mwanakijiji
11-13-2008, 09:21 AM
HIvi katika Tanzania kweli hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kukaa chini na kusema once and for all kuwa the comedy that is higher education is enough? Huu mtindo wa kugoma, kufukuzwa chuo, kuomba radhi, kurudi chuoni, kugoma, kufukuzwa, kuomba radhi n.k utaisha lini?
Ina maana sisi kama Taifa tumeshindwa kabisa kufikiria jinsi gani tunaweza kufanya elimu ya juu kuwa:
a. tunayomudu (affordable)
b. tunaoweza kuifikia (accessible)
c. tunayoihitaji (relevant)
d. inaoenda na wakati (timely)?
Hakuna watu wanaoweza kufikiria ni jinsi gani tunaweza kuepukana na matatizo haya ya kijinga ambayo yanajirudia rudia utadhani mkanda wa video uliokwama kwenye mashine? Je ipo haja ya kuomba wafadhili waje kutusaidia kuendesha elimu ya juu kama tulivyoomba wawekezaji waendeshe ATCL, Posta, NBC, n.k Yawezekana suluhisho liko kwa wafadhili? Au ndio tukubali yaishe tu?