
Imekuwaje kama kuna mwamko na CCM wamechukua tena Busanda? Inawezekana estimation za upinzani zilikuwa exaggearted? Inawezekanaje eneo ambalo halina maji safi, umeme, barabara za uhakika miaka karibu 50 baada ya uhuru, na bado wanapigia kura chama ambacho kwa muda wote huo wamewasahau na kuwanyima huduma hizo muhimu? Clearly, something is wrong, somewhere. Au mimi ndiye ninaye miss something, then pls help!!!